Tafuta

Vatican News
Kusoma Kuruni wakati wa Mfungo wa Ramadhani Kusoma Kuruni wakati wa Mfungo wa Ramadhani   (ANSA)

Afrika Ramadhani:Matashi mema kutoka Nigeria na Mauritius

Katika fursa ya kuanza mwezi wa Radhamani,ujumbe kwa waislamu umetoka kwa Askofu Jimbo Katoliki la Oyo nchini Nigeria na Baraza la Kidini kisiwani Mauritius wakishauri mazungumzo ya kidini na kushirikishana mahitaji katika wakati huu muhimu wa siku za kiroho.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Umetolewa wito kwa ajili ya mazungumzo ya kidini na kulaani vurugu na muda mrefu ambao wakristo na waislamu wanaendelea kulipa gharama kubwa barani Afrika. Aliyezindua wito huo ni kutoka jimbo Katoliki la Oyo nchini Nigeria katika ujumbe wa fursa ya  kutoa matashi mema kwa wafuasi wa Kiislam ambao wameanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, siku ya Jumanne tarehe 13 Aprili 2021. Kwa namna ya pekee, ujumbe unasisitiza kuwa mwaka huu katika mwezi mtukufu wa kiislamu umeangukia katika kipindi cha Pasaka kwa Wakristo ambao bado wanaendelea na maadhimisho hayo, ni usambamba unaoibua shauku kubwa. Na wakati huo huo, kuna masikitiko makubwa ya kuongezeka kwa mauaji katika nchi mbali mbali za Afrika Magharibu kutokana na mashambulizi ya kigaidi ambayo yanawalenga wakristo na waislamu kwa namna hiyo hiyo. Askofu Emanuel Badejo wa Oyo anaeleza wasiwasi mkubwa juu ya  vurugu za sasa kuongezeka, utekaji nyara, ujambazi na umwagaji wa damu katika nchi yao. Hayo ni matukio yanayo wakumba wakristo  sawa  na wasilamu na  kuwafanya maisha yao ya kila siku kuwa magumu sana na ukosefu wa usalama kwa wote, amebainisha.

Heshima za utamaduni wa Afrika zilindwe

Kufuatia na hilo ndipo anatoa wito ili utamaduni wa kiafrika uweze kulindwa ambao unaheshimu utakatifu wa maisha na haki kwa raia wote na kulinda maelewano ya kudumu. Hayo ni malengo ambayo wakristo na waislamu wenyewe wanapaswa kuungana kwa pamoja ili kuhamasisha fadhila za usawa, za amani na haki, kwa namna ya kuweza kuleta pamoja jamii ya Afrika Magharibu katika njia ya utulivu na matarajio. Kama wakatoliki, wanabainisha jinsi ambavyo wamejifungua kufanya kazi na waislamu kwa ajili ya maendeleo ya binadamu yenye kuleta matunda mema ambayo yanaborehsa wakati ujao wa kizazi na kijamii kwa ujumla, amehitimisha Askofu wa Oyo ujumbe wake.

Ujumbe kwa Waislamu kutoka Baraza la kidini la Mauritius

Kwa upande wa Kisiwa cha Mauritius, Baraza la Kidini katika ukumje wake kwa waislamu, wanasisitiza juu ya matokeo ya janga la Covid-19 wakati wa ibada za kiislamu. Kwa miaka miwili mfululizo misikiti imebaki imefungwa. Tunawatakia matashi mema waamini wa kiislamu ambao wametambua kuvumilia kuishi mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakiwa nyumbani, na mwamko huo huo kama kipindi cha kawaida.

Kukaribiana na ndugu wenye kuhitaji katika kipindi cha mfungo

Baraza hili la kidini  aidha linaamini kutokana na muktadha wa kipindi cha mfungo ambacho kinawakilisha kwa jumuiya ya kiislam, mwamko wa mshikamano, ili kuchangia kwa wahitaji  wengine hasa wale ambao wana hali ngumu kijamii. Tasaufi ambayo inakaribia na Mungu muumbaji, kwa mujibu wa ujumbe huo ni kwamba itapelekea kukaribiana na ndugu wote wenye kuhitaji ili nao waweze kupata chakula cha kutosha na wasiwe na njaa au matatizo mengine ya maisha ambayo yahabaribu hadhi ya kuwa mwanadamu. Mungu wa huruma awapatie waislamu wote neema yake katika kipindi hiki cha mfungo ili sala zao ziweze kusikika, wanaitimisha.

15 April 2021, 13:52