Tafuta

2021.04.27 Padre Christian Carlassare akiwa Hospitalini 2021.04.27 Padre Christian Carlassare akiwa Hospitalini 

Christian&Luca,wanaunganishwa na upendo kwa watu!

Historia ya Askofu Mteule wa Rumbek aliyejeruhiwa huko Sudan Kusini na Balozi wa Italia aliyeuwawa nchini Congo DRC inaonesha wazi maisha yao yalivyounganishwa na hisia moja,shauku na upendo kwa watu.Padre Eliseo Tacchella,mmissionari wa Comboni amethibitisha kuwa sura hizo mbili ni nguzo kwa msaada wa wote na upatanisho.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kuna uzi mwekundu ambao unaunganisha mambo ya kibinadamu ya wanaume wawili ambao waliishi  kwenye bara la Afrika ambao pamoja na mambo mazuri yaliyopo bado kuna utata dhahiri wa kisiasa na kijamii. Uzi huo ni tabia ya hisani na upendo kwa wengine ambao umeweza kuwafikia watu katika maisha yao hata kama wao hawajawahi kupata fursa ya kukutana uso kwa uso na watu hawa. Kwa maana nyingine  historia ya Padre Christian Carlassare, askofu aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa jimbo la  Rumbek, Sudan Kusini, na kajeruhiwa miguuni kwa risasi  usiku kati ya tarehe 25 na 26 Aprili 2021  na wauaji wawili akiwa nyumbani kwake, ina uhusiano mkubwa  na Luca Attanasio, aliyekuwa balozi wa Italia  aliyeuawa huko kaskazini mwa Goma, nchini Congo Drc, mnamo tarehe 21 Februari mwaka huu wakati wanatoka kwenye shughuli ya Ujumbe  wa kibinadamu wa Mpango wa Chakula Ulimwenguni.

Askofu Mteule Christian
Askofu Mteule Christian

Wote wawili wamekuwa na tabia za utu kwa kina na kama wale wanaojikana kwa ajili ya wengine, kuhamasisha amani na mshakimano, kusaidia kwa njia ya mipango thabiti, kwa watu ambao wamekutana nao katika safari zao za maisha. Wale wanaowafahamu  vizuri ni Padre Eliseo Tacchella, mmisionari wa Kikomboni ambaye amekuwa nchini Congo kwa zaidi ya miaka thelathini.  Akihojiana na mwandishi wa Vatican News , amesema kama  ndugu yake wa shirika, Christian Carlassare kweli ni mtoto wa Mtakatifu Daniel Comboni kwa sababu, baada ya shambulio hilo, hakuwahi kutumia neno 'majambazi' au 'washambuliaji' lakini ametumia neno 'watu'. Jambo jingine ambalo limemempa butwaa ni lile lenye manukato ya msamaha ambapo kwa maneno yake aliyotoa yamesikika msamaha ambao unatoka moyoni mwake kwa dhati.

Askofu Mteule Christian akiwa na Jumuiya yake
Askofu Mteule Christian akiwa na Jumuiya yake

Carlassare, mchungaji aliyevutwa na Injili: Padre Tacchella aidha emesema kuwa ni ishara dhahiri kwamba Askofu Mteule Christian Carlassare amevutwa na Injili na kwa kumpenda Yesu kwa kushirikiana na ndugu zake wa shirika lake na watu wa Sudan Kusini. Yeye amekuwa akijituma kila wakati katika upatanisho wa watu wote na baada ya shambulizi hilo alitaka ulimwengu ujue kwamba kwa miaka hii watu wake wamekuwa wakiteseka zaidi yake, wakipigwa na risasi.

Balozi Attanasio wako sawa katika mateso ya wengine: Wakati Luca Attanasio alipouawa kwenye msafara wa kutoka kutoa msaada wa  kibinadamu wa Mpango wa Chakula Ulimwenguni  (WFP) ulioelekezwa kwa mji wa Congo huko Rutshuru, lakini maisha yake yalihusika  hata katika mipango mingi ya kutoa msaada wa kijamii kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na hakupoteza fursa ili kuwekwa kwenye nyanja za kila juhudi zozote kujaribu kutafuta utulivu na amani wa kitaifa. Na ndipo hapo unaweza kuona kuwa ipo hatua nyingine muhimu ya kufananna Padre Carlassare ambayo ni utambulisho na mateso ya wengine.

Luca Attanasio
Luca Attanasio

Padre Eliseo Tacchella pia alikuwa anamjua vizuri balozi Luca kwa sababu walikuwa wanaandikiana mara kadhaa kwa sababu alimuulizia kuhusu Congo tangu alipofika nchini humo. Kwa maana hiyo kinachounganisha Luca na Christian ni shauku ya kutenda mema na hamu ya kuunda umoja.  Padre Tacchella ametibitisha kuwa ikiwa alimpigia  simu Luca Attanasio kwa shida, fulani aliitatua kwa wakati. Hata Masista wa Comboni, ambao aliwatembelea mara kwa mara, walipata msaada mkubwa kutoka kwa Balozi Luka na  ndiyo mtazamo ule ule ambao Padre Tacchella ameufananisha na kuuona kwa Askofu Mteule Carlassare kwamba Christian ni mtu wa amani, mchungaji ambaye anataka upatanisho.

Msaada usio na kizingiti: Kwa uhakika kulengwa na  kwa jaribio la kuwapiga risasi watu wenye thamani ya utu wema na hadhi ya maisha ni swali linalimsumbua Padre Tacchella kwa nini hii inatokea?  Lakini kwa kujibu amesema yeye bila shaka amepata jibu kutoka kwa  Yesu aliyesulubiwa. Mtu anayefanya miujiza, ambaye hufanya wema kwa ajili ya wote, anasulubiwa kwa sababu anavunja masilahi ya ubinafsi ya watu wengine. Kwa maana hiyo tabia ya aliyekuwa balozi Luca na Askofu Mteule Christian inakasirisha na kusumbua wengi kwa sababu inaoneshwa wazi mambo ambayo wangependa yafichike.

01 May 2021, 10:13