Tafuta

2018.05.19 Quebec nchini Canada 2018.05.19 Quebec nchini Canada 

Maaskofu wa Quebec:Kusali na kutenda dhidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake

Maaskofu wa Quebec nchini Canada wanasema wanaamini kuwa inawezekana kubadilisha hali ya sasa ili unyanyasaji dhidi ya wanawake ukome,wanawake waaminike na kulindwa,pamoja na watoto wao,wanawake wapate rasilimali wanayohitaji,na wanaume wenye jeuri wasaidiwe na huduma zinazolengwa ili kuzuia uchokozi na kupunguza hatari ya kurudia tena.Ni kufutia mauaji ya wanawake 14 tangu mwanzo wa janga la Covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kati ya Mwezi wa Februari na Machi huko Quebec, sehemu kubwa ya Canada yenye watu wengi baada ya Ontario, na eneo ambalo linatumia lugha rasmi ya kifaransa, hivyo wanaozungumza kingereza ni wachache, wanawake saba wameuwa na waume zao au wenzi wao na kufanya kuwa jumla ya wanawake 14 waliouwawa tangu mwanzo wa Janga la Covid-19 kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa hivi karibuni na Tume inayohusu Kanisa na Jamii ya Baraza la Maaskofu wa Quebec. Hata hivyo wanasema “mwathirika mmoja ni mwathirika zaidi kama mtu wa imani, kwa maana hiyo tuunganishe sauti zetu na kwa mashirika yale ambayo yanajikita kuthibiti vurugu za nyumbani, ili kuomba serikali kitaifa, ifanye kazi ya kutekeleza mapendekezo 190 yaliyomo kwenye Ripoti ya 'Ujenzi wa Dhamana' na kufadhili vya kutosha utekelezaji wake. Ripoti hiyo iliwasilishwa rasmi mnamo 15 Desemba 2020, Ripoti hii iliandikiwa, kwa takriban miaka miwili ya kazi, na Kamati ya wataalam 21 juu ya msaada kwa wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia na wa nyumbani, iliyoteuliwa na mtendaji mnamo Machi 2019. Lengo lake ni kuelezea masuala ya kuzingatiwa ili kutekeleza hatua mpya na kutoa huduma bora zaidi katika mfumo wa haki kwa wahanga wa vitendo kama hivyo vya vurugu.

Inawezekana kubadilisha unyanyasaji dhidi ya wanawake

“Tunaamini kuwa inawezekana kubadilisha hali ya sasa ili unyanyasaji dhidi ya wanawake ukome, wanawake waaminike na kulindwa, pamoja na watoto wao. Jambo kuu pia ni wito wa maaskofu hao ambao wanasema kuwa: “wanawake wapate rasilimali wanayohitaji, na kwamba wanaume wenye jeuri wasaidiwe na huduma zinazolengwa ili kuzuia uchokozi na kupunguza hatari ya kurudia tena”. Mfano wa kufuata, uliooneshwa na maaskofu wa Quebec, ni ule wa Yesu, yule ambaye aliwapatia heshima wanawake waliotengwa wakati wake na kufundisha kwamba upendo kwa jirani ni muhimu zaidi kuliko mengine yote. Zaidi ya hayo, Ufufuko wake unaleta tumaini mbele ya vurugu na uovu uliopo ulimwenguni.

Kulaani dhuluma zote ndani na nje ya Kanisa

Ikumbukwe kwamba maandishi ya maaskofu yalifuatana na mipango maalum: kwa mfano, mnamo tarehe 31 Machi makanisa ya Quebec yalipiga kengele kuadhimisha wanawake wahanga wa unyanyasaji; mnamo tarehe 2 Aprili, Ijumaa Kuu, wakati wa Njia ya Msalaba, jumuiya zilisoma nia maalum za maombi, Chini ya Msalaba, kwa kuwaombea wanawake na wasichana wa jamii zao ambao wamepata aibu, kupigwa na vurugu hadi kifo chao. Walibeba msalaba kama Yesu. “Tunalaani dhuluma zote, pamoja na zile zilizofanywa ndani ya Kanisa. Tunaomba kwamba Kanisa letu na jamii yetu iwe kielelezo cha ulinzi, kinga na amani ”. Sala hiyo maalum pia ililenga janga la kusikitisha la wanawake wa asilia: “Wengi wao wamepotea au wameuawa. Waliwakumbuka wengine kuwa wanafanya uzoofu wa vurugu na ubaguzi, kwa mfano katika sekta ya huduma ya matibabu". Kwa sababu hii, waliombaa kuhamasisha kusikiliza, mazungumzo na kuondoa ubaguzi wa rangi. Mwishowe, wazo liliwaendea wote wahanga wa biashara haramu, vita na mateso ya kidini na kuomba kwamba dini ziwe chombo cha amani na umoja”.

13 April 2021, 13:56