Tafuta

2021.03.08  Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:Mazungumzo na waandishi wa habari kwenye ndege 2021.03.08 Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:Mazungumzo na waandishi wa habari kwenye ndege 

Amerika Kusini:Ziara ya kitume ya Papa nchini Iraq izae matunda.

Shukrani kwa Papa zinatoka Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barani Amerika Kusini(Celam) kutokana na ziara yake ya kutembelea Jumuiya ndogo na inayoteseka katoliki ya Iraq.Ujumbe wa Celam unahitimishwa kwa mwaliko wa Maaskofu wote wa Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien ili kuendeleza uhamasishaji wa sala isiyo na mwisho kati ya makuhani,watawa na waamini walei ambayo inamsindikiza Mfuasi wa Petro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amerudi mjini Vatican tarehe 8 Machi 2021 kutoka Iraq. Kwa watu wengi wameifikiria safari yake ni ya kihistoria ambapo miongoni mwao  ni Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini (CELAM). Katika ujumbe wao bada ya zira hiyo, Maaskofu hao wanaelezea shukrani zao kwa Papa Francisko kwa kufanya ziara hiyo katika Nchi ambayo inaishi jumuiya ndogo katoliki na inayoteseka. Celam inaonesha ukaribu wake na kusali ili ziara yake ya kichungaji aliyohitimisha katika muktadha wa janga la Covid-19, na ambalo linaendelea kuumiza ulimwengu mzima, iweze kuleta matunda. Maaskofu wanabainisha katika ujumbe huo kwamba imekuwa ziara ya kutunza ustaarabu ambao unaonesha ishara ya Baba yetu Ibrahimu ambaye anaunganisha Wakristo, Wayahudi na Waislamu na kufanya kuwa wajumbe wa familia moja ya kibinadamu.

Papa ametembelea watu walioteseka

Huu ni ushuhuda wa ujasiri uliooneshwa na Baba yetu mpendwa Papa Francisko, kwa kutembelea wale ambao wanateseka kutokana na matokeo ya itikadi kali za kidini na hadi kufikia kufiadini wamesisitiza maaskofu hao. Papa Francisko alijiwakilisha kwao kama mwanahija wa kidugu ulimwenguni na ziara yake itakuwa chombo ambacho bilashaka kitawatia moyo na kuwaimarisha imani katika Kanisa hili linaliteseka. Ziara hii ya Papa nchini Iraq, itakuwa sehemu ya matukio muhimu zaidi ya historia na itabaki imesimikwa mzizi ndani ya mioyo ya ndugu zetu wairaq ambao hawatasahau kamwe kuwa Baba Mtakatifu mwenyewe alikwenda katikati yao”, wanaeleza.

Ziara ya Papa itahamasisha heshima ya utakatifu wa maisha

Matumaini ya Celam lakini pia uhakika ni kwamba safari hiyo itaweza kusaidia kushinda chuki na vurugu, kwa kuhamasisha zaidi heshima ya utakatifu wa maisha. Wanamshukuru tena Papa kwa ajili ya ushuhuda wake wa ukaribu na wale ambao wanakabiliana na matokeo ya vita, kuteswa na matatizo. Ujumbe wa Celam unahitimishwa kwa mwaliko wa Maaskofu wote wa Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien ili kuendeleza uhamasishaji kati ya makuhani, watawa, na waamini walei, sala isiyo isha ambayo inamsindikiza Mfuasi wa Petro ili ziara yake ya kitume nchini Iraq izae matunda mengi ya kichungaji na kuhamasisha zaidi mazungumzo ya kidini.

09 March 2021, 15:55