Tafuta

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Juba nchini Sudan Kusini ameaga dunia. Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Juba nchini Sudan Kusini ameaga dunia. 

Askofu Mkuu Mstaafu Lukudu Loro wa Jimbo la Juba,Sudan Kusini ameaga dunia

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu latoliki la Juba huko Sudan Kusini Paolino Lukudu Loro ameaga dunia tarehe 5 Aprili akiwa hospitali ya Nairoi Kenya.Askofu Mkuu akieleza wasifu wake marehemu amesema alikuwa nyota ya Kanisa na jamii ambayo imezimika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu mstaafu Paolino Lukudu Loro wa Jimbo la Juba, Sudan Kusini ameaga dunia akiwa huko Nairobi Kenya mwenye umri wa miaka 80. ifa hizo zimetolewa na Mfuasi wake wa Jimbo Kuu Askofu Mkuu Stephen Ameyu,  tarehe 5 Aprili akimmwelezea kuwa Askofu Mkuu mstaafu Lukudo Loro alikuwa kama nyota ambayo imezimika.

Mchungaji huyomzee alipata kiharusi wakati alikuwa Juba, baadaye  akasafirishwa kwenda Kenya ili kutibiwa na kufia huko. “Kama mchungaji wenu ameandika Askofu Mkuu Ameyu ninwauletea habari ya kusikitisha zaidi ya maisha yangu yote. Askofu mkuu Pauline Lukudu Loro, alikuwa nyota ambaye daima ilikuwa ingaaza macho yake katika Kanisa letu na taifa letu kwa zaidi ya miaka thelathini. Habari hii ya kusikitisha haituhusu Kanisa tu, bali pia jumuiya  pana ya jamii yetu  Sudan Kusini”.

Siku nne za maombolezo zimetangazwa na kiongozi wa sasa wa Jimbo kuu la Juba. Askofu Mkuu Mstaafu Paolino Lukudo Loro alipewa daraja la kikuhani mnamo Aprili 1970. Miaka minne baadaye, aliteuliwa kuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo la El Obeid, Sudan. Kwa maana hiyo aliteuliwa kuwa askofu wa makao hayo mnamo Mei 1979.

06 April 2021, 16:42