Tafuta

Vatican News
ASKOFU  MKUU  MIGUEL CABREJOS WA JIMBO KUU KATOLIKI  TRUJILO (PERU) NA RAIS WA CELAM ASKOFU MKUU MIGUEL CABREJOS WA JIMBO KUU KATOLIKI TRUJILO (PERU) NA RAIS WA CELAM 

Siku ya kimataifa ya udugu wa kibinadamu:pyaisheni jitihada za Aparecida na kuunda uhusiano kidugu na mshikamano

Kwa upande wa Askofu Mkuu Cabrejos,rais raisi wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika ya Kusini (celam)anasema udugu kibinadamu maana yake ni kuwa na mshikamano wa kweli,uhusiano na kuacha ujuu juu,kukataa sera za uwongo ambazo zinatafuta itikadi tu na kuchanganya idadi ya watu,hasa maskini na wanyenyekevu,wakisahau utetezi wa afya na utu wa binadamu.Ni katika muktadha wa kuadhimisha Siku ya I ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu na kuishi kwa pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya udugu wa kibidamu, iliyofanyika tarehe 4 Februari, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini (CELAM) Askofu Mkuu Miguel Cabrejos Vidarte, wa jimbo Kuuu Katoliki  Trujillo (Perù),ametoa mwaliko wa kupyaisha jitihada zilizochukuliwa na Baraza la V kuu la Shirikisho la Celam huko Aparecida, mahali ambamo walikuwa wanasisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa umoja, kama wafuasi wamisionari ili kufanya uzoefu wa kweli wa uhusiano kidugu na mshikamano kati ya watu wao.

Kukataa sera za uongo

Kwa upande wa Askofu Mkuu Cabrejos, hii ina maana ya kuweka mbali ujuu juu  na kukataa sera za uwongo ambazo zinatafuta itikadi tu na kuchanganya idadi ya watu, hasa maskini na wanyenyekevu, wakisahau utetezi wa afya na utu wa binadamu. Na hii hasa katika wakati wa sasa wa kihistoria, ambao mwanadamu ameitwa kutembea ili kuelekea kwa mwingine, kujenga urafiki wa kijamii ulio wa kweli na undugu wa ulimwengu.

Ni kujenga mchakao wa udugu

Hata mabaraza ya Maaskofu, majimbo, mashirika ya Bara la Amerika ya Kusini wamewaalikwa kuadhimisha Siku hiyo ambayo imefanyika kwa mara ya kwanza kwa tafakari kuu hasa ya kujikita katika matendo ya kweli. Wengine, kama Baraza la Maaskofu wa Costa Rica (Cecor) wametoa ujumbe wao kwa waamini wote na madhehebu mengine ya kidini, watu wenye mapenzi mema kujenga mchakato wa udugu na haki kwa ajili ya wote.

Ni kwa njia ya kutunza mmoja na mwingine inawezekana kuunda dunia iliyo bora

Wakati ambapo janga la Covid-19 limeathiri ubinadamu wote, wanaomba watu watafakari  juu ya matendo yao, ili waweze kuchangia zaidi kila siku katika ujenzi wa ulimwengu bora na unaojali zaidi, ambao unafuata njia za amani, ambazo hutafuta halisi nzuri ya pamoja. Ni kwa njia hiyo tu wanaweza kutunza kila mmoja na nyumba ya kawaida ambayo watu wote wanaishi kwa pamoja, wamebainisha katika ujumbe huo uliotiwa saini na rais wa Cecor, Askofu  José Manuel Garita, wa Jimbo katoliki la Ciudad Quesada.

06 February 2021, 15:46