Tafuta

Vatican News
2021.04.09 Askofu Mkuu akiwa na makuhani baada ya wengine kupewa daraja la ukuhani Jimbo Kuu Katoliki Bamenda/Camerun 2021.04.09 Askofu Mkuu akiwa na makuhani baada ya wengine kupewa daraja la ukuhani Jimbo Kuu Katoliki Bamenda/Camerun 

Kameruni:Kazi za Kanisa mahalia na msaada wa Vatican

Kanisa Katoliki nchini Kameruni linaweza kujifikiria kama kiungo cha kurahisha mazungumzo.Kwa maana wao ni kama wawakili kati ya sehemu zote mbili hata kama ni wao wanaopaswa kusuluhisha na wanaweza kufanya hivyo kwa kuzungumza pamoja.Ni maneno ya Askofu Mkuu wa Bamenda akielezea hali ya mizozo iliyoibuka tangu 2016 hadi leo hii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika taarifa ya Askofu Mkuu Andrew Nkea Fuanya wa jimbo kuu la Bamenda nchini Kameruni akielezea juu ya hali halisi ya nchi hiyo kutokana na mzozo wa ndani amethibitisha kuwa “Kanisa Katoliki nchini Kameruni linaweza kujifikiria kama kiungo cha kurahisha mazungumzo. Kwa maana hiyo sisi ni kama wawakili kati ya sehemu zote mbili hata kama ni wao ambao wanapaswa kusuluhisha na wanaweza kufanya hivyo kwa kuzungumza pamoja. Eneo la Kiingereza asilimia 40 ya watu wanakiri imani ya kikristo na uwepo wetu unalenga kurahisisha amani. Tunafanya kazi sana na watu mahalia, lakini hata na wanajeshi na wapiganaji kwa sababu ya kuleta mazungumzo na yapate kushinda. Lazima isemwe kuwa kazi ya kurahihsa amani, hata hivyo imepelekea kulipa gharama kubwa kwa maana ya kupoteza maisha ya wengi au vurugu ambazo wamepata walei wakristo na makuhani”.

Askofu Mkuu amesisitizia zaidi juu ya hali ya uchungu ambayo tangu 2016 katika kanda ya wanaozungumza Kiingereza nchini humo wanapitia wakati mgumu wa mizozo, vurugu za ajabu, umaskini na vitisho. Askofu Mkuu ameeleza  hayo kwa sababu hata wahudumu wa kikanisa kama makuhani au watawa ni walengwa wa kufanyiwa vurugu hizo licha ya kuwa kama mawakili wa amani. Hali hiyo ya mizozo ya ndani  imepelekea kuunda kwa janga la kutokuelewana kwa kina. Askofu anabainisha kuwa waamini wote katika Kanisa kuanzia  na nafasi yake iliyonayo ,kumekuwapo kipindi ambacho serikali imewafikiria kama washiriki wa karibu na waasi, kwa namna kwamba wale waliojitenga waliowaona kama wanapinga serikali,  kwa sababu tu Kanisa linalaani  vikali vurugu dhidi ya raia wote.

Askofu Mkuu kwa maana hiyo  amesema: “Walakini, tunajua kwamba Kanisa la Kristo linateswa kama vile yeye mwenyewe alivyosema katika Injili kwamba “watamtesa mwalimu na watumishi wake”. Kwa maana hiyo  hii  sio hali mpya kwetu ambayo tunachagua kuendelea kulipa gharama kubwa hadi tutakapofikia amani katika mikoa yetu tunayopenda na watu wetu wapendwa”. Katika muktadha wa kimataifa Askofu Mkuu wa Bamenda amebainisha, kuwa yameundwa matarajio na matumaini makubwa baada ya  safari ya hivi karibuni ya Kardinali Pietro Parolin, ambaye alitembelea nchini Kamerun mnamo mwezi Januari mwaka huu. Katibu wa Vatican alikuwa kiongozi mwenye  mamlaka wa kwanza kutembelea watu wa maeneo la kaskazini mashariki na kaskazini magharibi mwa Kameruni tangu kuanza kwa mgogoro mnamo 2016.

Kulingana na  Askofu Mkuu Andrew Nkea Fuanya amebainisha kuwa: “Ninaamini kuwa ziara ya Kardinali inabaki kuwa hatua ya uamuzi kuelekea amani. Kardinali Parolin alikuja Bamenda kunikabidhi Palio, kama Askofu Mkuu (Metropolitan) mpya wa Jimbo Kuu, lakini zaidi ya yote kuelezea ukaribu wa Papa na watu wanaoteseka. Ilikuwa faraja kubwa kwa mapadre na maaskofu, watawa na waamini, kwa sababu Papa yuko karibu nasi”. Kardinali Parolin alifanya mkutano na makuhani na Maaskofu, ambapo ilikuwa ni msukumo mkubwa kubaki waaminifu katika utume wao na na kwa kuwatia moyo mkubwa  watu wa Mungu katika umisionari wao. Kardinali Parolin alieleza na kuonesha jinsi ambavyo Papa anafuatilia hali yetu kwa karibu sana akiwa na wasiwasi mkubwa. Licha ya vitisho vya upinzani dhidi ya wale ambao walikuwa wamekwenda kwenye mikutano, ilikuwa ni mwitikio wa idadi ya watu uliokuwa mkubwa na ulionesha bila shaka yoyote jinsi watu walivyofurahi katika nafasi hiyo ya kukutana na mjumbe wa Papa, ambaye alikuja na ujumbe wa amani. Ziara yake ilikuwa hatua muhimu katika njia ya kuelekea amani ya mikoa yetu”, amesisitiza Askofu Mkuu katika Taarifa shirika la habari za kimisionari Fides.

Kwa kuhitimisha Askofu Mkuu wa Bamenda amesema kuwa: “Ni muhimu kwetu kujua kwamba Vatican inafuatilia na inajaribu kukuza amani, ikiongea na pande zote mbili. Jitihada za Kanisa kwa ngazi ya kimataifa na kikanda mahalia ni jambo la msingi. Sisi, hapa, kama Maaskofu, tunawajulisha Vatican juu ya kila hatua na kwa maana Vatican inaweza kutoa mchango, kupitia shughuli za Maaskofu wa hapa. Idadi ya watu wana imani kubwa na Kanisa na ndio sababu vyama vingi vinatazama Vatican kama mdau anayeaminika na ambaye anaweza kusaidia mazungumzo na upatanisho”.

17 April 2021, 15:27