Tafuta

Vatican News
2021.02.15: Nembo ya Mkutano wa Vijana na Papa nchini Iraq. 2021.02.15: Nembo ya Mkutano wa Vijana na Papa nchini Iraq.  

Iraq,Sako:Ziara ya Papa sio kutatua matatizo ya nchi

Katika fursa ya maandalizi ya ziara ya Papa Francisko nchini Iraq inayotazamiwa tarehe 5 hadi 8 Machi ijayo,Patriaki wa wa Walakaldayo amesma kuwa ni makosa kufikira kwamba ziara ya Papa ni kutatua matatizo yao yote.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Patriaki Kikaldayo, Kardnali Louis Raphael Sako akijibu kwa taarifa rasmi kwa wale ambayo wameonesha matazamio tofauti kuhusu ziara  Papa Francisko nchini Iraq yaliyosambazwa kupitia vyombo vya kijamii iliyopangwa kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi ijayo, amesema “Papa Francisko haji Iraq kutatua shida zetu zote za jumuiya za Kikristo katika eneo hili. Na hamtazmi yeye kuwarudisha Wakristo ambao walihamia nje ya nchi Iraq, au kupata mali zao zilizoporwa. Badala yake, ni serikali ya Iraq inayotakiwa kuunda mazingira yakuwezesha hali hiyo ya kurudi.”

Katika taarifa hiyo fupi, iliyotolewa na idhaa rasmi za Upatriaki wa Kikaldayo, Patriaki Sako amebaini kuwa Papa hataweza kutembelea madhabahu yote, lakini wakati huo huo ameangazia umuhimu mkubwa wa ishara ya maeneo yanayoguswa na ziara ya kipapa ambayo ni pamoja na Uru, Najaf, Mosul na Quaraqosh, mahali ambapo askofu wa Roma ataweza kueneza maneno ya upendo, udugu, upatanisho, uvumilivu na kuheshimu maisha, utofauti na wingi wa tamaduni.

Wakati huo huo, kwa siku hizi, Patriaki wa Kikaldayo, Kardinali Louis Raphael Sako anaendelea kukutana na wawakilishi wa taasisi, vikosi vya kisiasa na vikundi vya kijamii na kidini, wote wakiwa na hamu ya kuonesha nia na kuridhika kwa ziara ijayo ya Papa Francisko. Miongoni mwa wengine, Patraki pia amepokea uwakilisho kutoka muungano wa kisiasa wa Washia al Hikma (Harakati ya Hekima ya Kitaifa pamoja na mbunge Saib Khidir, mwakilishi wa watu walio wachache wa Yazidi).

19 February 2021, 14:54