Tafuta

Baraza la Maaskofu Chad Baraza la Maaskofu Chad 

Chad:Maaskofu washauri mazungumzo na jitihada stahiki kwa ajili ya wema wa Nchi

Kwetu sisi Wakristo,njia bora kuu ya mazungumzo ni maombi ambayo yanajumuisha kubadilishana maneno na Mungu,kumweleza kile kinachotusumbua,hata ikiwa anajua,kumsikiliza kwa kutafuta jibu lake katika Neno lake.Ni kwa kung’amua mapenzi yake katika hali za maisha yetu ndipo tunaweza kutimiza.Ni ujumbe wa Maaskofu Katoliki nchini Chad katika fursa ya Siku kuu ya Ufufuko wa Bwana..

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Mbele ya muktadha wa sasa wa jamii, kisiasa, kwa ajili ya amani ya kuishi na kuwa na maendeleo ya maelewano, Maskofu Katoliki nchini Chad wametoa ushauri wa kuwa na mazungumzo ambayo yawe ya kweli na yenye kuleta matunda. Ni katika barua yao ya kichungaji kwa umma katika fursa ya Maadhimisho ya Pasaka, itakayoadhimishwa Dominika tarehe 4 Aprili 2021.  Wiki iliyopita, Baraza la Maaskofu walithibitisha kuwa amani ni kiungo msingi cha kuishi, lakini kwa wale ambao wanatawala au wanashauku ya kutawala, mapenzi halisi ya amani na hamu ya wema mkuu wa taifa ungeweza kuibuka! Katika tofauti za madhehebu ya kidini, waamini wanatiwa moyo kufanya mazoezi ya utamaduni wa kuvumiliana na wa upatanisho kwa ajili ya kurahisha kuishi kwa pamoja, wanaandika maaskofu lakini ambao, hata hivyo, wanaona hali ya wasiwasi iliyosababishwa na tabia za uchochezi na maneno ya yasiyo mazuri na makali.

Maaskofu wanatambua kwamba ikiwa kuna makubaliano juu ya tabia ya kidunia na ya jamhuri ya serikali, juu ya kutoshikika kwa mipaka ya sasa, kuhusu suala la hatari ya kijihadi na juu ya tabia nzuri ya utofauti wa kiutamaduni, vidokezo kadhaa vya tofauti hizi vinastahili kutafakariwa. Maaskofu wanasema: “Hii ndiyo kesi ya usawa wa raia kwa kuzingatia haki na majukumu yanayotokana na sheria, usimamizi wa rasilimali za nchi kwa faida ya wote, ya matumizi mabaya ya mamlaka ya serikali na ya kuchanganyikiwa kwa majukumu, ya heshima kwa nguvu za kutunga sheria, ya utendaji na mahakama, na mwishowe usimamizi wa usalama katika mizozo, uchumi, kijamii na afya”.

Aidha Maaskofu wanasema kuwa: “Kwetu sisi Wakristo, njia bora kuu ya mazungumzo ni maombi ambayo yanajumuisha kubadilishana maneno na Mungu, kumweleza kile kinachotusumbua,hata ikiwa anajua,kumsikiliza kwa kutafuta jibu lake katika Neno lake. Ni kwa kung’amua mapenzi yake katika hali za maisha yetu ndipo tunaweza kuyatimiza”. Maaskofu wanaongeza kuwa “mazungumzo yanahitaji kusikiliza na mazungumzo kati ya pande mbili, inahitaji ukweli, utafutaji wa wema wa wote, unyenyekevu na uwezo wa kutambua kuwa mwingine anaweza pia kuwa mbeba ukweli”. Kwa maana hiyo mwaliko wao ni “kuinua macho yao juu ya Msalaba, kushiriki katika maombi yao kibinafsi na ya jumuiya ili kila mmoja aimarishwe katika imani mbele ya majaribu ya maisha ya kila siku”. Kuhusiana na hali ya sasa nchini humo, wakifikiria sherehe za Pasaka, viongozi hao wameshauri kutafakari juu ya jinsi uwepo wa Kristo unaweza kurudisha na kuazaliwa matumaini na uaminifu katika familia, jamumuiya za parokia, na katika Kanisa Familia ya Mungu na kisiasa.

Kwa upande wa maaskofu, ishara za matumaini ya kutiwa moyo na kuungwa mkono viongozi wa vyama vya kiraia ambao kwa subira wanaendelea kuamini mazungumzo ya kijamii na kujumuisha; mipango ya kuungana tena kwa viongozi wa kisiasa kwa jina la faida kubwa ya taifa; uwezo wa wale wanaoshikilia nguvu kutomdhulumu mwenzake; wale ambao, wanahatarisha maisha yao, wanaendelea kupigana, hata kwa kutokuelewana, kwa usalama wa afya katika muktadha wa janga la Covid-19. “Safari yetu nyuma ya Kristo inatimizwa kwa kubeba misalaba yetu na safari yetu inaweza kuwa safari ya wokovu tu, ikiwa inastawishwa kwa kusoma Maandiko, jitihada za kitaalam na katika vyama vya kisiasa. Tunapinga majaribu ya unyanyasaji wa maneno, maadili au ya mwili”. Hatimaye Maaskofu mtashi yao ni kwamba maisha bora ya baadaye kwa nchi na dhamira thabiti inayolenga kuweka uhusiano wa kijamii itawahamasisha asasi za kiraia na viongozi wa kisiasa kuheshimiana na kufanya mazungumzo kwa jili ya wema na faida ya nchi yao.

02 April 2021, 15:09