Tafuta

2021.04.03: Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu, Yerusalemu Mkesha wa Pasaka 2021 2021.04.03: Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu, Yerusalemu Mkesha wa Pasaka 2021 

Katika Pasaka kila kitu kinatimizwa na kupyaishwa katika mateso,kifo na ufufuko!

Ufufuko wa Bwana uliwashangaza wengi waliokuwa karibu nao.Ilimtokea Maria Magdalena ambaye alimpenda kwa moyo wake wote,kwa roho yake yote.Ni jambo la kushangaza kwa Petro ambaye pia alimtambua kama Kristo,Mwana wa Mungu na alikuwa amepokea jukumu la kuwathibitisha ndugu zake katika imani.Licha ya kusoma Injili mara nyingi labda bado hatujaelewa kuwa kila kitu kinatimizwa na kufanywa upya hasa katika mateso kifo na ufufuko wa Yesu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Msiogope! mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; Amefufuka; hayupo hapa! Hapa ndipo mahali walipokuwa wamemweka.”  (Mk 16.6). Tangazo hili, lililotolewa na malaika, hapa kaburini, asubuhi ya Pasaka, ni jambo la kushangaza sana kwamba hata kwa wale ambao walimjua na kumfuata Yesu kwa karibu zaidi. Ni jambo la kushangaza kwa Maria Magdalena, ambaye alikuwa ameponywa na Yesu na kurudishiwa na yeye maisha halisi. Ndiyo maneno anayoanza nayo Padre Fancesco Patton OFM;,  Msimamizi wa Nchi Takatifu katika ujumbe wake kwa njia ya Video ambao ameutoa katika furaha hii ya Siku Kuu ya Ufufuko wa Bwana 2021.

Katika ujumbe huo Padre Patton anasema ilimtokea hata Maria Magdalena ambaye alimpenda kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote na kwa nguvu zake zote. Ni jambo la kushangaza kwa Petro, ambaye pia alimtambua kama Kristo, Mwana wa Mungu na alikuwa amepokea jukumu la kuwathibitisha ndugu zake katika imani. Ni jambo la kushangaza kwa Yohane, mwanafunzi mpendwa, ambaye alikuwa amekaribia kifuani mwake Yesu ili kuweza kuchota kwa  kina siri yake na upendo wake. “Hayupo hapa, amefufuka!,” “Kifo kimeshindwa!”

Hiki ni kile ambacho kiukweli kipo katika  kina cha mioyo yetu kila mmoja wetu anatamani, kwa sababu tunahisi na tunajua kuwa tumeumbwa kwa ajili ya  maisha, na kwa maisha kamili, yenye furaha na milele. Ni shauku ya maisha ambayo tunabeba ndani. Shauku kwamba mwaka huu umekuwa na changamoto ngumu ambayo mara nyingi na ulimwenguni pote, tulihisi janga linatuzingira kama adui asiyeonekana, wakati tuliona watu tunaowapenda wanaugua virusi hivi ambavyo vimechukua pumzi na nguvu, na wakati wapendwa wetu wengine wamemezwa na kifo na wakafa wakiwa peke yao.

Ujumbe wa Pasaka wa Padre Patton Msimamizi wa nchi Takatifu

Padre Patton anasema “Shauku ya maisha ambayo katika sehemu nyingi za ulimwengu tayari ilikuwa katika mgogoro kabla ya janga, ya  vita na njaa, mizozo ya kibinadamu, shida ya ubinadamu na utandawazi wa kutokujali, ya  mitindo isiyo ya kibinadamu ambayo ni ya kupigwa marufuku. Kama macho ya wanafunzi, hata macho yetu yako  pia hatarini kufunikwa na maoni na kuamini kwamba kifo kina nguvu kuliko uhai na ndio mwisho wa kila kitu. Na licha ya kusoma Injili mara nyingi, labda bado hatujaelewa kuwa kila kitu kinatimizwa na kufanywa upya hasa katika mateso kifo na ufufuko wa Yesu.

Padre Patton akiwa katika mahali ambapo Yesu alifufuka kweli anasema kuwa:“Walakini, hapa mbele ya kaburi hili tupu, lazima kupaza sauti, “Kifo kimeshindwa! Kwa sababu Yesu amefufuka. Hapa ndipo mahali walipokuwa wamemlaza”. “Kifo kimeshindwa!” kwa sababu upendo una nguvu kuliko kifo. Upendo usio na mwisho ambao Yesu aliishi ili kuishi kwetu kwa kibinadamu, na kifo chetu, ni nguvu kuliko kifo. Ana uwezo wa kujenga tena maisha yetu mafupi haya ili yawe ya milele, na kujaza mwili wetu huu wa kufa na Roho wake Mtakatifu ili tuweze kuingia katika maisha yake ya kimungu.

Katika alfajiri ya ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu, kifo kilishindwa milele. Na sihitaji kujua kitu kingine zaidi. Sihitaji tena kuona au kugusa kaburi hili tupu, ambalo kwa miaka elfu mbili limeshuhudia kwambaYeye yuko hai na kwa miaka elfu mbili anatangaza, kwamba pamoja Naye, mimi pia, wewe pia, tutakuwa hai milele. Pasaka njema! amehitimisha

04 April 2021, 14:51