Tafuta

Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Malaika  huko Los Angeles, Marekani Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Malaika huko Los Angeles, Marekani  

Marekani:Uhuru wa kidini ni haki msingi

Mungu Baba yetu aliumba kila mwanadamu kwa utakatifu na hadhi,haki na wajibu sawa.Sisi sote tumeitwa kuunda familia moja ya wanadamu,ambayo iishi kama kaka na dada.Hivyo ni muhimu Wakatoliki,kama wafuasi wa Kristo,wadumishe utambulisho wao wa Kikristo wakati wanafanya kazi kwa ajili ya wema wa jamii.Amesema hayo Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Marekani Askofu Mkuu José H. Gomez,Jimbo Kuu Katoliki la Los Angeles.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Uhuru wa kidini ni haki ya msingi wa  kulinda ambao Wakatoliki wamealikwa kusisitizia. Amesema hayo Askofu Mkuu  José H. Gomez, wa Jimbo Kuu katoliki la Los Angeles na rais wa Baraza la  Maaskofu Marekani (Usccb), akizungumza tarehe tarehe 15 Aprili 2021, katika Mkutano Katoliki wa Minnesota, uliofanyika kupitia mtandao. Hotuba yake ililenga hasa, juu ya maono ya Kanisa ya haki  kijamii na wema wa wote, akirejea katika Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko wa Fratelli tutti yaani wote ni Ndugu, kuhusu Udugu na Urafiki kijamii. “Mungu Baba yetu aliumba kila mwanadamu kwa utakatifu na hadhi, na haki na wajibu sawa; sisi sote tumeitwa kuunda familia moja ya wanadamu, ambayo inatakiwa kuishi kama kaka na dada. Kwa njia hiyo, ni muhimu kwamba Wakatoliki, kama wafuasi wa Kristo, wadumishe utambulisho wao wa Kikristo wakati wanafanya kazi kwa ajili ya wema wa jamii. Kanisa sio chama cha kisiasa na sisi sio wanaharakati, lakini kama Wakatoliki tunaanzia na msingi wa dhana maalum juu ya kusudi la jamii, maana ya maisha na furaha ya mwanadamu.

Askofu Mkuu Gomez amesisitiza, kwamba kwa bahati mbaya, siasa na utamaduni wa leo hii ni wa kidunia, kiasi kwamba kuwanakuwapo na udhibiti wa maoni ya Kikristo kwenye wavuti na mitandao ya kijamii, pamoja na kutengwa kwa waamini ambapo husababisha wasiwasi katika maeneo mengine ya muktadha wa umma. Askofu Mkuu ameeleza kuwa “hizi ni tabia ambazo zinakataa kanuni msingi za waanzilishi wa Marekani kulingana na ambazo ahadi za taifa za usawa na uhuru wa binadamu haziwezi kudumishwa bila misingi thabiti ya kidini na maadili. Wakati unapo poteza maana ya Mungu, basi maana ya kweli ya maisha ya mwanadamu na wema wa kawaida wa pamoja  unapotea kwa sababu bila Mungu, siasa hupunguzwa kuwa mapambano ya madaraka kati ya maslahi yanayoshindana, na gharama kubwa hiyo hulipwa kila wakati na maskini na wanyonge ambao wanateseka mikononi mwa wenye nguvu na wenye upendeleo”,  rais wa Baraza la la Maaskofu Katoliki Marekani (Usccb) ameweka bayana hilo.

Kwa maana hii, Askofu Mkuu Gomez amewahimiza Wakatoliki kusisitizia juu ya umuhimu wa haki ya msingi ya uhuru wa kidini na juu ya mchango muhimu ambao Kanisa linapaswa kutoa katika kukuza haki ya kijamii na kusaidia kuunda jamii ya Marekani. “Hatuwezi kuruhusu Kanisa lichukuliwe kama shirika la msaada au mahali pa sala tu”. Hii inahitaji ujasiri na usadikisho kwa upande wetu. Lazima tulinde haki zetu na lazima tuishi imani yetu katika maisha ya kila siku kwa furaha na uaminifu”. Na tena, rais wa Baraza la Maaskofu Marekani (Usccb) amewataka Wakatoliki kurudisha utambulisho wa wanafunzi  wa kimisionari, ili kumtangaza Kristo na kuhamasisha maono ya Mungu juu ya mwanadamu, aliyeumbwa kwa sura yake na mfano wake na kwa maana hiyo amejaliwa hadhi sawa na haki. Leo hii, hata hivyo, kiongozi huyo amebainisha kwa masikitiko,  kuwa siasa imekuwa dini mpya, lakini bila Mungu ni katili, isiyo na msimamo, isiyo na huruma  na matumaini, kwa sababu kumkana Mungu kunamaanisha kupoteza ukweli na kupotoka kwa mwanadamu. Kwa njia hiyo, haki kijamii ya kidunia, hata ikiwa ina nia njema, haiwezi kuunda hali zinazohitajika kwa ajili ya  maendeleo ya kweli ya binadamu”, amesisitiza.

Katika maono Katoliki, kwa dhati  haki ya kweli kijamii inahusu ujenzi wa jamii ambayo watu wake wanaweza kuwa wema, kupendana na kujali wengine. Haki kijamii sio juu ya nguvu ya kikundi au kupatikana kwa bidhaa nyingi, lakini ni azima iambatane na fadhila za kibinadamu, huruma na msamaha. Askofu Mkuu wa Los Angeles vile vile akiendelea amesisitiza kwamba “kwa mtazamo huu, madhumuni msingi ya serikali na siasa lazima yawe ni kulinda utakatifu na hadhi ya mtu huyo, tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo chake  asili. Na jukumu la Wakatoliki lazima liwe lile la kuleta maono haya katika mazungumzo ya umma, kuamsha tena kwa kila mtu ule ufahamu wa upendo wa Mungu, kuwa wajenzi wa amani na upatanisho. Na kwa njia hiyo kamwe, wasiamini  chuki au dharau, maneno ya chochezi, kamwe hakuna  wengine kama maadui, hata kama wengine wanatutendea isivyo haki au kututukana”, amesisitiza Askofu Mkuu  Gomez. Kama Wakatoliki, ni lazima tumuache Mungu ahukumu kwa sababu kazi yetu ni kumtangaza Kristo, kuwapenda maadui zetu na,kuwa  mfano na ushuhuda, kusaidia jamii yetu kuelewa kuwa sisi sote ni kaka  na dada, watoto na binti wa Mungu, walioumbwa na hadhi sawa na washiriki  hatima ya kawaida na pamoja  na matumaini ya pamoja ”.

Ikumbukwe kwamba Mkutano Katoliki wa Minnesota hapo awali ulitazamia kufanyika kama mkutano wa ana kwa ana. Baadaye iliamuliwa kufanyika kwa njia ya mtandao sababu ya mivutano ambayo haikuweza kuepukika huko Minneapolis kufuatia na kifo, cha Mwafrika kijana  wa Marekani  Daunte Wright mnamo tarehe 12 Aprili,  Mauaji yake, ambayo yalifanyika nje kidogo ya mji, na kussababisha maandamano makali dhidi ya polisi. Kufuatia na Tukio la kusikitisha ambalo Askofu Mkuu  Gomez pia amesisitiza kuwa: “Tunaomba amani, haki, kwa familia za watu wote waliohusika katika vurugu za hivi karibuni. Jueni kwamba Kanisa linaendelea kujitoa uongozi wa muda mrefu katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi Marekani yote”. Ubaguzi  ni dhambi kubwa, ugonjwa wa kiroho na ukosefu wa haki kijamii. Lazima tuwe pamoja kama Kanisa moja ili kuondoa uovu huu kutoka mioyo yetu, kutoka kwa mioyo ya majirani zetu na kutoka katika miundo ya jamii yetu ”amehitimisha.

Ikifafanuliwa kama sauti ya sera ya umma ya Kanisa Katoliki, Mkutano Katoliki wa Minnesota unaunga mkono Huduma ya maaskofu kwa serikali katika maeneo fulani maalum katika: kushirikiana na viongozi wa kisiasa kuunda sheria kwa ajili ya utunzaji wa heshima ya binadamu na faida ya wote; elimu katoliki katika maadili na adili muhimu katika sera ya umma; uhamasishaji wa jumuiya ya Wakatoliki ili kufanya sauti yake isikike katika jamii. Kutoka Baraza la Maaskofu wanajumuisha maaskofu, mapsdre, watawa, wamini na wengine walei kutoka Minnesota, wanaowakilisha majimbo sita mahalia kama vile: Mtakatifu Paulo na Minneapolis, Crookston, Duluth, New Ulm, Mtakatifu Cloud na Winona.

UHURI WA KIDINI NI HAKI MSINGI
17 April 2021, 15:40