Tafuta

Vatican News
Wagonjwa wa Covid katika Hospitali ya jiji la Manila wameongeka Wagonjwa wa Covid katika Hospitali ya jiji la Manila wameongeka  

Ufilipino:Mei 5-8 ni siku za maombi na upendo kwa wagonjwa wa covid-19

Kanisa nchini Ufilipino limezindua siku za maombi na upendo kwa ajili ya waathiriwa wa janga la Covi-19 kuanzia tarehe 5-8 Mei ijayo katika muktadha wa maadhimisho ya maka 500 ya Uinjilishaji.Ni kusheherekea Jubilei kwa shukrani,furaha na ushikirishano.Hadi sasa maambukizi ya covid yanazidi kuongezeka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jimbo kuu la Manila nchini Ufilippino, limetangaza Siku za Maombi na upendo kwa ajili ya waathiriwa wa janga la  virusi vya Corona au Covid-19  ambapo nchini humo imewaathiri zaidi watu mia tisa elfu na zaidi ya kumi na sita elfu waliokufa. Ujumbe uliotangazwa na Msimamizi wa Kitume mahalia, Askofu mkuu Broderick Pabillo kwamba  kuanzia tarehe 5 hadi 7 Mei wataanza sala kuanza saa 12.00 jioni katika maparokia yote, Jumuiya za kitawa na katika jimbo kuu kutakuwa na kuabudu Ekaristi Takatifu, wakati huo huo itatangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari ili kuruhusu waamini wote kushiriki kiroho. Kwa mujibu wa maandishi ya Askofu  Pabillo amesema katika nyakati hizi, zimejaa matatizo na mateso mengi, zaidi ya watu wagojwa kwa sababu ya Covid-19, wapo idadi kubwa ya watu waliopoteza kazi, ambao wamelazimika kufunga shughuli zao na wana matatizo sasa ya afya ya kiakili.

Lakini mbele ya janga la namna hii, Askofu Mkuu anawashauri kwamba ni lazima kusali kwa sababu Mungu ni mwenye nguvu na anasikiliza na kupenda watu wake. Wote waunganishe mikono na sauti zao na mioyo yao katika sala na upendo kuomba msaada wa Bwana ili aweze kusaidia tatizo hili. Askofu Mkuu Pabillo aidha ameandika kwamba wapeleke altaleni machozi yao na uchungu wao wote kwa utambuzi mkubwa na matumaini ambayo yanatokana na ufufuko wa Bwana Yesu. Vile vile Msimamizi huyo wa kitume ametoa ushauri kuwa kila parokia itenge nafasi ya kufanya kumbu kumbu kwa kupamba picha za wanaparokia wote waliokufa katika mchakato wa mwaka mzima 2020 hadi sasa kwa namna ya kuweza kuwakumbuka waamini wote hao na kusali kwa ajili yao.

Na wakati huo huo Askofu Mkuu pia amewaalika kufanya matendo ya upendo kwa wale wote wenye kuhitaji. “Nawatia moyo maparokia, shule, taasisi za kitawa ili kuandaa mpango kwa ajili ya kugawa chakula na mahitaji mengine kwa wale ambao wanajikuta na matatizo, na hivyo kukuza wazo hili la msaada wa pamoja kati ya watu, kwa mfano wa Jumuiya ya kwanza ya kikristo huko Yerusalemu”. Kwa kunukuu kauli mbiu ya kampeni ya Caritas nchini Ufilippino ya 2020,  isemayo “Uchukue kile ambacho kinahitajika tu na ubakize kwa ajili ya wengine; uwape kile ambacho unaweza” Askofu Mkuu amebainisha jinsi ambavyo wametambua kuwa inawezekana, na hivyo wawe na  moyo wa ukarimu kwa kushirikisha kile ambacho wanacho hata kama ni kidogo kwa ajili ya wengine ili hata mmoja hasikose mahitaji yake.

Naye Kardinali Orlando Quevedo, Askofu Mstaafu wa Jimbo la Cotabato, amewaalika wakatoliki wa ufilippino kusheherekea kwa namna ya Shukrani, furaha na ushirikishano, kwa mwaka wa Jubilei ambayo inaendelea ya miaka 500 tangu kuanzishwa unjilishaji nchini mwao. Akizungumza mara baada ya Misa iliyoongozwa na Balozi wa Kitume Askofu Mkuu Charles Brown huko Cebu, katika kufanya kumbu kumbu hii ya Ubatizo wa Ardhi ya Ufilipino, hivi karibuni  kukumbuka tukio ambalo lilifanyika mnamo tarehe 14 Aprili 1521 katika mji huo huo, Kardinali Quevedo amewashauri waamini waadhimishe na kushuhudia kwa shauku kubwa zawadi ya imani waliyoipokea  kwa karne 5 zilizo pita. Kwa kuongozwa na sentesi ya kiinjili inayaoongoza Jubilei isemayo  “umepewa zawadi ya bure na kutoa bure”na  kuwa na zawadi ya kutoa, kama shirika la Habari za Maaskofu Cbcp linavyoripoti

Kardinali  Quevedo ametoa shukurani na kwamba Wafilipino wanapaswa kustoa shukrani na si tu kwa sababu ya baraka ya vitu kwa miaka hii 500 lakini zaidi kwa ajili ya baraka ya kiroho ambayo Mungu amewakirimia. Ikiwa hawawezi kusema asante Bwana kwa njia ya maisha , maadhimisho hayo hayatakuwa na maana yoyote, amesisitiza Kardinali kwa maana hiyo amewaalika wakatoliki wa ufilippina kufrahia kwa zawadi ambazo Mungu amewaatia na kwa namna ya pekee kufuata kwa sababu kwamba wafanyakazi wa ufilipino wamehamia katika ulimwengu wakishirikishana imani yao, si tu kwa maneno lakini kwa furaha yao katika maadhimisho ya Ekaristi.

Furaha, ngoma na nyimbo ni namna tofauti ya kuwa wakristo lilinganisha na kile ambacho kinajulikana na watu wa Ulaya, wa wakati uliopita, lakini kwa sasa wanaona fura ambayp inajionesha na wafaya kazi kutoka mbali kwa namana ya kusaidiki na kuabudu Mungu. Kulingana na hiyo ndipo Kardinali ametoa ushuri wa tatu wa kushirikisha imani. Furaha lazima ipelekee kushirikishana, si tu kwa maneno, lakini kwa njia ya kushuhuda katika maisha yak ila siku. Hii ina maana ya kuishi kwa kufuata mfano wa Yesu na nchi hicho ambacho Yesu anatusbiri kwao, amehimitimisha Kardinali Quevedo. Kati ya matukio yaliyofanyika siku hiyo ilikuwa ni kubatiza watoto sana katika uwanja mkubwa wa Cebi mbele ya Msalaba wa Magellano, uliosimikwa katika sikuku hiyo hiyo ya tarehe 14 Aprili 1521 na mfumbuzi mmoha wa kirno akiweka wakfu wa Ukristo katika nchi hiyo.

Ikumbukwe Baraza la Maaskofu wa Ufilipino (Cbcp) wameanadaa maadhimisho ya Jubilei kwa miaka 9 ya Uinjilishaji Mpya, kila mwaka umewekwa mada maalum: mafunzo fungamani ya imani  (2013), ya walei (2014), ya maskini (2015), Ekaristi na familia (2016), Parokia kama muungano wa jumuiya (2017), Ukleri na watawa (2018), Vijana (2019), Mazungumzo ya kidini (2020) na Utume wa watu ( Missio ad gentes) (2021). Katika fursa hii ya Jubileio, tarehe 14 Machi iliyopita, Papa Francisko aliongozia Misa Takatifu maalum katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican akiwa na jumuiya ya kifilipino, na wakati wa mahubiri yake alishauri Kanisa l Ufilipino kuwa Kanisa moja ambayp linajitoa zawadi ulimwenguni.

26 April 2021, 15:40