Tafuta

Siku ya Ufufuko Yesu anamwambia Maria Magdalena usinishike bali kimbia ukawatangazie wanafunzi wangu Siku ya Ufufuko Yesu anamwambia Maria Magdalena usinishike bali kimbia ukawatangazie wanafunzi wangu 

Canada:Pasaka ni ishara ya Kanisa la tumaini na furaha

Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Canada,Askofu Richard Gagnon,katika ujumbe wake wa Pasaka kwa waamini wake amechagua sura ya Maria Magdalena aliyekimbia kutangaza ufufuko wa Bwana kwa Mitume.Askofu Mkuu amesema Pasaka ni Siku kuu ya ishara ya Kanisa moja ambalo linakwenda mbele kwa tumaini na furaha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maria Maddalena aliyekimbia  kuwatangazia wanafunzi  kuwa Kristo amefufuka ndiyo sura aliyochagua Askofu Mkuu Richard Gagnon,wa Jimbo Kuu Katoliki la Winnipeg, na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Canada wakati akifungua ujumbe wake katika fursa ya Siku kuu ya  Pasaka kwa waamini wake. Askofu amebainisha kuwa  Maria Magdalena kiukweli anawakilisha Kanisa lenyewe kuwa linakwenda mbele kupeleka ujumbe wa matumaini na furaha. Hisia mbili ambazo zimebainisha Askofu na ambazo ni muhimu sana baada ya mwaka wa Covid-19, kwa kuishi kipindi cha kufungwa, vizuizi, kutokuwa na uhaika, kufutwa kwa misa , kukata tamaa, magonjwa na vifo. “Tumeona jumuiya zetu za kikanisa zinateseka kwa ukima, askofu Mkuu Gagnon na kuongeza kuwa   makanisa yaliyofungwa ndani na huku nchi ikizidiwa na maumivu”. Lakini licha ya hayo anaongeza kiongozi huyo kuwa, familia zao za Kikristo zinaendelea kuwa mahali ambapo imani ni hai  hata kushamiri. Na sasa, hasa kwa nguvu na kampeni ya chanjo, pia kwa kufungua tena maeneo ya ibada katika maeneo mengi ya nchi na katika hali ya hewa ya joto wanaweza  kutazamia siku za usoni zilizo bora kwa maana ya hali mpya ya matumaini.

Kwa kuongezea Mari Magdalene, rais wa Braza la Maaskofu nchini Canada  CCCB) amekumbuka alama nyingine muhimu,  ile ya mshumaa wa Pasaka ambao huangaza gizani kutukumbusha kuwa Yesu ndiye nuru ya ulimwengu. Wakati wa Mkesha wa Jumamosi Takatifu,  amesema mshumaa wa Pasaka hutembea kando ya barabara ya makanisa ukifuatana na maneno yasemayo “ Mwanga wa Kristo, Je  siyo ishara ya kile  ambacho wanaitwa kufanya wanapoendelea  katika janga hili? Je! Hawakuitwa kuwa ishara za matumaini wanapojenga tena jamii zao  baada ya uharibifu uliosababishwa na virusi vya corona  mwaka jana? Kwa upande wa Askofu Mkuu wa Winnipeg pia ushauri wake ni kujifunza kutokana na uzoefu wa mwaka jana ili kulifufua Kanisa. “Janga hili, kwa hakika limetufundisha jinsi imani yetu ilivyo muhimu, nzuri na ya thamani; sakramenti ni muhimu sana kwetu sisi; Imeonesha ni kiasi gani Neno la Mungu limejaa matumaini kwetu”. Kazi ya waamini, kwa maana hiyo itakuwa ile ya kujenga upya, kupyaisha, kutangaza, kwenda nje na kuwa nuru itakayooneshwa katika Mkesha wa Pasaka. “Hili ni Kanisa baada ya gonjwa!, amerudia kusisitiza askofu wa Canada.

Ujumbe wa maaskofu kwa njia ya rais wao unazingatia miaka miwili maalum iliyotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko: ule uliowekwa wakfu kwa Mtakatifu Yoseph, kwenye maadhimisho ya miaka 150 tangu kutangazwa kwake kama Msimamzi wa Kanisa la ulimwengu, mbayo unaendelea hadi tarehe 8 Desemba ijayo, na Mwaka wa Familia Amoris Laetitita, iliozinduliwa mnamo tarehe Machi 19 mwezi huu kuadhimisha miaka mitano tangu kuchapishwa kwa Wosia wa Kitume wa Famiglia-Amoris Laetitita, juu ya Upendo ndani ya familia. Kutokana na mipango hii yote miwili, Askofu Gagnon amesisitizia, juu ya msukumo ambao unatkiwa uibuke ili kuamka, kutembea, kusonga mbele kwa kufanya wema kwa ajili ya jumuiya zetu, hata kupita zaidi ya mipaka yao”.

Kuhusiana na hilo, Askofu Mkuu wa Winnipeg amekumbuka ziara  ya kitume ya hivi karibuni ya Baba Mtakatifu Francisko kwenda Iraq, ambayo ilifanyika tangu tarehe  5 hadi 8 Machi, na jinsi Papa alivyowahimiza Wakristo wa nchi hiyo iliyoteswa kurudi na kuchukua jukumu la kujenga upya jumuiya yao pia kwa kutazama familia kama Makanisa ya nyumbani, mahali ambapo imani inaishi na kulishwa, na kama chanzo cha furaha na upendo wa ukarimu hata katika majaribu na shida. Katika Pasaka hii, labda zaidi ya hapo awali amesisitiza rais wa Baraza la Maaskofu nchini Canada (Cccc) kuwa kuna sababu nzuri ya kuwa na imani na kuishi ukweli na uhalisi wa kweli wa Kikristo, kwa kuzingatia taa na vivuli vyote. Kuwa na imani ya Pasaka, kwa hakika inamaanisha tu kuamini kwamba mkono wa Mungu unaweza kuwepo kila mahali, kwa sababu vitu vyote hufanya kazi pamoja kwa faida ya wale wanaompenda Bwana.

31 March 2021, 13:17