Tafuta

Vatican News
Kwa upande wa Kanisa la Marekani serikali ya shirikisho ina jukumu msingi katika kushinda na kusahihisha historia ya ubaguzi ambao umeshamiri nchini humo Kwa upande wa Kanisa la Marekani serikali ya shirikisho ina jukumu msingi katika kushinda na kusahihisha historia ya ubaguzi ambao umeshamiri nchini humo 

Usa:Maaskofu wanapongeza hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi

Maaskofu nchini Marekani wanaelezea matumaini kwamba utawala mpya utafanya kazi muhimu ya kukuza usawa wa makazi na hadhi ya binadamu.Vile vile viongozi wanapongeza kutorejeshwa tena kwa mikataba na vituo vya kizuizini vya kibinafsi,ambapo Maaskofu wameonesha ufanisi mara kadhaa.Hizi ni amri mbili mpya za utendaji kutoka kwa Rais Joe Biden zinazolenga kuhamashishaa usawa wa rangi katika sera za makazi na magereza nchini Marekani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maaskofu nchini Marekani waneonesha kufurahishwa kwano na hatua mbili mpya. Wa kwanza kurejeshwa  kwa “Kanuni ya Kuongeza Haki ya Makazi” (Affh), kifungu kilichozinduliwa mnamo 2015 na utawala wa Obama ili kufanya kuwa ufanisi zaidi wa vifungu vilivyoletwa mnamo 1968 dhidi ya ubaguzi wa makazi dhidi ya wachache. Msimu wa kiangazi uliopita, kifungu hicho kilifutwa na kubadilishwa na kanuni mpya iliyoitwa “Kulinda Jumuiya na Chaguo la Jirani” ambalo lilibatilisha vita dhidi ya vitendo vya kibaguzi kama vile kukataliwa kwa uwekezaji wa maendeleo ya miji katika vitongoji vilivyo na watu wachache au katika uuzaji na upangishaji ya nyumba.

Amri ya pili ya utendaji, kwa upande mwingine, inahitaji Idara ya Sheria kutosasisha mikataba yake na magereza binafsi katika ngazi ya shirikisho. Kiukweli nchini Marekan, idadi kubwa ya wafungwa zaidi ya milioni mbili wanashikiliwa katika vituo vya kibinafsi, vinavyojulikana kuwa katika hali mbaya ambayo wafungwa wanashikiliwa na tabia mbaya ya walinzi wa magereza. Hatua hiyo ni hatua ya kwanza katika mageuzi mapana ya mfumo wa magereza yaliyotangazwa na Rais Biden kuifanya iwe ya kibaguzi kidogo na kuwezesha ukarabati na uingizaji wa kijamii wa wafungwa.

Kulingana na maaskofu, hatua hizo mbili ni hatua ya kwanza katika mwelekeo sahihi. Kwa maana hiyo inaoneshwa tamko lililotiwa saini na Asofu Paul S. Coakley, rais wa Tume ya Haki na Maendeleo ya Binadamu ya Baraza la  Maaskofu Marekani  (Usccb), na Askofu  Shelton J. Fabre, rais wa Tume ya Maaskofu dhidi ya ubaguzi wa rangi. Katika barua hiyo inabainisha kuwa kufutwa kwa kanuni ya Affh chini ya urais wa Trump ilikuwa imepunguza jukumu la utawala wa umma kukuza ufikiaji sawa wa makazi kupitia hatua za kudhibitisha. Kwa upande wa Kanisa la Marekani hata hivyo, serikali ya shirikisho ina jukumu  msingi katika kushinda na kusahihisha historia ya ubaguzi ambao umeashiria nchi hiyo.

Kwa njia hiyo maaskofu wanaelezea matumaini kwamba utawala mpya utafanya kazi hii muhimu ya kukuza usawa wa makazi na hadhi ya binadamu. Vivyo hivyo, viongozi hao wa Kanisa  pia wanapongeza kutorejeshwa tena kwa mikataba na vituo vya kizuizini vya kibinafsi, ambapo Baraza la Maaskofu Marekani (Usccb) wameonesha ufanisi mara kadhaa. Matumaini yao ni kwamba hatua hiyo mpya pia itaenea kwa vituo vya wafungwa wahamiaji wasio kuwa halali.

04 February 2021, 14:06