Tafuta

2019.09.26 Euthanasia,kifo laini. 2019.09.26 Euthanasia,kifo laini. 

Canada:euthanasia na kifo laini ni mauji huru ya makusudi ya mwanadamu!

Maaskofu Canada wamethibitisha mara baada ya idhini ya hivi karibuni ya muswada wa uwezo wa kufanya zoezi la kifo laini,wanasema:"Euthanasia na kujiua kwa kusaidiwa ni mauaji ya makusudi ya maisha ya mwanadamu".Msimamo wao unabaki wa kukataa tendo hilo kwamba ni kukiuka Amri za Mungu.Hali hiyo inaharibu hadhi ya kushirikisha pamoja kwa kuzuia,kukubali na kusindikiza wanaoteseka na kufa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baraza la Maaskofu wa Canada (CCCB) wamelaani idhini ya hivi karibuni ya muswada wa C-7 ambao unapanua uwezekano ya kupokea msaada wa matibabu ili kufa ambayo hapo awali ilikuwa imetengwa tu kwa wale ambao walikuwa na sababu za kifo cha asili. Kwa maneno yao wanasema “Msimamo wetu unabaki wazi: euthanasia na kusaidia kujiua ni mauaji ya makusudi ya maisha ya mwanadamu kwa kukiuka Amri za Mungu; Hali hiyo inaharibu hadhi ya kushirikisha pamoja kwa kuzuia, kukubali na kusindikiza wale wanaoteseka na walio katika hali ya kufa. Kwa kuongezea, wanadhoofisha jukumu la msingi tunalotakiwa kuwatunza watu wadhaifu na walio hatarini zaidi katika jamii”.

Sheria hiyo kiukweli inapanua uwezekano kwa watu ambao hawawezi kuwa katika hatari ya kifo cha karibu, lakini ambao wamefikia hali ya kuteseka kimwili au kisaikolojia kwa sababu ya ugonjwa usiotibika au ulemavu. Katika barua iliyosainiwa na Askofu kuu Richard Gagnon, wa jimbo Kuu la Winnipeg na rais wa Baraza la maaskofu, Katoliki la Canada inasisitiza kuwa badala yake “maisha ya mwanadamu lazima yalindwe tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo chake cha asili, kwa awamu zote na kwa hali zote”, wakati kwa idhini ya sheria mpya, wagonjwa wa akili na walemavu wanaweza kupata shinikizo ambazo kwa bahati mbaya ni za kweli za hatari na zinazoweza kuharibu”. Maaskofu, pia wanatoa shukrani zao na kuonesha msaada wao kwa wafanyakazi wote wa kiafya na watu wa kujitolea wenye huruma ambao wanaendelea kutetea maisha kwa kupinga euthanasia na kusaidia kujiua, kuhamasisha utunzaji wa familia, marafiki na wapendwa katika mateso yao, au kusaidia wagonjwa na wanaokufa”. Kwa maana hiyo ombi la CCB kuhamasisha ufikiaji wa haraka wa huduma ya afya ya akili, msaada wa kijamii kwa wagonjwa wa akili na kwa mipango ya kuzuia kujiua, pia kulinda wagonjwa wa muda mrefu, wale wanaougua magonjwa yanayosumbua au wale ambao wanaishi pekee katika vituo vya kulazwa hospitalini.

Wakati huo huo, maaskofu wa Canada wananukuu Barua “Samaritanus bonus” yaani ya ‘Msamaria mwema’ kuhusu utunzaji wa watu katika hatua mbaya na za mwisho wa maisha, iliyochapishwa na Baraza la Kipapa  Mafundisho Tanzu ya Kanisa  mnamo Septemba 2020 na ambayo inathibitisha kuwa:  “Maumivu na kifo hayawezi kuwa vigezo vya mwisho ambavyo hupima hadhi ya binadamu, ambayo ni sawa kwa kila mtu, kiuukweli kwamba yeye ni mwanadamu”  na kwa kuongezea, maaskofu wa Ottawa wanatia moyo wanaume na wanawake wenye mapenzi mema  ili wasife moyo. “Tutawasindikiza katika sala na katika ulinzi wa dhati  dhidi ya utamaduni wa kifo ambao unaendelea kuharibu hadhi na heshima ya maisha ya mwanadamu katika nchi yetu”. Baraza la Maaskofu pia linataka uwezekano kuwa na dhamiri kwa wafanyakazi wa afya ambao wanaopinga euthanasia na kusaidia kujiua: “Haikubaliki ikiwa walilazimishwa kushiriki katika vitendo ambavyo dhamiri zao zinaona kuwa ni mbaya kiadili. Hasa kwa kuwa mauaji ya moja kwa moja ya mtu hayawezi kuzingatiwa kama jukumu”. Kwa sababu hii, maaskofu wanasema wanapinga kabisa kuruhusu kuangamizwa na kusaidiwa kujiua katika taasisi za Katoliki.

Pia kuna ushauri wa nguvu wa kuhamasisha tiba shufaa (Palliative care) ambayo ni kwa faida ya hali ya kimwili, kimhemko na kiroho kwa mgonjwa, hasa ikiwa inatolewa mapema. Kiukweli, wanaweza kupunguza na kudhibiti maumivu ya mwili, kisaikolojia na kiroho na mateso, na vile vile upweke na kutengwa, hisia za kupoteza hadhi na mzigo wa msaada ambao mara nyingi hupatikana na familia, marafiki na wanahowasaidia Wagonjwa. “Tiba shufaa na sio Euthanasia au kusaidiwa kujiua, ni jibu la huruma na la kuwa na mshikamano na mateso na kwa yule anayekufa”, maaskofu wa Canada wanasisitiza tena. Wito kwa waamini pia ni kujitoa na kuhusika katika ngazi ya mtu binafsi, parokia na jumuiya kuendelea kuweka shinikizo kwa wanasiasa waliochaguliwa juu ya masuala haya. Wanaomba kwa Mungu kwa bidii ili wapate neema mpya kwa namna ya kwamba hofu na kukata tamaa vilivyofanywa uzoefu kwa wengi uweze kuacha nafasi ya ujasiri na matumaini na ili kila mtu aweze kukubali wito wa kusaidia wanaoteseka na wanaokufa kwa mtazamo wa yoedo na huruma ya Kristo Mfufuka.

16 April 2021, 15:13