Tafuta

Vatican News
2020.09.18 QUERIDA AMAZONIA NI WOSIA WA PAPA FRANCISKO BAADA YA SINODI YA KANDA YA AMAZONIA 2020.09.18 QUERIDA AMAZONIA NI WOSIA WA PAPA FRANCISKO BAADA YA SINODI YA KANDA YA AMAZONIA 

Repam:Wanawake wawili wachaguliwa katika ngazi kuu ya uongozi kikanisa!

Katika taarifa iliyotolewa kuhusu hatua ya uchanguzi wa viongozi wapya washauri wakiwemo wanawake wawili katika Mtandao wa Kikanisa wa Amazonia(Repam),inathibisha:“Hii ni hatua mojawapo ya safari ya umoja ambayo,kama Hati ya Sinodi ya Kanda ya Amazon inathibitisha:tabia ya kuheshimu hadhi na usawa wa wale wote waliobatizwa,na ushirikiano katika karama na huduma ili kutambua pamoja sauti ya Roho.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mtandao wa Kanisa la Amazonia (Repam) umepanua ngazi ya urais wake kwa kuweka watu wengine watatu, wakiwemo wanawake wawili ambao ni Sr. Maria Carmelita de Lima Conceição, na Yesica Patiachi Tayori, mtu asilia kutoka Harakbut, ambao watakuwa na jukumu la  washauri katika chombo hiki cha mtandao wa kikanisa wa Baraza la Maaskofu katoliki wa Amerika ya Kusini; na mtu wa tatu Rodrigo Fadul Andrade atakuwa Naibu Katibu. Wote watatu wameongezwa katika bodi ya wakurugenzi wa chombo hicho. Rais ni Kardinali Pedro Barreto; makamu wa rais, Monsinyo Rafael Cob, na katibu mtendaji, João Gutemberg Sampaio ambaye ni mtawa  wa Marist.

Katika taarifa kuhusu uchanguzi wa viongozi hao inasema: “Hii ni hatua mojawapo ya safari ya umoja ambayo, kama Hati ya Mwisho ya Sinodi kwa Kanda ya Amazonia inathibitisha,  hasa kwa tabia ya kuheshimu hadhi na usawa wa wale wote waliobatizwa, na ushirikiano katika karama na huduma, kutokana  na  furaha ya kukusanyika pamoja ili kutambua pamoja sauti ya Roho”. Kwa mujibu wa taarifa hiyo inasema : “Kusikiliza sauti ya wanawake ilikuwa moja ya mada za Sinodi ya mwisho ambayo ilithibitisha umuhimu wa kushauriwa na kushiriki katika michakato ya kufanya maamuzi, pia kupata huduma za Kanisa ambazo hazihitaji mpaka kuwekwa wakfu, lakini zinazo waruhusu walei kujieleza vema” .

Kwa kuongezea Sr. Maria Carmelita na Yesica ni walizaliwa wa Amazonia, ambao wanapaswa kusaidia kuunda Kanisa lenye uso wa Amazonia, kama ilivyotakiwa na Sinodi yenyewe, na vile vile na Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia  wake wa Kitume wa Querida Amazonia. Kwa upande wake, Sr. Maria Carmelita, Mkuu wa Shirika la watawa Wasalesian wa Amazon nchini  Brazil, amekaribisha huduma yake mpya na hisia ya shukrani kwa mwendelezo huu uliotolewa katika pendekezo la Papa, ambalo ni kwamba, Kanisa linaendelea kuwa sinodi na kwamba kila mtu inaweza kukusikilizwa. Sista amesema: “Ninahisi furaha kuu ya kuweza kutoa sauti kwa wale ambao kila wakati hawana nafasi ya kuzungumza” na kusisitiza akihitimisha kuwa “Hii ni moja wapo ya changamoto nyingi zinazojitokeza leo hii, pamoja na furaha ya utume mpya”.

06 March 2021, 15:11