Tafuta

Vatican News
2018.12.06 Chuo Kikuu cha Mtakatifu Patrick huko Maynooth, Ireland 2018.12.06 Chuo Kikuu cha Mtakatifu Patrick huko Maynooth, Ireland 

Ireland:Mwanake mlei wa kwanza kuongoza kitengo cha kitaalimungu huko Maynooth

Baraza la Maaskofu Kitaifa nchini Ireland,katika siku kuu ya Mtakatifu Patrick msimamizi wa nchi hiyo,wametangaza uteuzi wa mwanamke wa kwanza na mlei wa kwanza kuwa rais wa kitengo cha Kitaalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Maynooth.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Dk. Jessie Rogers ni mwanamke wa kwanza na mlei wa kwanza kuteuliwa kuwa mkuu wa Kitivo cha Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Maynooth, nchini Ireland. Tangazo hilo lilitolewa tarehe 17 Machi 2021 na Baraza la Kitaifa la Maaskofu katika Siku  kuu ya Mtakatifu Patrick msimamizi wa nchi hiyo , na barua ambayo maaskofu wanasema kuwa “wanafurahi na habari hiyo” na kusisitiza kwamba Dk. Rogers anakuwa na jukumu lake jipya la uzoefu wa kimataifa na wa kiekumene. Bi Roger asili yake ni kutoka Afrika Kusini ambaye alianzia masomo yake ya Chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch, kilomita 50 kutoka mji wa Cape. Baadaye alihamia Ireland mnamo 2000, na kufundisha katika Chuo cha Bikira Maria hasiye na doa kabla ya kujiunga na Kitivo cha kitaalimungu katika Chuo cha Mtakatifu Patrick mnamo 2014.

Msomi wa maandiko mtakatifu na mtaalamu wa Agano la Kale

Bi. Roger ni msomi wa Maandiko Matakatifu na mtaalamu katika Agano la Kale, ambaye amejikita katika kazi yake ya kielimu hasa kwenye fasihi ya hekima ya kibiblia. Katika miaka ya hivi karibuni, ameongezea nyanja yake ya utafiti ambayo ni pamoja na mafunzo ya kiroho na kujizatiti katika Taalimungu ya utoto wa Yesu. Pamoja na majukumu mengine, Mkuu mpya huyo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kibiblia ya Kiairland, Jumuiya ya Afrika Kusini ya Mafunzo ya Mashariki ya Karibu; wa Jumuiya ya Ulaya ya Taalimungu Katoliki na Chuo cha Kimataifa cha Wakufunzi wa Uchaji au Taasisi ya Mafunzo ya Kichungaji ya Ireland. Ikumbukwe kwamba Chuo cha Mtakatifu Patrick huko Maynooth kinakaribisha Chuo Kikuu cha Kipapa na Seminari ya Kitaifa. Kwa sasa, wanafunzi 765, na miongoni mwao wa shahada ya kwanza wameandikishwa katika Chuo Kikuu hicho.

18 March 2021, 14:37