Tafuta

Vatican News
Mtu wa kujitolea akisafisha Kanisa la Dili , huko Timor Mashariki Mtu wa kujitolea akisafisha Kanisa la Dili , huko Timor Mashariki  (ANSA)

Askofu Mkuu wa Dili:Janga halisimamishi tumaini la Pasaka

katika ujumbe wa Pasaka Askofu Mkuu Virgilio do Carmo da Silva wa Dili, huko katika ujumbe wake wa Pasaka ameandika kuwa hata ikiwa Sherehe ya Ufufuko wa Bwana inakuja katika mazingira magumu ya janga,roho ya Pasaka haipaswi kuzimishwa na tumaini Kikristo katika Kristo Mfufuka halipaswi kuzuiwa.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Hata ikiwa Sherehe ya Ufufuko wa Bwana inakuja katika mazingira magumu ya janga, roho ya Pasaka haipaswi kuzimishwa na tumaini Kikristo katika Kristo Mfufuka halipaswi kuzuiwa. Ameandika hayo Askofu Mkuu Virgilio do Carmo da Silva wa Dili, huko  Timor  Mashariki, katika ujumbe wake wa Pasaka. Nchi, kwa sasa inaona kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19, ambayo imesababisha serikali kuzindua kizuizi kipya kutoka tarehe 3, Aprili hadi 2 Mei

Serikali imeazimia kutenga katika manispaa ya Dili, Baucau na Viqueque na sherehe za kidini zilizo na ushiriki wa waamini kusitishwa. Kwa njia hiyo ibada siku tatu ya maandalizi ya Pasaka zimefuatwa kwa waamini kupitia mitandao ya kujamii. Janga linawalazimisha kukaa nyumbani na kuzuia harakati zao, lakini Kristo daima anakuwa tumaini lao  na ujumbe wake unaweza na lazima uenezwe kila mahali, amesisitiza. Kwa maana hiyo mwaliko kwa waamini ni kwamba waelekeze macho yao kwa Mungu ili aweze kuponya majeraha yao yote, anasema Askofu Mkuu da Silva.

Mkuu huyo pia amehimiza wasisahau wale wanaoishi peke yao au ambao wako katika karantini na hawawezi kuungana tena na familia zao. Askofu Mkuu wa Dili  ameelezea mshikamano wake na wafanyakazi wa matibabu wanaofanya kazi bila kuchoka mchana na usiku na wale wote wanaofanya kazi wakiwa mstari wa mbele kusimamia dharura ya kiafya. Wakati huo huo, Jimbo kuu limechukua hatua za kutoa msaada kwa wagonjwa shukrani kwa mapadre, watawa na wa watu wa wajitolea wenye uwezo katika saikolojia na dawa ambao wanaweza kuwasiliana ikiwa kuna uhitaji. Msaada wa nyenzo kwa watu walio katika shida unatoka na kusambazwa na Caritas za huko.

Ikumbukwe kwamba, licha ya kutosajili vifo vyovyote kwa sasa, Timor ya Mashariki imeona maambukizi ya virusi vya corona vikiongezeka sana kwa mwezi mzima wa Machi. Kati ya wakaazi milioni 1.5, hadi sasa, kuna kesi 643 chanya, kati yao 41 pekee wamepona mnamo Machi 31.Ni  Matarajio kwa maana hiyo kuanza  kampeni ya chanjo ambayo inapaswa kuanza hivi karibuni, na kuwasili kwa kwa hatua ya kwanza ya chanjo ya AstraZeneca.

03 April 2021, 16:14