Tafuta

2021.04.09 Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mula owa Jimbo Kuu la Juba, Sudan Kusini. 2021.04.09 Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mula owa Jimbo Kuu la Juba, Sudan Kusini. 

Ask.Mkuu Ameyu:Papa Francisk akiwa tayari atakwenda Sudan Kusini

Wakati Sudan Kusini inapoanza kutoa chanjo kwa wafanyakazi wake,Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mula wa Jimbo kuu la Juba ametafakari juu ya Pasaka na Covid-19.

Sr. AngelaRwezaula -Vatican.

Msamaha ni Pasaka yenyewe na Pasaka ni msamaha, Askofu Mkuu Ameyu ndivyo amemwambia mwandishi wa uwakilishi wa Vatican News, Mbikoyezu John Gbemboyo, katika jiji la, Juba, walato Askofu Mkuu akizungumzia juu ya msamaha ambao Yesu alimpatia mwizi aliyetubu pale msalabani. “Tunaweza kupata tu mbingu kupitia msamaha wa wengine. Msamaha huu lazima uanzie na sisi. Lazima tusameheane kutoka ndani ya mioyo yetu. Msamaha ni kamili wakati tumesamehe wengine. Kupitia msalaba na ufufuko wa Kristo, sisi pia tunaweza kupata mbingu hapa katika maisha yetu”, amesisitiza Askofu Mkuu Ameyu.

Covid-19: Ukosefu wa chakula na lishe ya kiroho

Kuhusu Covid-19, Askofu Mkuu amesema hali ilikuwa kama kwamba watu nchini Sudan Kusini walikuwa wanakabiliwa sio tu na upungufu wa kiroho, lakini pia ilikuwa ngumu kwa watu wa kawaida kujikimu na kutoa chakula kwa familia zao kwa maana hiyo amesema “Covid-19 imeathiri maisha yetu, imekasitisha njia zetu za utamaduni na jadi ya maisha ya parokia. Imebidi tuweke kando shughuli nyingine muhimu pia kwa sababu ilibidi tuhudumie kwanza  waagonjwa Covid-19. Hatuwezi kuwatumikia waamini wetu kama tulivyofanya  hapo zamani”. Akiendelea amesema “Waamini hawana  chakula cha kiroho. Lakini sio tu lishe ya kiroho, kiukweli, watu wetu wengi wanakosa hata chakula. Walakini, ningependa makuhani wetu waendelee kuwahudumia watu kwa kadri wawezavyo, hata wakati mwingine hii inamaanisha kutoka mbali kupitia radio na njia zingine za elektroniki. Padre anaposherehekea Misa nyuma ya milango iliyofungwa ya parokia, yeye hubaki katika muungano na watu”, kiongozi huyo wa Juba amefaafanua.

Papa Francisko anabeba watu wa Sudan Kusini moyoni mwake

Alipoulizwa kuhusu Baba Mtakatifu Francisko ambaye anapenda katembelea Sudan Kusini, Askofu Mkuu Ameyu amelezea imani yake kwamba Baba Mtakatifu Francisko atafanya hija hiyo Sudan Kusini wakati ukifika:  “Baba Mtakatifu tayari alielezea nia yake ya kuja Sudan Kusini labda miaka miwili iliyopita. Kwa hakika alipokuja Kenya, Uganda, na Jamhuri ya Afrika ya Kati (2015), alitaka kutembelea hata Sudan Kusini na kisha kuendelea na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa bahati mbaya, wakati huo, hali nchini Sudan Kusini haikuwa nzuri kwa sababu ya vita. Papa amekuwa karibu sana na anafikiria watu wa Mungu huko Sudan Kusini. Baba Mtakatifu ana hamu ya kuwaona watu wake huko Sudan Kusini, na tuko tayari kumpokea. Sina shaka kwamba moyoni mwake, Papa Francisko amebeba watu wa Sudan Kusini, watu maskini wa Sudan Kusini, ambao wameteseka sana”, amehihitimisha.

13 April 2021, 13:58