Tafuta

Vatican News
Kuanzia tarehe 5 hadi 12 Septemba 2021 Kongamano la Ekaristi kimataifa jijini Budapest nchin Hungaria litafanyika Kuanzia tarehe 5 hadi 12 Septemba 2021 Kongamano la Ekaristi kimataifa jijini Budapest nchin Hungaria litafanyika 

Kard.Erdo:Hungaria ina njaa ya Ekaristi,Papa atashuhudia tumaini!

Askofu Mkuu Kardinali Erdo wa Esztergom-Budapest akitoa maoni yake kuhusu tangazo la Papa la matarajio ya uwepo wake katika misa ya kufunga Kongamano la Kimataifa la Ekaristi litakalofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 12 Septemba katika mji huo amesema“ni wote na si wakatoliki tu,wana shauku kubwa ya Papa na itakuwa mwanga baada ya giza nene na janga".

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kardinali Peter Erdö, Askofu Mkuu wa Esztergom-Budapest na Mkuu wa Kanisa la Hungaria, anatazama kwa matumaini na matarajio ya Kongamano la Ekaristi kimataifa ambalo litafanyika katika Mji Mkuu wa Ungaria kuanzia tarehe 5 -12 Septemba  2021. Kwa moyo mkuu na furaha ambayo imejionesha katika maneno ya Papa Francsko, wakati akizungumza na kujibu waandishi wakati wanarudi kutoka Iraq, ya kwamba anatamani awepo katika Misa ya kufungwa kwa  kongamano hilo. Kwa upande wa  waamini wake katika nchi hiyo amesema: “Hata kama  kipindi hiki  huku Budapest uwepo wa waamini katika misa umesitishwa kutokana na janga la virusi vya corona, makanisa hayajafungwa, watu wanakuja kusali mbele ya ekaristi Takatifu. Ni jambo la kushangaza sana kuwaona  kiu na njaa ya watu hawa kwa ajili ya Ekaristi”.

Kardinali Erdö akisimulia jinsi Kanisa lilivyosikiliza maneno ya Papa wakati wa mkutano huo amesema, walisikiliza kwa  kwa furaha kubwa, lakini si tu wakatoliki bali ni jamii nzima ya Hungaria. Hata katika televisheni za kitaifa zilitangaza mara moja habari iyo na hata jumuiya mbali mbali za kidini, makundi ya kijamii na wote wanashauku kubwa. Wanamsubiri Papa kama ushuhuda wa Matumaini na kwa sababu uwepo wake unaweza kuleta matumaini zaidi katika giza na janga la sasa.  Kardinali Erdo amesma “Kwa sasa ni kuanza kwa upya maisha, kujipyaisha neema ya roho na ndiyo kweli lengo la mkutano huo”. Ni matumaini ya Kardinali kuwa wanaweza kukutana na Kristo huko Budapest, kwa namna ya sherehe kubwa mwezi Septemba

Kongamano kwa hakika litafanyika kwa mujibu wa Kardinali Erdö, baada ya kuahirishwa mwaka jana 2020 hadi 2021 kwa sababu ya Covid-19  na hakuna shaka, wako wanajiandaa kikamilifu licha ya maongezeko virusi. Mpango wa Papa Francisko wa kuadhimisha Ekaristi na kutoa baraka ni katika Uwanja wa Mashujaa mahali ambapo wanakaribisha Kongamano la 53 la Ekaristi. Karibu na Altare ya Misa ya Mwisho huko di Budapest, mchana tarehe 12 Septemba, kutakuwa hata na Msalaba wa Utume ambao ni ishara ya tukio ulichongwa na  mnamo 2007 katika fursa ya utume wa kimisionari na msanii orafo Csaba Ozsvári, aliyeaga dunia 2009.

Msalaba huo una urefu wa Mita 3,20, ndani ya mti wa mwaloni unaofunikwa na karatasi ya shaba ambayo imewekwa katika kisanduku cha Msalaba Mtakatifu na masalio ya watakatifu wa Hungaria, kutoka kwa Mtakatifu Adalbert hadi Mtakatifu Stefano, kutoka kwa Mtakatifu Thomas Becket hadi mwenyeheri Papa Innocent XI na mwenyeheri Anna Kolesár. Papa Francisko alibariki Msalaba (ambao sasa huko katika hija nchini Hungaria, lakini umewekwa katika Kanisa Kuu Esztergom) tarehe 20 Novemba 2017 , mwanzoni mwa ziara  ya kitume ya maaskofu wa Hungaria jijini Roma, akizindua kama ishara ya upyaisho wa kweli wa watu wa Hungaria kuanzia na thamani ya Injili na Ekaristi. 

13 March 2021, 17:18