Tafuta

Wakimbizi huko Kenya Wakimbizi huko Kenya  

Maaskofu Kenya wanapinga kufungwa kwa Kambi za wakimbizi

Maaskofu nchini Kenya wanapinga kufunga makambi ya Kakuma na Daadab na hivyo wanasema hakuna kuwarudisha wakimbizi kwa nguvu katika nchi zao za asili.Badala yake Serikali inatakiwa kuzingatia nafasi yake na kuwatunza wakimbizi wote kwa umakini hasa wakati huu wa kipindi cha janga la Covid-19,wakati binadamu anajikuta anakabiliana na changamoto kubwa kiuchumi na kisaikolojia.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Baraza la Maaskofu nchini Kenya (KCCB) wakati wakipinga kuiomba Serikali yao isifunge Makambi ya wakimbizi huko Kakuma na Daadab wanathibitisha kuwa “Serikali inatakiwa kuzingatia nafasi yake na kuwatunza wakimbizi wote kwa umakini hasa wakati huu wa kipindi cha janga la Covid-19, wakati binadamu anajikuta anakabiliana na changamoto kubwa kiuchumi na kisaikolojia”. Katika uthibitisho huo uliotiwa saini na Askofu Mkuu Philip Anyolo, wa Jimbo Kuu Katoliki la Kisumu na Rais wa KCCB, maaskofu wa Kenya wanaelezea wasiwasi wao wa kurudisha wakimbizi kwa kulazimisha. “Katika kambi ya Daadab wasomali ndiyo wengu: kwa mujibu wa sheria kimataifa wakimbizi wa kimataifa wanaweza kurudi nchini mwao ikiwa serikali umeanzishwa tena demokrasia inayoheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria”.

Serikali ichukue hatua ya kuwasaidia wakimbizi

“Kwa sababu ya janga la Covid-19, kaka na dada zetu ambao wanaishi katika kambi wamekuwa katika mazingira magumu”, wanathibitisha Maaskofu wa Kenya ambao wanaomba kuchukua hatua za kiafya ili kuhakikisha ulinzi wa zaidi ya wakimbizi 400.000 wanaoishi katika makambi ya Dadaab na Kakuma. Ili kupata suluhisha la masuala hayo, Maaskofu wanaomba serikali kufanya mazungumzo na sehemu husika ili kupata suluhisho la kudumu kwa ajili ya wakimbizi na wakati huo huo kutoa msaada kwa wale ambao wanaamua kwa hiari yao kurudi katika Nchi yao ya asili.

Kambi za Kakuma zilianza mnamo 1992

Kambi ya wakimbizi ya Kakuma Kaskazini Magharibi mwa Kenya iliundwa mnamo 1992. Mwanzoni ilikuwa na wakimbizi kutoka Sudan ambao walifika hapo wakitokea Ethiopia na Somalia. Dadaab ni kambi iliyoko katikati mashariki ambayo kwa muda mrefu imekuwa kambi kubwa sana ulimwenguni na kiukweli inajumuishwa pamoja na makambi mwengine.  Makambi matatu ya kwanza yaliundwa mwanzoni miaka ya 90. Makambi mengine baadaye ameongezeka kuanzia mwaka 2011 , kwa sababu ya mogogoro wa vyakula katika Pembe ya Afrika. Na zaidi, Somalia, Sudan ana Ethiopia, makambi mawili yanayokaribisha wakimbizi hata kutoka Tanzania, Uganda, Sud Kusini na Jamhuri ya Congo.

UNHCR ina wasi wasi mkubwa juu ya wakiimbizi hawa

Akinukuu uingiaji wa kigaidi katika miundo hii mnamo Novemba 2016, serikali ya Nairobi ilitangaza nia yake ya kuifunga, bila kutekeleza uamuzi huo, ambao tayari ulikuwa unapingwa vikali na Maaskofu. Walakini, mnamo Machi tarehe 24 mwaka huu, Katibu wa Baraza la Mawaziri la Mambo ya Ndani,  Fred Matiang'i alitangaza azma ya serikali kufunga kambi za Dadaab na Kakuma, akimpatia Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa (UNHCR) wiki mbili ya kuwakilishaji wa  mpango huo.  Kw sasa UNHCR ina wasiwasi juu ya athari ambayo uamuzi huu utakuwa nayo juu ya ulinzi wa wakimbizi nchini Kenya, pamoja na muktadha wa janga la Covid-19 linaloendelea. Vile vile shirika hili wamesema kuwa wataendelea na mazungumzo yao na maafisa wa Kenya juu ya suala hili. Hata hivyo tarehe tarehe 8 Aprili Mahakama Kuu ya Kenya ilisitisha kwa muda uamuzi wa serikali wa kufunga miundo hiyo miwili

15 April 2021, 14:31