Tafuta

Vatican News
Maaskofu wa Congo-Brazzaville Maaskofu wa Congo-Brazzaville  (Copyright 2009)

Congo-Brazaville,Juni 6,Siku ya utume wa Walei:Kuhamasisha Mafundisho jamii ya Kanisa

Katika fursa ya maadhimisho ya Siku ya Utume wa Walei nchini Congo-Brazaville,mnamo Juni 6,wanaandika kuwa:“Sisi Walei ambao ni mkono wa Kanisa katika dunia tunaitwa kuwa mashuhuda na watendaji wa mafundisho haya,kwa lengo kuu la kujenga ustaarabu wa upendo na mshikamano”.Kutokana na maambukizi ya Covid,ujumbe wa Cnalc utasomwa kila Parokia

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kwa nini mnakaa hapa siku nzima bila kazi? Aya hii iliyochukuliwa kutoka Injili ya Mathayo (20,6) ni mada inayoongoza Siku ya Kitaifa ya Utume wa Walei ambayo Kanisa Katoliki la Congo-Brazzaville litaadhimisha mnamo tarehe 6 Juni ijayo. Kwa mtazamo wa tukio hilo, Baraza la Kitaifa la Wakatoliki Walei (Cnalc) limetoa ujumbe ambao unawahimiza waamini wote kuhamasisha mafundisho jamii ya Kanisa. Katika ujumbe huo wanaadika kuwa: “Sisi Walei ambao ni mkono wa Kanisa katika dunia tunaitwa kuwa mashuhuda na watendaji wa mafundisho haya, kwa lengo kuu la kujenga ustaarabu wa upendo na mshikamano”.

Ni nguzo nne msingi zilizokumbukwa na Baraza ambazo ni ukweli, haki, uhuru na upendo ambazo pia ni nguzo nne za amani. Kupitia hizo, kiukweli, kanuni nyingine za mafundisho ya kijamii ya Kanisa zinaweza kutekelezwa, kama faida ya wote, maelekozo ya mali ulimwenguni, ushirika, ushiriki, mshikamano, chaguo la upendeleo kwa masikini na waliotengwa. Kwa kunukuu katika Waraka wa “Mater et magistra” unaohusu maeneleo ya masuala ya kijamii katika mwanga wa mafundisho ya Kikristo, uliyosainiwa na Mtakatifu Yohane XXIII mnamo 1961, Baraza la Walei Katoliki wa Congo-Brazzaville (Cnalc) wanasisitiza kwamba mafundisho jamii ya Kanisa yanatoa zana na njia ya kufanya kwa ajili ya kutenda kwa usalama katika mazingira yao ya kuishi, na kwa kuruhusu ujio, wa ustaarabu wa upendo na mshikamano ulimwenguni.

Mafundisho jamii, kwa dhati yanawakilisha chombo muhimu cha uinjilishaji kinachoruhusu Kanisa kutimiza utume wake wa kinabii wa kutangaza, kulaani na kuongoza, katika huduma ya jamii. Kwa sababu hizi, walei wanahimizwa kujiweka katika huduma ya mafundisho jamii ya na kuwa mashuhuda halisi. Ni changamoto ambayo inaonekana haiwezekani kushinda, lakini hakuna lisilowezekana kwa wale wanaoamini, linasisitiza Baraza la Walei wa Congo Brazzaville. Kwa kuwatia miyo wa kueneza imani Utume wa Walei unaelezea kujitoa kwa uinjilishaji kwa kutumia methali ya ile ya ndege ambao hujenga viota vyao kwa kubeba tawi moja baada ya jingine, majani baada ya mengine, bila kupoteza tumaini. Kwa maana hiyo, kwa kuwa na matumaini, walei lazima wafanye kazi kila wakati kwa amani na maelewano katika nyumba, vitongoji, mahali pa kazi, katika vikundi vya kanisa, katika jamii.

Inahitajika kutoa uhai kwa vyanzo vya mema ambavyo, kwa wakati na kwa utendaji wa Roho Mtakatifu, vitaenea ulimwenguni kote, kama madoa ya mafuta hapo ndipo parokia na vikundi vya Kanisa havitakuwa mahali pa migogoro na mifarakano na vitakuwa vituo vya malezi ya kidini na kibinadamu, vinavyolenga dhamira thabiti ya kupendelea huduma kwa Kanisa na kwa jamii. Kwa sababu ya janga la Covid-19, ambalo huko Congo-Brazzaville limesababisha, hadi sasa, zaidi ya maambukizi elfu 11 na zaidi ya vifo 150, Siku hiyo tarehe 6 Juni sherehe haitafanyika kama ambavyo ingefanyika kwa umati kama zamani walakini, katika kila parokia, ujumbe wa Baraza la Walei Katoliki(Cnalc) utasomwa.

29 May 2021, 14:59