Tafuta

Vatican News
Wanafunzi wasichana waliokuwa wametekwa nyara nchini Nigeria Wanafunzi wasichana waliokuwa wametekwa nyara nchini Nigeria  

Nigeria:wanafunzi wakombolewa inabaki mapambano dhidi ya ugaidi na Covid-19!

Furaha ni kubwa kukumbolewa kwa wasichana wa shule waliokuwa wametekwa nyara Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wakati huo huo wamerekodi mashambulizi ya kijihad katika ngome za Umoja wa Mataifa.Padre Patrick Alumuku, wa Abuja anatoa ushuhuda wa matumaini hata katika harakati za kufika chanjo dhidi ya Covid-19 katika muktadha wa mpango wa Covax.

Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Nigeria inarudisha mvuto wa hewa ya utulivu baada ya kukombolewa wanafunzi 279 waliotekwa nyara katika shule moja ya serikali ya Zamfara Kaskazini. Hata hivyo baada ya kukataa kukumbolewa kwao siku zilizopita, hatima ya watoto hao imeweza kutolewa rasmi ya habari nzuri, kuwa wasishcna hao wako mahali fulani pa usalama wa serikali wote wakiwa na afya njema. Aliyetaarifu hivyo ni mkuu wa serikali ya Zamfara, Bello Matawalle, kwa kuthibitisha kuwa kukombolewa kwao hakukuwa na fidia. “Ni wakati mzuri wa furaha kwa Nchi” amesema. Kuhusiana na suala hilo naye Padre Patrick Alumuku, Mkurugenzi wa mawasiliano ya Jimbo Kuu Abuja, ambaye ametoa taarifa hata juu ya ujumbe uliotolewa na Rais wa Nigeria kwa Taifa zima akiwahakikishia juu ya jitihada za serikali kwa ajili ya kuzuia utekaji mpya wa nyara kwa wanafunzi.

Padre Alumuku amethibitisha kuwa hali ya sasa katika nchi ni ngumu sana na amezungumza juu ya muungano wa nguvu kati ya majihad wa Boko Haram na makundi mengine ambayo yamefika kutoka Kaskazini hasa makundi yanayotoka Libia, Mali, Chad na Niger, ambao wameshuka nchini Nigeria wakifikiri kuwa na Rais wa nchi Mwislam anaweza kufanya chochote kile amabacho wanapenda katika nchi. Zaidi mashambulizi kwenye ngome za Umoja wa Mataifa, Padre Patrick ameeleza kuwa magaidi wanataka kuhusisha, si tu nchi ya Nigeria, lakini hata Jumuiya ya Umoja wa mataifa kwa kutaka kuonesha kuwa wanao uwezo wa kushambulia kila mahali.

Hata hivyo mbele ya hali halisi hii ya kutisha katika nchi hiyo, mwanga kidogo umeonekana hata kwa kufika nchini humo, dozi milioni 3,9 za chanjo dhidi ya Covid-19, kupitia mpango wa Covax. Baada ya Ghana  na Ivory Coast na nchini Nigeria  sasa wanaandaa kampeni ya chanjo iliyotolewa katika mfumo unaotazamiwa wa nchi zenye kipato cha chini. Kwa mujibu wa Padre Patriki ni matarajio kuwa yote yanaweza kwenda vizuri. Na wanamshukuru Mungu kuwa katika maeneo yao, janga halikuleta matokeo mabaya kama ilivyo katika Nchi nyingine. Na kwamba walikuwa na hofu kubwa kutokana na kutokuwa na hospitali za kutosha na uwezo wa kukabiliana na dharura hii ya virusi kama ingewakumba kwa namna ya ilivyo wakumba bara la Ulaya na Amerika zote, na Marekani, ni wazi kwamba ingekuwa ngumu sana. Hatimaye, Padre Patriki anaomba ili chanjo iweze kuwafikia wanageria wote.

Nigeria kwa hakika inajikuta inayumbishwa na ugaidi. Tukio la mwisho ni la Jumatatu jioni ambapo majihad wa Iswap, Kundi ambalo lina makoa yake Kaskazini mashariki mwa nchi, walifanya mashambuzli mawili katika mji wa Dikwa, kwa kuligusa ngome la Umoja wa mataifa ambalo lilikuwa na wahudumu wa kibinadamu ambao walikimbilia kwenye maandaki lakini washambulia kambi ya kijeshi kwa mujibu wa taarifa ya habari ya AFP na afisa mkuu wa majeshi na chanzo kisichojulikana. Habari ya mwisho inasema ngome ya msaada wa kibinadamu imechomwa moto na wanamgambo hao lakini hakuna mfanyakazi yoyote aliyeathirika na ili kuwazuia majihad hao, walituma nguvu za kijeshi huko Dikwa katika mji wa Marte kilomita 40 kutoka mji huo.

03 March 2021, 09:44