Tafuta

2021.04.11 Misa ya Papa katika Kanisa la Roho Mtakatifu in Sassia 2021.04.11 Misa ya Papa katika Kanisa la Roho Mtakatifu in Sassia 

Poland,Wiki ya Huruma:Tumeitwa kuwa na huruma

Tangu tarehe 11 Aprili ya Dominika ya Huruma ya Mungu hadi 17 Aprili 2021 ni Wiki ya Huruma ya Mungu inayoongozwa na na kauli mbiu:“Tumeitwa kuwa na huruma”, katika Kanisa la Poland ambao kiutamaduni wanaadhimisha.Kauli mbiu hii,kwa mujibu Rais wa Tume ya Kutoa msaada ya Baraza la Maaskofu,iko wazi sasa ambapo wafuasi wa Kristo wanaalikwa kuwa na huruma na wasihukumu ili wasikumiwe,wasamehe ili wasamehewe.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Kutazama jirani na mahitaji yake hasa mupungufu yake ya kiroho na mahitaji yote ya kimwili ndiyo maana ya kuwa na kuwa na huruma. Na ndiyo maana ya kuwa na huruma. Aliyekumbusha hayo ni Askofu Wiesław Szlachetka, Rais wa Tume ya kutoa msaada ya Baraza la Maaskofu wa Poland (Kep), katika ujumbe uliochapishwa tarehe 11 Aprili 2021 katika Dominika ya Huruma ya Mungu ambayo nchini Poland kiutamaduni inaanza na ‘Wiki ya Huruma’ ambayo itahitimishwa tarehe 17 Aprili 2021 ikiongozwa na kauli mbiu: “Tumeitwa kuwa na huruma”. Kauli mbiu hii, kwa mujibu wa Askofu, anasema “iko wazo sasa ambapo wafuasi wa Kristo, wote wanaalikwa kuwa na huruma, wawe huruma na wasihukumu ili wasije hukumiwa, wasamehe ili wapate kusamehewa, watoe ili watapate kupokea. Huu ni ufupisho wa kuwa na hisia kwa ajili ya wale wenye kuhitaji hasa wale wanaoishi katika matatizo na katika fadhilai hii ya huruma ambayo inawagusa sana watu wa Polanda katika mioyo ambayo inadunda moyo wa Msamaria mwema”.

Kwa kutoa mfano halisi katika hilo Askofu Szlachetka ametaja Euro milioni 8.826.800 zilizokusanywa na Caritas ya Kipoland tangu mwezi Machi 2020 hadi leo hii. Walitozitoa walikuwa ni raia binafsi, makampuni binafsi na ya serikali, kwa ajili ya kusaidia kupitia mipango 182 ya ufadhili wa zaidi ya watu 300,000 waliokumbwa moja moja na na janga la Covid-19. Kwa namna ya pekee wazee, madaktari, watoto ambao ndiyo kiini cha mipango ya hisani, na pia kuelekeza kwa wale wasio kuwa na makazi, vile vile hospitali, nyumba za kutunza wazee mahali ambamo wametoa zawadi za mashine za kupumulia, vitanda, barakoa, glavu na vifaa vyote vya kujikinga. Kwa upande wa wadogo kinyuma chake walinunua zaidi ya Komputa 400 za mikono ili kusaidia mafunzo ya mbali, pamoja na ufadhili wa masomo, kwa wanafunzi kuanzia 500. Yote hayo shukrani hata kwa watu wa kujitola ambao wamefana jitihaza za kutoa msaada kwa kila aliyekuwa na mahitaji, amesisitiza Askofu huku akitoa shukrani za dhati.

Lakini pamoja na matatizo ambayo wameishi nchini Poland, mahali ambapo dharura ya kiafya imesababisha hadi leo zaidi ya maambukizi milioni mbili na zaidi ya vifo 58,000, Caritas ya Kitaifa haikusahau Nchi hiyo ambayo inapambana na matatizo mengi, kama vile ukosefu wa maendeleo kiuchumi, ukosefu wa miundo mbinu ya kitibabu, ukosefu  wa usalama kijamii. Kwa Mujibu wa Askofu Szlachetkaametaja hasa sehemu nyeti ya nchi nyingine kama vile Siria Iraq na Lebanon mahali ambapo  Kanisa wameanzishampango wa kihisani uitwao “ Familia kwa familia  ambao shukrani kwa mchango wa  watu 20,000 wameweza kukusanya zaidi ya Euro milioni 13.

Kwa kuongezea, wakati wa Wiki ya Huruma, kiongozi huyo alihimiza waamini “kuwaombea wale wanaohitaji. Hata kumwombea jirani yetu ni moja wapo ya kazi za huruma, kwa sababu huruma ina maana ikiwa tu inatokana na  upendo”. Wiki ya Huruma ilianzishwa mnamo 2013 na Baraza la Maaskofu wa Poland  (Kep), ambayo inakusudia kuhamasisha waamini kwa ajili ya mahitaji ya wengine. Asili yake, hata hivyo, ilianzia mnamo tarehe 23 Februari 1937ambapo katika mwaka huowalifanya Kongamano  kwanza kitaifa la wakurugenzi wa Caritas wa majimbo ya Poland , ambalo liliamua kuandaa “Siku ya Huruma. Ilisimamishwa wakati wa Vita vya Pili vya Kidunia na matukio kama hayo yakaanza tena mnamo  1945 hadi 2013, mwaka ambao Wiki hii ilipata kuwa ya kitaasisi. Wakati wa mpango huo, maparokia yote ya kitaifa yanaweza kuanza shughuli za kihisani na kuandaa sherehe maalum kulingana na mpango maalum uliopendekezwa na maaskofu.

16 April 2021, 14:40