Tafuta

Vatican News
2021.03.07 :WANAWAKE LAZIMA KULINDWA DHIDI YA WOGA WA MNYANYASAJI,DHIDI YA VURUGU NA DHIDI YA DAI KALI LA KUMILIKI 2021.03.07 :WANAWAKE LAZIMA KULINDWA DHIDI YA WOGA WA MNYANYASAJI,DHIDI YA VURUGU NA DHIDI YA DAI KALI LA KUMILIKI 

Siku ya wanawake kimataifa:paza sauti ya kilio cha kupinga vurugu

Askofu Mkuu wa Mario Delpini wa jimbo kuu katoliki amechapisha ujumbe katika fursa ya Siku ya wanawake duniani ifanyikayo kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka akiomba waomba:kila mwanamume anayempiga mwanamke na anamdharau dada,ndugu. Kila nyumba iliyoharibiwa kuwa gereza,kila uzuri uliogeuzwa kuwa tamasha,kila ndoto iliyo badilishwa kuwa jinamizi, na kila mwanamke anaye tumiwa kama kitu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Dhidi ya woga wa mnyanyasaji, dhidi ya vurugu zinazotokea, dhidi ya dai kali la kumiliki, dhidi ya utafutaji wa kudhalilisha, nitapaza kilio cha kupinga. Nitakuwa sauti ya kila mwanamke aliyejeruhiwa, wa kila kijana aliyekataliwa, wa kila uzuri uliotumiwa, wa kila uaminifu uliosalitiwa. Nipaza kilio cha kupinga na kuomba haki kwa kila mtoto aliyebakwa, kwa kila msichana aliyedanganywa, kwa kila ukomavu wa kufedheheshwa, kwa kila kifo cha nguvu. Ni maneno ya Ujumbe wa Askofu Mkuu wa Mario Delpini wa jimbo kuu katoliki la Milano, Italia yaliyochapishwa tarehe 7 Machi 2021 katika kueleka kilele cha  Siku ya Wanawake Kimataifa ifanyikayo kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Askofu Mkuu wa milano anaombea kila mwanamume anayempiga mwanamke na anamdharau dada, ndugu. Kila nyumba iliyoharibiwa kuwa gereza, kila uzuri uliogeuzwa kuwa tamasha, kila ndoto iliyo badilishwa kuwa jinamizi, na kila mwanamke anaye tumiwa kama kitu.

Kinyume na vurugu, hata hivyo, amehitimisha Askofu Mkuu Delpini, kuwa kuna ushirikiano kati ya wanaume na wanawake, kwani yule asiye kuwa na ushirikiano na mwingine anajikunjia katika upweke na kujikunja kufikiria ubaya na mawazo yasiyo kamilika katika maisha na katika upendo. Wakati huo huo, Caritas ya Kiambrosi ya jimbo Kuu katoliki la Milano, Italia pia limezindua tovuti mahali ambapo inawezekana kuomba msaada dhidi ya unyanyasaji wa wanawake, jambo ambalo ni la kushangaza, linalozidi sana na katika janga limelazimisha wahanga wengi kubaki wamefungwa nyumbani, pamoja na wauaji wao.

Kulingana na Takwimu za Italia, msimu uliopita 2020 simu za kupambana na vurugu hzo ziliona ongezeko la asilimia 73% wakiomba msaada, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2019.  Ili kupanua, kwa njia hiyo mtandao wa kuomba misaada, tovuti mpya yenye jina: Non è amore, yaani sio upendo: ( https://noneamore.caritasambrosiana.it/ imezinduliwa. Hii imeundwa kuwa chombo sio tu cha habari na ufahamu, lakini pia njia ya kuomba msaada kwa njia salama, tovuti hii inatoa maelekezo ya kujua dalili za kutambua kwanza ishara za kuonesha unyanyasaji wa nyumbani, na vile vile uwezekano, kupitia fomu maalum, ili kuingia kwenye uhusiano na waendesha huduma ya kupambana na vurugu kwa njia inayolindwa, kwa kuvinjari kifaragha na ili usije kushukiwa na mwezi na hivyo kusumbuliwa naye. 

07 March 2021, 16:43