Tafuta

Vatican News
Virusi vya Corona:Kesi za vurugu dhini ya wanawake zimeongezeka zaidi kutokana na dharura ya covid-19 Virusi vya Corona:Kesi za vurugu dhini ya wanawake zimeongezeka zaidi kutokana na dharura ya covid-19  (ANSA)

Caritas:Janga la Covid lemezidisha vurugu dhidi ya wanawake

Janga la covid-19 limeongeza vurugu dhidi ya wanawake.Jambo hilo la kusikitisha linazungumziwa katika barua iliyochapishwa na Caritas ya Kiambrosi Jimbo Kuu Milano kwa kuzingatia Siku ya Kimataifa ya Maombi na Tafakari kuhusu biashara Haramu ya Binadamu,ambayo itaadhimishwa tarehe 8 Februari ijayo,sambamba na kumbu kumbu kiliturujia ya Mtakatifu Josephine Bhakita.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika kujiandaa kwa Siku ya Maombi Dhidi ya biashara Haramu ya binadamu, Caritas ya kiambrosi, ikishirikiana na mashirika mengine pamoja na Kituo cha kimisionari cha  PIME, wanahamasisha mkutano wao uliopewa jina  “Biashara haramu, ukahaba na utumwa. Mipaka mipya na changamoto mpya” utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 6 Februari 2021. Mkutano huo utatangazwa moja kwa moja kwa njia ya mtandao kuanzia saa 4.00 hadi 6.00 kamili mchana. Hata hivyo janga la Covid-19 limewafanya wanawake kuzidi kuwa katika mazingira magumu na kusumbuliwa na kwa  njia hiyo  wahanga wa unyanyasaji na manyanyaso bado yapo makubwa zaidi kuliko zamani. Ni mbiu iliyotolewa na kituo cha Caritas ya Kiambrosi katika barua iliyochapishwa katika fursa hiyo ya Siku ya Kimataifa ya Maombi na tafakari dhidi ya biashara ya binadamu. Kwa mujibu wa barua hiyo inasema hali ya utumwa ambamo wameshikiliwa pia imeongezwa kwa kiwango kisichokuwa cha kawaida cha shida isiyo ya kusema.

Kwa wastani, asilimia 70 yao wamelazimika kutafuta msaada wa vyakula, ambao hawakuhitaji hapo awali. Sio tu: kama anavyosema Sr. Claudia Biondi, Mhusika wa  eneo  linalohusu biashara na ukahaba wa kitengo cha Caritas  cha Ambrosi kwamba virusi vya corona imehamisha mchezo wa ukahaba zaidi na zaidi kupitia mtandaoni na kuwafanya wahanga kuwa wasioonekana zaidi, na ambapo  ni ngumu kuwafikiwa ikiwa siyo wateja na wanyonyaji, na kwa  njia hiyo wako na upweke na  kutengwa zaidi.

Kuhusu nchi asili za wahanga wa biashara ya binadamu, shirika la kutoa misaada la jimbo kuu la Milano limetangaza kuwa  nchini Romania iko katika nafasi ya kwanza, na 53% ya waliopo, ikifuatiwa na Albania na Nigeria, kwa asilimia 21 na 17. Walakini, kupungua kwa uwepo wa wanawake wa Kiafrika haimaanishi kuwa wako salama, na kwamba kutokana na kushindwa kuvuka Bahari ya Mediterania, wamebaki wafungwa katika kambi za mahabusu zilizopo Libia na huko, ili kuishi na kutumaini kupata pesa za kutosha kuendelea na safari, wanajitoa kwa walio wafunga. Vivyo hivyo hata kwa wasichana wa Niger, waliolazimishwa kujiuza kwa wanaume wanaohusika na uchimbaji wa dhahabu kwenye migodi, taarifa inabainisha.

Mahitaji ya ngono ya kulipwa, kiukweli hayajawahi kushuka, hata kufikia kushinda hofu ya kuambukizwa, Caritas ya kiambrosiana imesisitiza. “Inahitajika kuongezeka kwa dhamiri kwa upande wa wateja Haiwezekani kupunguza miili ya wanawake kama vile haina roho, lakini lazima kujifunza kutazama mchezo wa huu nyuma yake historia hadithi zao. Wakati huo huo, amebainisha, Bwana Luciano Gualzetti mkurugenzi wa Caritas ya kiambrosi Milano huku akitoa mwaliko wa   kutoa  kwa wahanga hawa kuwa  sio ukarimu tu, bali pia fursa halisi za kuingia kwenye soko la ajira, kwa sababu shida ya kijamii ambayo ilifunguliwa na janga haiwezi kuwa kisingizio cha kusahau juu ya wale wa mwisho, na kinyume chake, lazima iwe fursa ya kuanza kwa upya kuanza nao.

Ikumbukwe Siku ya tarehe 8 Februari ilizinduliwa mnamo 2015 na Baraza la Kipapa la wakati huo la Kichungaji kwa ajili ya Wahamiaji na Watu Wanaosafiri na Haki na Amani na Muungano wa vyama vya kimataifa vya wanawake na wanaume vya wakuu wa Mashirika ya kitawa. Maadhimisho hayo yamekusudiwa kuwa jibu wito wa  Baba Mtakatifu Francisko katika kupambana na hali ya biashara ya watu na kuwatunza wahanga. Uchaguzi wa tarehe iyo haukuwa wa bahati mbaya kwani tarehe 8  Februari,  kiukweli ni  kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Josephine Bakhita, mtumwa wa Sudan, aliayechiliwa huru na baadaye kujiunga na shirika la Wakanossian, na ambaye alitangazwa kuwa Mtakatifu mnamo 2000.

05 February 2021, 14:05