Tafuta

Vatican News
Nchi ya Lebanon imekuwa daima na mashikamano na makaribisho ya wakimbizi wa kipalestina na Siria licha ya mgogoro wa ndani wa kijamii na kiuchumi Nchi ya Lebanon imekuwa daima na mashikamano na makaribisho ya wakimbizi wa kipalestina na Siria licha ya mgogoro wa ndani wa kijamii na kiuchumi  (AFP or licensors)

Comece:wito wa maaskofu wa Ulaya kwa ajili ya watu wa Lebanon

Kuna wasiwasi mkubwa nchini Lebanon uliotokana na mgogoro wa kisiasa kiuchumi na kijamii,kwa maana hiyo,Tume ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya(Comece wanashauri Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuingilia katika ili nchi iweze kupata suluhisho la kuwa na msimamo mpya kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kamati ya Baraza la Maaskofu katoliki wa Ulaya (Comece) wameshauri Jumuiya ya Ulaya kusaidia watu wa Lebanon katika mapambano ya kupata utambulisho na kuunda kwa upya kiungo cha kijamii cha Lebanon mbele ya mgogoro mkubwa unaoendelea katika nchi hiyo. Katika wito wao uliochapishwa tarehe 26 Mei 2021 na Maaskofu, hao umetokana mara baada ya kupokea barua iliyotumwa kutoka katika Mkutano wa Mapatriaki na maaskofu katoliki nchini Lebanon (Apecl) waliotuma kwa Kardinali Jean-Claude Hollerich, rais wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu  Ulaya (Comece ) ambayo ilikuwa inaelezea wasi wasi wao wa hati zilizojitokeza kwa sasa katika mgogoro wa kisiasa, kijamii, kiafya na kiuchumi ambacho kinaendelea kusumbua watu wa Lebanon.

Kwa mujibu wa Kanisa mahalia, ongezeko la hali mbali inaweza hatari ya utambulisho wenyewe wa nchi, ambayo imekuwa na utamaduni wa kukutana na udugu ambao unaifanya kuwa mahali pa asili yake, mahali ambamo kuna jumuiya mbali mbali za kidini na kiutamaduni. Kwa kunukuu miito mingi ya Papa Francisko, Kanisa la Lebanon linashauri jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kusaidia watu wa Lebanon ili kuhakikisha wanatunza haki zao binafsi, za pamoja na kitaifa huku wakichangia katika harakati za mapambano dhidi ya mgogoro wa kiuchumi hadi kufikia ulinzi wa kiungo cha kijamii na kuhifadhi utambulisho na upekee wa Lebanon.

Katika barua yenyewe, Mapatriaki na maaskofu katoliki wanabainisha hata ulazima wa zipo na zitabaki daima katikati ya huduma ya wazalendo wote bila ubaguzi wowote na litaendelea kufanya kazi bila kichoka kwa ajili ya wema wa wote. Maaskofu wa Umoja wa Ulaya wanaunga na kushirikiana wawasi wasi huo wa Kanisa mahalia nchini Lebanon, na kwa maana hiyo wanaelezea mshikamano wao na jamii ya Lebanon ambayo umetajirishwa na wingi wa jumuiya mbalimbali wakiwemo wahamiaji wa Kisiria na Kipalestina.

Katika mkutano wa hivi karibuni na Olivér Várhelyi Kamishna wa Ulaya akizungumzia juu  ya upanuzi  wa chanjo, Tume ya Maaskofu wa Ulaya, wamepeleka wasi wasi huo katika umakini wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, kwa kupendekeza mitindo ya dhati ili kukabiliana na mahitaji ya kijamii, kiafya, kiuchumi, kielimu kwa watu wa Lebanon. Bila uwepo wa sera za kisiasa na matendo ya kweli yanayostahili kwa umma, Kanisa na mashirika ya kidini, kama vile (Caritas Lebanon na  Œuvre d’Orient) wako wanaendelea kutoa huduma zao za kibinadamu zinazowezekana kwa  jumuiya nzima. Pamoja na hayo yote, mgogoro wa kijamii, kiuchumi, umezidi kuongezeka hata kwa sababu ya janga la virusi vya Covid-19 na ambayo kwa hakika vimegusa  maisha ya watu wengi na wao katika  utendaji wao. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Comece, Padre Manuel Barrios Prieto, zaidi amethibitisha kuwa wanahimiza na kuwatia moyo Jumuiya ya Ulaya ili kutafuta njia za ubunifu wa jitihada na washirika wa Makanisa na wadau wengine wa kidini katika maeneo ya Lebanon.

27 May 2021, 15:05