Tafuta

2021.04.30 Viongozi wa dini akiwemo Patriaki Pizzaballa wa Yerusalemu wamekutana na Mfalme Abdullah II wa Yordan. 2021.04.30 Viongozi wa dini akiwemo Patriaki Pizzaballa wa Yerusalemu wamekutana na Mfalme Abdullah II wa Yordan. 

Yordan,Mfalme Abdullah akutana na Patriaki Pizzaballa:Ulinzi wa maeneo matakatifu Yerusalemu

Jumanne tarehe 27 Aprili kwa Mfalme Abdullah II wa Yordani amekutana na Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu,Pierbattista Pizzaballa,Theophilus III,Patriaki Mkuu wa Kiorthodox wa Uigiriki wa Yerusalemu,pamoja na Mufti Mkuu wa Yerusalemu,Muhammad Hussain.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kuthibitisha uungwaji mkono kwa Wakazi wa Yerusalemu na kusisitizia jukumu la kihistoria na kidini la kulinda maeneo yao matakatifu ndilo lilikuwa ni lengo kuu la mkutano wa Jumanne tarehe 27 Aprili 2021 kati ya Mfalme Abdullah II wa Yordani, Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatino wa Yerusalemu, Theophilus III, Patriaki Mkuu wa Kiorthodox wa Uigiriki wa Yerusalemu, pamoja na Mufti Mkuu wa Yerusalemu, Muhammad Hussain na wawakilishi wa wa Waqf wa Kiislam wa jiji hilo.  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tovuti ya Upatriaki wa kilatino Yerusalemu, inathibitisha kuwa Mkutano huo, ulifanyika katika Ikulu ya Al Husseini ya, karibu na mapigano makali yaliyotokea Yerusalemu siku ya Ijumaa ya kwanza ya Ramadhani tarehe 16 Aprili 2021.

Katika siku za hivi karibuni kwa mujibu wa Patriaki Pizzaballa wakati wa mkutano amesema kuwa mji wao wa Jerusalem umekuwa tena katikati ya mivutano, migawanyiko na maonesho ya chuki. Kwa bahati mbaya hii sio mara ya kwanza na wanaogopa hata haitakuwa ya mwisho. Lazima waombe sana na kwa uaminifu, ili Mungu aguse mioyo migumu ya wanadamu. Wakati huo huo, kiongozi huyo alihimiza kila mtu kufanya kazi pamoja ili hali hii iishe na Yerusalemu iwe tena Jiji Takatifu, jiji la sala na maombi, makaribishaji na ulio wazi kwa watu wote.

Akielezea matashi yake mema kwa  ajili ya Watu wa Jordan  kwa karne moja ya Ufalme, iliyoanzishwa kama kanda ya Yordan mnamo 1921 na ambayo ikawa na Ufalme wa Hashemite wa Jordan mnamo 1946, Patriaki Pizzaballa amekumbuka kwamba ni muhimu kurudia kusisitizia jukumu ambalo nyumba ya  Hashemite ilikuwa nayo na jiji la Yerusalemu, kuheshimu hali ilivyo, kama dhamana ya usawa wa raia wake wa imani zote, ili waweze kupata katika maeneo yao matakatifu, sala, makaribisho na mikutano ya amani na siyo kwa kukuta uwanja wa vita. Mtazamo wa Mfalme Abdullah wa Pili, ameeleza Patriaki Pizzaballa kwamba, ni wito wake wa kufikia haki na amani ambayo imesaidia kuunda jumuiya  ambayo Wakristo na Waislamu wana uraia sawa na hatima sawa. Matumaini ya Patriaki Pizzaballa ni kwamba mfano huu utakuwa mfano kwa nchi nyingine za kanda pia.

Kwa upande wake, Patriaki Theophilus III amesisitizia juhudi za mkuu wa Jordan katika kuhifadhi utambulisho wa kihistoria wa Yerusalemu na uwepo wa Kikristo huko. Katika maneno yake alisema kuwa: “Mfano halisi ambao unaishi katika Ufalme wa Hashemite ni wa kutia moyo sana na kutuunga mkono, hasa wakati ambapo uwepo wa Kikristo katika Ardhi Takatifu, ni muhimu sana kwa uwepo wa kihistoria na amani ndani ya mkoa wetu, unaokabiliwa na changamoto mpya na kubwa”.

30 April 2021, 14:22