Tafuta

Vatican News
2021.02.17 Kipindi cha Kwaresima 2021.02.17 Kipindi cha Kwaresima 

Poland:Ujumbe wa pamoja wa Kwaresima wa makanisa ya Kikristo

Kipindi cha Kwaresima au wakati wa Mateso ni kipindi cha maandalizi kwa Wakristo wote ili kusherehekea fumbo mateso na Ufufuko,kipindi cha uongofu,sala,kufunga,kutoa sadaka na utunzaji maalum wa maskini na wanyonge,lakini lazima iwe kipindi cha kufanya uchunguzi binafsi wa dhamiri,kukiri kasoro,kurekebisha uharibifu uliosababishwa na matendo na kwa kutamka. vitendo vya upatanisho na kujitoa kuishi kiinjili.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kwaresima mwaka huu inaweza kufunga mioyo ya kuheshimu maadili ya pamoja ambayo ndiyo chanzo cha Injili. Tuache maneno yake yatutie moyo kuheshimiana na kuzungumza kwa pamoja.  Huo ni uthibtisho wa taarifa ya pamoja ya wasemaji wa makanisa ya madhehebu ya Kikristo huko Poland katika ujumbe wao wa pamoja katika fursa ya kipindi cha Kwaresima. Kulingana na kilichotolewa kwenye Tovuti ya Baraza Maaskofu wa Kipoland  hati hiyo ilisainiwa na Padri Leszek Gęsiak, msemaji wa Baraza la  Maaskofu wa Kanisa Katoliki; Agnieszka Godfrejów-Tarnogórska, msemaji wa Kanisa la Kiinjili nchini Poland; na Łukasz Leonkiewicz, msemaji wa Kanisa la Kiorthodox Poland.

Kipindi cha Kwaresima au wakati wa Mateso ni kipindi cha maandalizi kwa Wakristo wote ili kusherehekea fumbo mateso na  Ufufuko, kipindi cha uongofu, sala, kufunga, kutoa sadaka na utunzaji maalum kwa maskini na wanyonge, lakini lazima pia iwe kipindi cha kufanya uchunguzi binafsi wa dhamiri, kukiri kasoro, kurekebisha uharibifu uliosababishwa, kwa kutamka.  vitendo vya upatanisho na kujitoa kuishi kila siku kulingana namaelekezo ya Injili. “Kama wasemaji wa makanisa ya madhehebu ya Kikristo, tunataka kutoa wito kwa pamoja kwa wafuasi wote wa Kristo ili katika kipindi chote hiki cha mwaka ambacho kitufungue hata zaidi mwaka huu kuheshimu maadili yetu ya pamoja, ambayo chanzo chake ni Injili. Tuache maneno yake yatutie moyo wa kuheshimiana na kuzungumza kwa maana ya  kuimarisha vifungo vinavyoibuka katika shughuli zetu za kiekumene”.

Na kwa mujibu wa  msemaji wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini  Poland,  Padre Leszek Gęsiak, katika ujumbe wake amesema  “Lakini Kwaresima pia ni wakati mzuri wa kutekeleza ibada zetu zilizojikita katika mila na uchaji wa Kipoland, ambazo ni kielelezo cha mapenzi yetu kubadili mioyo yetu katika kipindi hiki maalum”. Kwa kuongeza amesema: “Tunajaribu kutafuta wakati wa kushiriki Njia ya Msalaba na pia katika mafungo kwenye jumuiya zetu za parokia, kwa kufuata kanuni za usalama kwa sababu ya dharura ya kiafya, ambayo ni kielelezo cha nia yetu ya kubadilisha mioyo yetu katika kipindi hiki maalum. Msemaji wa Maaskofu pia amewahimiza watu kutoa msaada wa vifaa: “Kazi za huruma ni kielelezo muhimu cha kujitoa kwetu katika kipindi cha Kwaresima. Bila wao, uongofu wa mioyo yetu na maana ya Kwaresima isingekuwa kamili. Tunakumbuka wagonjwa na wapweke kwa njia ya pekee, tukinyoosha mkono kwao” amehitimisha.

19 February 2021, 11:49