Tafuta

Vatican News
2020.08.06 padre Giorgio Marengo, Mongolia 2020.08.06 padre Giorgio Marengo, Mongolia  (Afmc (Archivio fotografico Missioni Consolata))

Mongolia:Pasaka inafanyika katika zizi dogo na hai!

Katika nchi ya Asia mahali ambapo ni karibu ya wakatoliki 1300 waliogawanyika katika Parokia nane na ambazo kwa sasa hataungana katika ibada na wala mikutano ya kidini kwa sababu ya janga la Covid-19. Msimamizi wa kitume wa Ulan Bator mji mkuu wa Taifa amsema katika mahojiano kuwakuna huzuni lakini hata matumaini kwa maana watu wako tayari kubabiliana. Kanisa la Mongoli limeanza shughuli ya uinjilishaji miaka 29 tu iliyopita.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Pamoja na janga la covid-19 kusababisha kufungwa kabisa kwa maeneo ya Ibada na kusitisha mikutano yote ya kidini, nchini Mongolia wataweza kuishi kwa uhai siku kuu ya Pasaka, inayobeba upendo na tumaini. Ndiyo maneno ambayo  yamesikika katika sauti ya Mwakilishi wa Kitume wa Ulan Bator, mji mkuu wa Nchi hiyo ya Kati Padre  Giorgio Marengo,wakati wa mahojiano na Vatican News, ambaye kwa utulivu ameeleza kuwa kati ya waamini upo kidogo huzuni,  lakini wakati huo huo wanaelewa vema dharura iliyopo mbele yao na watambua muktadha huo na ni  wenye uwezo wa kukabiliana na matatizo kwa roho ya pamoja.

Katika kipindi hiki cha Pasaka, wamekwisha andaa vema kutumia mitandao ya kijamii , ambayo kwa sasa ndiyo njia pekee ya kutoweza kupoteza jumuiya na kuifanyaibaki imara katika kuwasiliana. Kila siku, amesema wamefikiria kutangaza moja kwa moja hata maadhimisho ya Ekaristi zitakazofanyika. Kwa kuongezea amesema ni vema kuona jinsi watu wanavyosali kwa moyo huku wakiungana kiroho.  Hata hivyo amebainisha kuwa licha ya hayo wao wanao uwezekano wa kwenda kuwatembelea familia katika nyumba zao na wakati mwingine hata kuadhimisha pale ekaristi, kwa maana hiyo inageuka kuwa misa ya nyumbani.

Nchini Mongolia kuna wakatoliki 1,300 tu ambao wamegawanyika katika Parokia nane kitaifa, parokia 5 ziko katika jiji na nyingine 3 ziko nje ya mji. Kanisa hili linajumuisha hata jambo moja ambalo amesema halipaswi kusahuliwa au kuwekwa pembeni balo ni tatizo la uinjilishaji, kwa mujibu wa Askofu Marengo.  Taifa hili ni kubwa mara tano ya Italia, lakini linahesabu milioni 3 tu  ya wakati wote.  Siyo rahisi kwa makuhani, wamisionari kike na kiuke wa eneo hilo la kitume kuchunga zizi hilo dogo, amesisitiza

Kinachohitajika ni ubunifu ambao umewekwa katika mifumo mipya sasa ili kuweza kukaa nao karibu kila mwamini. Wameanzisha badhi ya mafunzo kupitia katekesi ambazo zinaendana vema na hali halisi ya dharura kama lile la sasa. Vile vile Wameandaa makundi ya watu watano, kulingana na kidondi hiki cha kidharura na vizuizi, ambao wanaanda maandiko na kutengeneza video ambazo zinatumwa kwa makatekisita. Kwa hakika mchanganyiko wa majukwaa ya kidijitali na mikutano ni muhimu.

Kanisa chini Mogllia lina miaka 29 tu ambalo limeazishwa na Uinjilishaji katika mwanga wa jua, anasema Padre  kwamba kwanza katika Nchi hiyo kulikuwa na kilio cha udikteta wa kikomunisti uliodumu kwa miaka 70. Watu wa kwanza waliowasiliana na wamisionari waliofika kwa miaka hiyo. Kwa maana hiyo bado anasema wanahisi kama hali halisi iliyoandikwa kwenye Kitabu cha Matendo ya Mitume kwa sababu bado wako mwanzoni katika hatua za kwanza za utangazaji wa Injili huku ndani ya muundo wa kijamii wenye aina nyingine za kidini. Changamoto kama hizo lakini zimeongezeka na wakati huo huo za kushangaza, hasa kwa kutazama idadi inavyendelea kuongezeka kwa kushangaza na kuweza kuwasindikiza yeye binafsi waamini katika kugundua Injili ya Bwana. Na furaha yake kubwa ni ile ya kuweza kugundua kuwa ni ndugu katika Kristo.

02 April 2021, 15:45