Tafuta

Vatican News
Watu wa kujitolea wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika maandalizi ya chakula kwa ajili ya wasio na makazi na wanaoishi katika hali ngumu Watu wa kujitolea wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika maandalizi ya chakula kwa ajili ya wasio na makazi na wanaoishi katika hali ngumu  (ANSA)

Uhispania:Jumuiya ya Mtakatifu Egidio bega kwa bega kwa wahitaji!

Katika kipindi cha janga la virusi vya Corona,Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa mwaka huu wa mwisho wametoa chakula cha jioni kwa watu laki tatu wasio na makazi na wenye kuhitaji zaidi,huko Madrid nchini Uhispania.Katika taarifa yao wanasema leo hii kuliko awali,kwa sababu ya udhaifu na kutokuwa na uhakika,ni muhimu kusaidia wale ambao wanateseka zaidi kwa sababu ya mgogoro wa kiafya,kiuchumi na kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Katika kilio kilichozoinduliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio huko Madrid kupitia katika ukurasa wa Tovuti yao, baada ya mwaka mzima wakiona kuongezeka zaidi na kwa namna ya kuleta wasi wasi wa umaskini, wameandika wakieleza hali halisi kuwa: “Janga la sasa linazidi kuongeza umaskini, lakini pia hata kuongezeka kwa mshikamano. Tunahitaji msaada kutoka kwako”. Hata hivyo wamebainisha kuwa wasi wasi wa umaskini si tu kwa wale ambao tayari walikuwa wanateseka na matokeo hayo, kama vile wasio kuwa na nyumba, lakini hata ndani ya familia zenye kipato cha chini, wazee na wafanyakazi wa siku.

Tangu tarehe 15 Machi 2020 hadi leo hii, Jumuiya hii katoliki imelazimika kuongeza maradufu nguvu zake ili kuweza kujibu mahitaji ya watu walio wadhaifu na katika mazingira magumu kutokana na pigo la mgogoro wa kiafya na kiuchumi. Watu 300,000 wameweza kupatiwa mlo wa jioni kwa wasio na makazi, na familia 1,500 wamesaidiwa ikiwa ni pamoja na kuheshimu hatua za kiafya za kuzuia Covid-19. Kwa mujibu wa taarifa ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inathibitisha hali halisi ya sasa ni ambayo isiyo elezeka.

Licha ya hayo mbele ya kuongezeka kwa mahitaji, hawakukosa hata hivyo kueleza kuwa pamoja na hayo yote lakini hata nguvu ya mshikamano imeongezeka mara dufu chini ya kivuli cha watu wengi ambao wamekaribia Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ili kuweza kuwasaidia wenye kuhitaji. Suala hili limeruhusu wao kusaidia kwa kiasi kikubwa idadi kubwa ya watu na mara nyingi. “Leo hii kuliko hapo awali, kulingana na hali halisi kubwa ya udhaifu na kutokuwa na uhakika, ni muhimu kuendelea kusaidia wale ambao wanateseka zaidi kwa sababu ya mgogoro wa kiafya, kiuchumi na kijamii, na kwa jitihada zaidi ya kutomwacha yoyote awe peke yake anayeteseka zaidi katika kipindi hiki na kuwa “Wote ni ndugu” na kujenga Kanisa kuanzia na walio wa mwisho”, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaeleza.

19 March 2021, 12:48