Tafuta

Vatican News
Kuombe watoto wasiozaliwa.Kiini ni maisha Kuombe watoto wasiozaliwa.Kiini ni maisha  (©unlimit3d - stock.adobe.com)

China,jimboni Macao:Misa maalum na kuzindua sanamu ya malaika wasiozaliwa

Askofu Stephen Lee,wa Jimbo la Macao nchini China aliongoza misa kwa ajili ya kuombea watoto wasio zaliwa kutokana na utoaji mimba. Wanawake na wasichana wengi katika mji huo wa Macao huishia kwenye duru za ukahaba hapa na pale na kwa sababu hiyo,utoaji wa mimba ni mkubwa sana,kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kanisa la Macao nchini China limeadhimisha misa maalum kwa ajili ya watoto wasio zaliwa na ambao wamekataliwa haki yao msingi ya maisha kutokana na mama zao kutoa mimba. Misa hiyo ilifanika tarehe 24 Aprili 2021 na kuzinduliwa kwa sanamu moja ikitaka kutoa maana ya kuheshimu viumbe hai wadogo Malaika na  wasio na hatia, kwa kukuza au kuhamasisha utambuzi wa kutunza maisha na utakatifu wake tangu kutungwa hadi kifo cha kawaida. Kwa mujibu wa taarifaza za habari katoliki barani Asia (UCA) sherehe hizo zilioongozwa na Askofu Stephen Lee, wa Jimbo la  Macao.

Padre Daniel Ribeiro,  Makamu wa Kanisa Kuu la Mama Yetu, jimbo la Macao  amesema kuwa  Kanisa limeadhimisha misa kwa ajili ya watoto wasio zaliwa kwa sababu linaamini utakatifu wa misha yote yakiwemo umbu lililotolewa mimba. Kwa mujibu wa Gazeti katoliki la kila wiki O'Clarim”, kwa lugha ya kireno, linasema kuwa mji wa Macao chini ya utawala maalum wa China, lilitawaliwa na wareno tangu 1557 hadi 1999, na ni maarufu kwa vituko vyake, yaani kwa bahati mbaya linajulikana kwa biashara ya kingono.

Wanawake na wasichana wengi huishia kwenye duru za ukahaba hapa na pale, na kwa sababu hiyo, utoaji wa mimba ni mkubwa sana, kulingana na vyombo vya habari vya nchini humo. Kwa kuongezea hilo ni kwamba utoaji mimba nchini China umekuwa halali tangu miaka ya 1950 na kwamba serikali inatoa njia na huduma za kuzuia mimba, pamoja na utoaji wa mimba unaochagua ngono. Jimbo la  Macao, linaloongozwa na Askofu Stephen Lee Bun Sang limegawanywa katika parokia 9, ambazo mnamo 2016 walikuwa wanahesabu wabatizwa 30,314 kati ya wakazi 646,800.

28 April 2021, 11:17