Tafuta

Kanisa Katoliki nchini Zambia limechukua hatua mpya ya kukubali suluhisho la kidijitali ili misa ziweze kutangazwa na televisheni ya kitaifa katika muktadha wa janga la sasa Kanisa Katoliki nchini Zambia limechukua hatua mpya ya kukubali suluhisho la kidijitali ili misa ziweze kutangazwa na televisheni ya kitaifa katika muktadha wa janga la sasa 

Zambia:Kanisa na harakati za kidijitali katika nyakati za janga

Kanisa nchini Zambia linaelekea kwenye nyaja ya kidijitali zaidi baada ya kutia saini ya makubaliano ya ushirikiano na kampuni muhimu ya mawasiliano ya ndani(Zamtel)ili kutangaza misa zote zinazorekodiwa nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Vyombo vya habari katoliki nchini Zambia vinaharakisha kuingia katika mabadiliko ya kidijitali. Mgogoro wa Covid-19 umetoa chachu na  nguvu zaidi ya mchakato huu, kuongeza ufahamu wa umuhimu wa njia mpya katika utume wa Kanisa. Kutokana na ufahamu huo yamenzishwa makubaliano  mpya ya ushirikiano yaliyosainiwa katika siku za hivi karibuni kati ya Televisheni ya  Lumen ya Zambia, ambayo ni runinga ya Baraza la  Maaskofu Katoliki nchini  Zambia (CBCZ), Televisheni ya Loyola ya Jumuiya ya Kijesuit na Kampuni muhimu ya mawasiliano ya ndani (Zamtel). Kwa mujibu wa maelezo ya blog ya Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA) inabainisha kuwa Zamtel itadhamini utangazaji wa Misa zinazorekodiwa na idhaa mbili Katoliki za Runinga katika nchi yote.

Mawasiliano ni asili katika Kanisa katoliki

Kwa mujibu wa maelezo ya Padre Patrick Mulemi, SJ, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Televisheni ya Loyola, wakati wa hafla ya kutia saini ya makubaliano  amesema ushirikiano huo ni sehemu ya maono ya vyombo vya habari Katoliki 2021 kuungana na kufikia zaidi ya waamini milioni 6 na umma kwa ujumla kupitia njia ya runinga. Akiongea wakati wa hafla hiyo  siku ya Jumatano, tarehe 24 Machi 2021, Padre  Mulemi, SJ., amekumbusha kuwa mawasiliano kwa  asili yake, katika Kanisa yamekuwa ni umuhimu sana. Aidha kuhani wa Kijesuit ameangazia hitaji la kutumia fursa kubwa zinazotolewa na teknolojia ya kidijitali ili kufikia idadi kubwa ya watu ambao hawawezi kushiriki kimwili katika matukio kama inavyotokea hasa katika miezi hii ya janga kubwa la ulimwengu.

Hatua ya Kanisa la Zambia linawakilisha utume wake

Kwa kuongezea Padre Patrick amebainisha ushirikiano mpya utasaidia Kanisa kutangaza Injili. Na pia enzi za kidijitali zinaonesha fursa nyingi katika utamaduni wa kisasa na Kanisa linapaswa kuchukua fursa kama hiyo kuwafikia watu kimawasiliano zaidi. Aidha, utaleta ajira mpya katika nchi ambayo bado kuna ukosefu mwingi wa ajira. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Zamtel, Sydney Mupeta, pia amebainisha  jinsi janga la Covid-19 limeleta mabadiliko ya kidijitali kuwa ya haraka zaidi, na kuongeza kusema kwamba hatua mpya iliyochukuliwa na Kanisa Katoliki nchini Zambia kukubali suluhisho la kidijitali ni hatua kubwa na inakua na sauti thabiti kwa shugghuli na kuwakilisha mabadiliko ya utume wake.

29 March 2021, 15:26