Tafuta

Vatican News
2020.11.11 Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki Zambia,Askofu George Lungu 2020.11.11 Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki Zambia,Askofu George Lungu 

Zambia:Maaskofu watoa wito dhidi ya ufisadi katika Siku ya Kitaifa ya Vijana

Katika muktadha wa mada ya Siku ya vijana,Rais wa Baraza la Maskofu Zambia(Zccb)amewahimiza vijana kujishughulisha kuliko kuunda na kuhakikisha wakati ujao,na sio wao tu,bali pia kwa vizazi vijavyo:“Ninyi ni mawakala wa thamani wa mabadiliko ya leo hii,kwa kujiandaa na kesho iliyo bora katika kutafuta mazingira ambayo yanakuza utambuzi wa ndoto za kila mtu”.Amehimiza mshikamano ili kupambana na ufisadi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Vijana waungane pamoja katika mapambano dhidi janga la ufisadi ambao umeenea katika Nchi. Ndiyo wito uliozinduliwa na Baraza la Maaskofu kitaifa nchini Zambia (Zccb),wakati wa fursa ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana tarehe 12 Machi 2021. Katika taarifa ya Askofu George Zumaire Lungu, wa jimbo katoliki la Chipata na Rais wa Baraza la Maaskofu (Zccb), amechapisha ujumbe huo akisema kuwa mfumo wa kijamii ambao umedidimia katika ufisadi unawakilisha kizingiti cha mchakato wa kutimiliza wakati ujao  na endelevu kwa vijana kwa sababu unawaibia ndoto zao na kuzima uwezekano wa fursa za kuibua uwezo ambao Mungu amewapatia wao kwa ajili ya wema wa pamoja.

Kwa maana hiyo, vijana wameshauriwa kuungana katika mapambano dhidi ya ufisadi kila mahali walipo na ulipoegemea, kwa sababu “ ni lazima kutoa mchango kwa wote. Haiwezekani kupambana pekee, badala yake ni kupambana kwa pamoja”. Katika ujumbe huo Askofu Lungu anaandika kwamba: “ufisadi haukubaliki, kwani unasonga ujana na zaidi katika umaskini, na kuwapa matumaini kidogo ya kuishi na kuwasonga katika chaguzi za maisha ya mahangaiko ambayo labda kamwe wasingeweza kufanya hivyo”.

Katika muktadha wa mada ya Siku ya vijana iliyochaguliwa mwaka huu, isemayo “Vijana, kujenga wakati ujao wenye msimamo na endelevu”, Rais wa Baraza la Maskofu Zambia (Zccb) amewahimiza vijana kujishughulisha kuliko kuunda na kuhakikisha wakati ujao, na  sio wao tu, bali pia kwa vizazi vijavyo: “Ninyi ni mawakala wa thamani wa mabadiliko ya leo hii, kwa kujiandaa na kesho iliyo bora katika kutafuta mazingira ambayo yanakuza utambuzi wa ndoto za kila mtu”. Kwa maana hiyo amewahakikishia msaada wa kila wakati kwa upande wa  Kanisa: “Furaha na matumaini, uchungu na mahangaiko ya watu wa wakati huu, hasa ya wale ambao ni maskini au kwa njia fulani wameathirika, ni furaha na matumaini, maumivu na wasiwasi wa wanafunzi wa Kristo, kama inavyothibitisha Hati ya kichungaji ya “Gaudium et spes”, ambayo ni matunda ya Mtaguso wa la Pili la Vatican”, amesisitiza Askofu Lungu.

Wakati huo huo, askofu huyo amebainisha kwamba “ Kanisa linahitaji msukumo, hisia, imani ya vijana,  pia uvumilivu wao ili wajue jinsi ya kungojea mahali ambapo bado halijafika”. Hatimaye matumaini ya Askofu Lungu ni kwamba vijana wataweza kuendelea na safari yao ya kusonga mbele, wakivutiwa na uso wa Kristo na wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Siku ya Kitaifa ya Vijana ilianzishwa na serikali ya Zambia mnamo 1966, na ambayo hufanyika kila mwaka, na ni katika  kukumbuka ghasia zilizotokea mnamo tarehe 12  Machi  1962, wakati vijana wa nchi hiyo waliuawa na vikosi vya usalama vya wakoloni. Tukio hilo linakusudia kuongeza hisia za kujitoa kwa vijana ndani ya jamii, na vile vile mchango wao katika maendeleo ya nchi, kama viongozi wa baadaye.

15 March 2021, 17:14