Tafuta

Vatican News

Kameruni:Moringa ni mti wa majani na mbegu zenye protini katika mboga,madini na vitamini!

Katika historia ya “Laudato si’” tunagundua nchini Kameruni kuhusu utunzaji wa kazi ya uumbaji unavyoweza kugeuka kuwa jitihada dhidi ya utapiamlo.Na hii ni kuhusu Mti wa Moringa ambao majani na mbegu zenye protini katika mboga,madini na vitamini,zinaweza kusaidia watoto na mama wajawazito kukidhi mahitaji ya lishe kwa mujibu wa maelezo ya Mmisionari wa Pime ambaye ni mratibu wa Caritas,Jimbo la Yagoua nchini Kameruni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni kuanzia na uzoefu mahalia na ishara thabiti, yaani kuanzia chini ili kujaribu njia mpya katika mapambano dhidi ya janga la utapiamlo barani Afrika. Kutokana na  jitihada za Ndugu Fabio Mussi, ambaye ni mratibu wa Caritas wa Jimbo la Yagoua, katika mkoa wa Kaskazini mwa Camerun, anaelezea kwa njia ya video jinsi ambavyo alishauriwa moja kwa moja kupitia  Waraka wa Papa Francisko wa 'Laudato si',  na wito wa Papa  wake w amara kwa mara wa kufanya  hatua zinazowezekana kudhibitisha kwamba kila  binadamu bado ana uwezo wa kuingilia kati vizuri, katika kulinda nyumba yetu ya pamoja na kufanya, ishara za ukarimu, mshikamano na utunzaji. Huyo ni mmisionari mlei wa PIME, ambaye asili yake ni kutoka Italia ya Kaskazini, amekuwa akifanya kazi kwa miaka 11 katika nchi ambayo 39% ya idadi ya watu wanaishi chini ya umaskini wa utisha.

Njaa, mabadiliko ya tabianchi, kukosekana kwa utulivu katika eneo linalozungumza Kiingereza, unyanyasaji dhidi ya watoto, familia na jamii nzima, uvamizi wa wapiganaji wenye msimamo mkali wa Kiislamu wa Boko Haram unaoendelea kutishia idadi ya watu na uchumi mbaya wa Camerun, hasa kilimo. Katika eneo la Kaskazini mwa Camerun, ameelezea mmisionari huyo wa Italia kuwa wana kiwango cha papo hapo au kikali cha utapiamlo ambacho kinazidi wastani wa kitaifa. Nchini humo, mikoa 6 kati ya 10 ina kiwango cha udumavu na utapiamlo wa muda mrefu wa zaidi ya 30%: katika mkoa ambao Ndugu huyo anafanya kazi ni 40%. Katika eneo ambalo pembezoni linaonekana kuwa limepunguza athari za janga la Covid-19, ambalo kwa hali yoyote sasa linarekodi wimbi la pili, magonjwa kama malaria na kipindupindu ni magonjwa ya mara kwa mara, amesema mmisionari huyo, na kuna hata visa vichache vya uti wa mgongo.

Akiendelea kusimulia mratibu wa Caritas wa Jimbo la Yagoua  amesema:“Kwa kuchunguza hali na viwango vya utapiamlo katika maeneo yetu, tuligundua kwamba mfumo bora unaostahili  kwetu sasa ni ule wa usambazaji wa virutubisho vya chakula, ambavyo kwa sasa vinaingizwa. Lakini tukajiuliza je hali hii ya mambo inaweza kuendelea kwa muda gani, kwa sababu virutubisho hugharimu na ni ngumu kutufikia kwa upande wetu. Kuna mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ambayo huingilia kati kupambana na uhaba wa chakula na utapiamlo, lakini akauliza , wakati mashirika haya yataondoka, bado itawezekana kuendelea na vita dhidi ya utapiamlo na bidhaa zile zile zinazoagizwa kutoka nje? Kwa kufanya uzoefu wa mahali hapo na nchi nyingine za jirani ikaonekana kuwa kuna suluhisho la kienyeji, yaani la asili. Inawezekana zaidi kwetu kutumia mmea wa kienyeji, ulioenea sana, lakini hauthaminiwi: na unaitwa “moringa. Ni mti ambao una virutubisho vyote kuwapa watoto viwango vya lishe, bila gharama kubwa”. Moringa, amefafanua mmisionari huyo, ni mti uliotokea India, lakini upo hapo kwa miongo kadhaa. Unastawi katika joto la kitropiki na hata ukame. Pia hukua kwa haraka na hutoa majani na mbegu zilizo na protini nyingi za mboga, madini na vitamini.

Kwa maana hiyo, katika kuhimiza kilimo na uzalishaji wa ndani, tuliona matokeo bora yanaweza kupatikana. Kwa kuongezea, majani haya au nafaka hazihitaji kufanyiwa chochote zaidi ya kuacha tu zikauke na kutumia kwenye chakula, ama kwa kuchanganya na vyakula ambavyo vinapikwa, au kwa kutumia kama chai. Kutoka katika takwimu walizo nazo mkononi, iliyojaribiwa katika nchi nyngine za Kiafrika na kuthibitishwa na vyuo vikuu mbali mbali, itatosha kwa watoto wenye utapiamlo kutibiwa na kijiko cha unga cha moringa kila siku, kwa miezi mitatu, na kuweza kupata nguvu na uzito.  FAO inaripoti kuwa majani ya moringa yana protini nyingi, vitamini A, B na C na chumvi za madini na inapendekeza matumizi yao kwa wajawazito, mama wauguzi na watoto wadogo.

Mratibu huyo wa Caritas amesema: “Tuligawanya mbegu zilizozaa mimea takribani 500 ya moringa: tulikusanya majani na kuyasaga kuwa unga, kisha kuandaa mifuko 50g, ambayo gharama yake itakuwa faranga 500 za (Cfa), ambayo ni senti 80 za euro. Tangu Septemba 2020, tulianza usambazaji wa bure kwa wanawake wengine ambao wanakuja katika vituo ambavyo tunafanya kazi, vituo vya afya vinavyohamasishwa na Kanisa Katoliki. Akina mama walio na watoto walio na shida ya utapiamlo wanaweza kupokea miche na mbegu za kupanda ili kupanda na kupata bidhaa wenyewe, kuwa uhuru". Mratibu huyo anasema "Kwa sababu ni muhimu kwamba maarifa juu ya matibabu ya dharura fulani, kama vile utapiamlo, yapitishwe kwa wanawake hawa ambao, licha ya kuwa hawajui kusoma na kuandika, wanajua vizuri kuwa kuwatendea watoto wao vizuri kunamaanisha kuhakikisha matarajio bora ya maisha kwa wote”. Unaweza kusikiliza pia juu ya historia hii:

MTI WA MORINGA WENYE PROTINI,MADINI NA VITAMINI
14 April 2021, 12:11