Tafuta

2021.03.02:ZIARA YA KITUME YA PAPA FRANCISKO NCHINI IRAQ TAREHE 5-8 MACHI 2021 2021.03.02:ZIARA YA KITUME YA PAPA FRANCISKO NCHINI IRAQ TAREHE 5-8 MACHI 2021 

Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:habari katika picha!

Ni sherehe kubwa ya wanairaq kumkaribisha Papa Francisko.Ni masaa machache yameabaki na Papa atakuwa katika Nchi hiyo ya kihistoria katika maisha ya uzao wa Ibrahimu.Kila sehemu na kila mahali kuna shangwe na shauku ni kubwa ya kumpokea Papa katika nchi hiyo.Maandalizi ya mikutano,sala na nyimbo zimeandaliwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Udugu nchini Iraq ni wema wa kuhimiza na kukuza ndiyo ujumbe wa Jumuiya ya Papa Yohane wa XXIII iliyoundwa na Padre Oreste Benzi kwa ajili ya Papa Francisko ambaye anakwenda ziarani nchi za Mashariki.

MAANDALIZI YA KUMPOKEA PAPA
MAANDALIZI YA KUMPOKEA PAPA

Wito ni mshikamano na udugu ili watu wa Iraq kwa kusaidiwa hata na Jumuiya ya Kimataifa ili waweze kushinda kila aina ya changamoto zilizopo mbele yao. Ni wito uliotolewa na Jumuiya ya hiyo ya Yohane XXIII ambayo inafanya kazi nchini Iraq na kwamba katika fursa hii ya ziara ambapo wote kwa pamoja wanakumbatia kikamilifu ujumbe wa Papa Francisko ambao anaupeleka kwa watu wa Iraq huku wakiamini kuwa ni namna ya kufanya wawe na uponywaji wa majeraha ya wakati uliopita ili kujenga wakati bora katika jumuiya mbali mbali za nchi.

KANISA KUU BAGHDAD
KANISA KUU BAGHDAD

Katika ujumbe mwingine wa pamoja wa mashirika ya kidini nchini Iraq wamemwelekeza Papa Francisko katika ziara yake kwamba kwa mara ya kwanza Papa anakwenda katika Nchi yao na kupyaisha jitihada kwao za ujenzi wa kiungo kimoja cha kijamii kilicho chanika na ili waweze kuishi kwa pamoja kama ndugu.

MAANDALIZI
MAANDALIZI

Kwa maana hiyo ni  masaa machache ambapo Papa Francisko atakuwa katika nchi ya Iraq ambayo inamsubiri kwa hamu kubwa na maandalizi mazuri. Vijana wengi sana wanamsubiri Papa Francisko na ambao wanasemea  walio wengin wameteseka sana na wanataka kuwa na amani.

KARDINALI SAKO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU ZIARA YA PAPA
KARDINALI SAKO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU ZIARA YA PAPA

Nchini Iraq, asilimia 57% ya idadi ya watu iko chini ya umri wa miaka 25. Kwa maana hiyo Papa Francisko atatembelea nchi inayoweza kuwa na utajiri mkubwa wa nguvu muhimu. Vita vimejaribu kuzima ndoto, lakini matumaini ya siku zijazo ni mazuri na bado yanaendelea kuwa hai. Ni wengi ambao wanatoa ushuhuda wa vita ambavyo hawatavisahau wakikimbuka hata ving'ora vitani.

MABANGO YA UJIO WA PAPA
MABANGO YA UJIO WA PAPA

Lazima tuombee safari hii. Sio safari  kwa ajili ya Wakristo wa huko tu, au kwa nchi moja. Ni safari kwa ajili ya nchi za  Mashariki. Tunaomba ili isaidie kila mtu: Wasunni, Washia na hata Wakristo kuwa wakweli katika mazungumzo. Ndivyo  Padre Jacques Mourad, mtawa mmonaki mkatoliki wa Siria wa jumuiya ya Deir Mar Musa, ambaye anajiandaa kuishi na kufuatia kiroho, yeye akiwa nchini Siria,  ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko, kwenda nchi jirani ya Iraq kunzia tarehe 5-8 Machi 2021.

MTAWA AKIWA ANAPANGA RANGI MSALABA
MTAWA AKIWA ANAPANGA RANGI MSALABA

Kwa njia hiyo Jumuiya mbambali za watawa wa kike na kiume wamejikita katika maandalizi na kuwaanda waamini kiroho ili kumpokea kwa imani na upendo kiongozi mkuu wa Kanisa. Vijana wamekuwa mstari wa mbele katika harakati za maandalizi. Padre Mourd anaendelea kueleza kuwa  ziara ya Papa inawakilisha hata fursa ya kipekee katika kuonja kwa namna moja wito wa jumuiya za kikristo za wazawa yaani wa nchi za Mashariki. Utume wake wa jumuiya zenyewe katika nchi zao, ndiyo namna ya kuishi kwa unyenyekvu na umaskini katikati ya waislamu.

MADHEHEBU YOTE KUISHI KAMA NDUGU
MADHEHEBU YOTE KUISHI KAMA NDUGU

Kwa njia hiyo ni kama, kulinda hata matarajio ya Yesu aliyeko hata katika tamaduni ya Waislamu. Bila utume huu, uwepo wa Wakristo wa nchi za Mashariki  hauwezi kuwa na maana. Kila kitu kinakuwa kugumu kwa Wakristo, na pia kwa wengine, ikiwa Wakristo hawabebi tumaini la Kristo pamoja nao Kwa kuishi uzoefu wake wa ushirikiano na wakimbizi Wakristo waliokimbia makazi yao huko Qaraqosh, Padre Mourad amefanya uzoefu kwa mara nyingine tena jinsi inavyotakiwa si kutafuta msaada wa kisiasa, uchumi au kijiografia kwamba ni  vitu ambavyo vinaweza kuwa muhimu katika kuhakikisha kukaa kwao katika maneno ya Nchi za Mashariki, na kumbe nguvu moja ya wakaristo ni kuishi upendo wa Yesu, na hakuna upendo mwingine zaidi y aule wa kufikia msalabani.

WATU WA KUJITOLEA WAKIONESHA MABANGO YA KUKARIBISHA PAPA
WATU WA KUJITOLEA WAKIONESHA MABANGO YA KUKARIBISHA PAPA

Padre Mourd amesema:“Wakristo wa Iraq tayari wameishi na wanaendelea kuishi ushuhuda wao wa Kikristo kwa njia isiyo ya kawaida, katika miaka yote ya vita. Sasa, kwa maana hiyo wale ambao wameshiriki katika siri ya Kristo hawana masilahi mengine, hawana maneno mengine ya kuongeza. Katika siku zao wanaishi hali ya kiroho ya msalaba wa Yesu, ambayo tulijivika wakati wa kupokea upako na mafuta, mara tu baada ya kubatizwa, kulingana na ibada za Makanisa yetu”.

AFISA USALAMA KATIKA HUDUMA YA ULINZI WA KANIZA LA MAMA YETU
AFISA USALAMA KATIKA HUDUMA YA ULINZI WA KANIZA LA MAMA YETU
04 March 2021, 19:32