Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Cabrejos Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Amerika ya Kusini (Celam). Askofu Mkuu Cabrejos Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Amerika ya Kusini (Celam). 

Celam:Maaskofu barani Amerika Kusini wataka waliotekwa nyara kuachwa huru

Tendo la kutekwa nyara Makuhani na watawa na walei watu wa Mungu ni la ukatili usio wa kibinadamu, lazima wakachiliwe hawa ndugu zetu kwa haraka. Wanaandika hivyo maasko wa Amerika ya Kusini kufuatia na tendo la utekwaji nyara wa watumishi wa Mungu hao uliotokea hivi karibuni huko Haiti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Amerika ya Kusini (CELAM) Askofu Mkuu Miguel Cabrejos, wa Jimbo Kuu Katoliki la  Trujllo (Perù), amemtumia barua yake Askofu Mkuu Launay Saturné, wa Jimbo Kuu la Cap-Haïtien na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Haiti , ambapo anaeleeza hisia zake za mshikamano kwa niaba ya Maaskofu wote wa Bara zima, kukutokana na habari za kuhuzunisha za kutekwa nyara na uhalifu zilizowatokea mapadre 5, watawa 2 na Walei 5 ambao wako mikononi mwa kundi la kihalifu huko Croix-des-Bouquets, eneo la Magharibi mwa mji wa Port-au-Prince.

Kwa maana anaeleza  kama Maaskofu wa Celam wanapaza sauti zao kwa nguvu zote kulaani tendo hilo la kikatili na lisilo la kibinadamu ambalo linaweka hatari ya afya na maisha ya makumi ya watu hao ambao wamejitoa maisha yao katika huduma ya Mungu na jirani. Celam inaomba zaidi ya hayo waachiliwe kwa jina la Mungu wa Upendo, wa Haki ana Huruma, wakombilewe haraka ndugu hao ambao wamejaribiwa bila hatia kwa sababu ya huru wao, na wakati huo huo wanaomba mamlaka husika kutumiza wajibu wao ili kuweza kuwakomboa ndugu hao.

Barua ya Rais wa Celam inahitimisha kwa kuamini kuwa inawezekana kwamba hakuna aliye na haki ya kumnyima mwingine huru wake binafsi, hasa ikiwa ni suala la kuteka nyara kwa lengo la kupata fidia  katika huru wa watu wasio na hatia. Haki ya kimataifa inathibitishwa kutolewa kwa hukumu kali katika tendo hili la ukiukwaji wa sheria.

15 April 2021, 14:18