Tafuta

Vatican News
2020.04.25 Mkutano wa Chama cha Vijana kuhudu mkakati wa kuzuia  Covid-19, Maputo, Msubiji.  2020.04.25 Mkutano wa Chama cha Vijana kuhudu mkakati wa kuzuia Covid-19, Maputo, Msubiji.  

Msumbiji:mgogoro wa Capo Delgado siyo wa kikanda tu ni wa kiduni

Wasiwasi mkubwa wa Shirikisho la Mabaraza ya Makanisa wa Afrika kusini maashariki kuhusiana na vurugu nyingi zinazowakumba raia wa mkoa wa Capo Delgado nchini Msumbiji ambao tangu 2017 wanasumbuliwa na makundi yenye silaha na umwagaji damu.Zaidi ya watu elfu mbili wamekufa na karibia watu 530,000 wamerundikana ndani kutokana na mgogoro huo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Suala la Cabo Delgado siyo tatizo la Msumbuji tu, ni dharura ya kikanda na kwa maana hivyo ni kushindwa kwa Afrika yote ambayo haiwezi kudharau hata kwa ngazi ya kidunia. Ni maoni  ambayo yametolewa na  Shirikisho la Mabaraza ya Makanisa ya Afrika Kusini (Foccisa), chombo hicho kinaomba uwepo wa matendo ya dhati na ya haraka ili kusaidia watu ambao wametishiwa vibaya sana na kushambuliwa na virugu katika mkoa huo ambpo tangu mnamo 2017 umekuwa uwanja wa umwagaji damu kutokana na makundi yenye silaha  ya kijihad ambayo yanaungana na yale yanayojiita Serikali ya Kiislamu. Zaidi ya watu elfu mbili wamekufa na karibia watu 530,000 wamerundikana ndani kutokana na mgogoro huo.

Janga hili mara nyingi limeelezwa katika ngazi ya Kimataifa na aliyekuwa Askofu wa Pemba, Luiz Fernando Lisboa, leo hii Askofu wa Cachoeiro de Itapemirim, nchini Brazil na ambapo Papa Francisko amekwisha toa mara nyingi miito   kadhaa kwa  ajili ya Mkoa wa Cabo Delgado. Na inakumbukwe wito uliotolewa mnamo tahere 25 Desemba  2020 wakati wa Ujumbe wa Urbi et Orbi wa Siku ya Kuzaliwa kwa Bwana. Mgogoro katika mkoa wa Msumbiji pia alikumbusha Papa Francsiko  katika hotuba ya kiutamaduni mwanzoni mwa mwaka huu alipokutana na wanadiplomasia tarehe 8 Februari 2021.

Shirikisho hili Foccisa ni mwanachama wa Mabaraza ya  Makanisa Ulimwenguni (WCC) ambayo ni  pamoja na Mabaraza ya Kitaifa ya Makanisa ya nchi 12 za kusini na mashariki mwa Afrika ambalo lilianzishwa mnamo 1980. Nchi wanachama ni:  Tanzania, Angola, Namibia, Zambia, Swaziland, Malawi, Kenya, Zimbabwe, Botswana, Lesotho, Msumbiji na Afrika Kusini, ambapo hata Baraza la  wa Maaskofu wa Afrika Kusini pia ni mwanachama. Katika taarifa yao iliyochapishwaAlhamisi tarehe  4 Machi 2021 mara baada ya mkutano wake, wa Makatibu wakuu wa Baraza la Kitaifa la Makanisa wanachama wa Shirikisho, wanahuzunisha na mashambulizi ya kinyama yalitofanywa na waamgambo hao dhidi ya raia wasio na hatia.

Kati ya matendo hayo ya kikatili ni pamoja na kukatwa vichwa vya watu, na kutoa  na kusafirisha sehemu za miili ya binadamu, uporaji, moto, mauaji ya jumla na ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu ambao unasababisha idadi kubwa ya watu wa eneo hilo, asilimia 10% ambao kwa  sasa wamehamia ndani. Katika muktadha huu wa kushangaza, makanisa ya kusini na mashariki mwa Afrika kwa njia hiyo yanatoa ombi la dharura kwa mamlaka ya Msumbiji na mashirika ya kimataifa ili kukomesha vurugu na kurejesha usalama katika mkoa huo  ulioko kaskazini mwa Msumbiji. Kwanza kabisa wanageukia Serikali ya Maputo ili iwe na ujasiri wa kuchukua hatua zinazofaa katika uzito wa hali badala ya kupuuza mgogoro kwa kuupunguza kuwa suala la uhalifu na baadaye  kuchunguza kijamii na kiuchumi sababu ambazo zinafanya Cabo Delgado kuwa ardhi yenye rutuba na iliyoiva kwa aina hii ya uasi .

Mkoa huo , kwa hakika ni maskini katika miundombinu, huduma za msingi, na kiwango cha juu zaidi cha watu wasiojua kusoma na kuandika nchini, lakini ni matajiri kwa malighafi, na amana kubwa ya gesi asilia, migodi ya grafiti, rubi na rasilimali nyingine  nyingi ambazo zina unyonyaji ambao umeanza hivi karibuni lakini hata hivyo kuwa na  faida kidogo sana  kwa wakazi wa eneo hilo. Kupitia uchambuzi wa hali hii  viongozi wa Kikristo wa Kiafrika wanasema, Serikali na watu wa Msumbiji wanaweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ujenzi wa jamii yao na kufanya kazi na jamii zilizoathiriwa ili kuboresha maisha yao. Kwa sababu hii wanahimiza pia msaada wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika (AU) na hasa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(Sadc): “Tunaziomba nchi na serikali za Kamati ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), kujibu haraka uasi nchini Msumbiji, mmoja mmoja na kwa pamoja kwa sababu, kiukweli, sio tu mgogoro wa Msumbiji na hivi karibuni utahusisha eneo lote na athari ya mali na uchumi kwa maisha na maisha ya maskini wa mkoa huu” wanaonya Foccisa.

Viongozi wa Kikristo pia wanageukia watendaji wa kiuchumi, hasa kwa kampuni zinazohusika na uchimbaji wa maliasili katika mkoa ambao wanasema, lazima wachangie kutafuta suluhisho la kudumu na sio tu kuhakikisha usalama wa shughuli zao. “Tunatoa wito kwa kila sekta ichukue jukumu lake katika saa ya uhitaji ”. Aidha wanawaalika hata waendeshaji wa mtandao wa simu za mikono kutoa simu  bure au angalau sehemu yao ili watu waombe msaada. Kwa namna ya Pkee viongozi wa Kanisa wanasema “inahitajika kusaidia waathiriwa dhaifu kama vile watoto, mama, walemavu, wagonjwa wa muda mrefu na wazee; hata hivyo bila kusahau waathiriwa wa Covid-19, ambao wanapambana na upumuaji”. Hatimaye wito kwa Umoja wa Mataifa ufuatilie kwa karibu mgogoro wa Msumbiji na mizozo yote inayotishia bara la Afrika leo hii kabla haijachelewa sana. Kwa upande wao, tamko hilo linahitimisha, Makanisa ya Kikristo ya kusini mwa Afrika  kuwa yataungana katika maombi na Baraza la Makanisa la Msumbiji kuomba zawadi ya amani katika nchi hizi.

06 March 2021, 12:43