Tafuta

Vatican News
2021.02.02 Siku ya Watawa duniani 2021.02.02 Siku ya Watawa duniani 

Poland:Tumshukuru Mungu kwa walioitikia ndiyo wito wake!

Wakati tunasheherekea siku nyingine ya Watawa ulimwenguni,tumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote walioitikia wito wake.Ameandika hayo Monsinyo Jacek Kiciński,Rais wa Tume kwa ajili ya Mashirika ya Kitawa na vyama vya kitume ya Baraza la maaskofu nchini Poland katika ujumbe wa Siku ya Watawa duniani ambayo uadhimishwa kila tarehe 2 Februari sambamba na Sikukuu ya kutolewa kwa Bwana Hekaluni.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Askofu Jacek Kiciński, Rais wa Tume kwa ajili ya Mashirika ya Kitawa na vyama vya kitume ya Baraza la maaskofu nchini Poland, katika ujumbe wa Siku ya Watawa duniani inayoadhimishwa kila tarehe 2 Februari ameandika kwamba: “ Wakati tunasheherekea siku nyingine ya Watawa ulimwenguni, tumshukuru Mungu kwa watu wote ambao wameitikia wito wa wake. Kiongozi  huyo amekumbuka kwamba sikukuu hii, inayoitwa kwa kawaida sikukuu ya Mama yetu wa Ngurumo, imeunganishwa kwa kuwashwa mshumaa  ikiwa ni ishara ya nuru inayoondoa giza la maisha yetu: “Chanzo na kilele cha sala yetu ni Ekaristi Takatifu na Chakula  ambacho kinaturuhusu kubaki katika muungano na Mungu. Ni kwa nguvu tu inayotokana na Ekaristi tunaweza kushinda kila mmoja na kubaki kila wakati kwenye mzunguko wa nuru ya Mungu” , ameandika

Rais wa Tume ya Taasisi za Maish ya kitawa na  vyama vya Kitume katika ujumbe wake wameangazia matukio hayo mawili yanayokwenda sambamba kuwa “Mungu amechagua wengine wetu kuwa, katika safari ya maisha kulingana na mashauri ya kiinjili kwa kufunga nadhiri, ishara ya siku zijazo ya Maisha ya kila mtu. Tunapoadhimisha Siku nyingine ya Kitawa Ulimwengini tumshukuru Mungu kwa wale wote ambao wameitikia wito huu”. "Katika kuingia hekaluni kwa ajili ya Ekaristi, tunakuja ili kuunda jumuiya ya imani, matumaini na upendo, anaandika tema  na kwamba, imani, ambayo huzaliwa kwa kusikiliza Neno la Mungu, inaweza tu kukomaa katika jumuiya.

Jumuiya ni nafasi ya ukuaji na maendeleo yake. Ni katika jumuiya, kati ya watu, kwamba mtu anaweza kupata upendo na kujifunza kupenda kweli. Jumuiya pia ni nguvu yetu wakati sisi ni dhaifu, msaada wetu tunapoanguka, inatusaidia kusonga mbele kuelekea katika malengo yetu pale tunapopoteza matumaini”. Askofu Kiciński amesisitiza katika ujumbe wake kuwa watu waliojitoa ndio ishara ya maana ya maisha ya jumuiya: “Katika jumuiya ya shirika lao, taasisi, katika jumuiya ya Kanisa au mahali ambapo wanafanya huduma yao, bila kujitenga na Hekalu, wanatukumbusha uwepo wa Mungu usiokoma maishani mwetu. Uaminifu wao katika maombi na kazi, katika ulimwengu ambao unadhoofisha uhusiano wa ndoa, familia na kijamii, unachukua maana fulani”, amesisitiza.

Leo watu wengi wanapata shida kubwa ya imani, wengine wanaacha jumuiya ya Kanisa. Katika hali hii, jumuyia za kidini zinakuwa chanzo cha nuru katika ulimwengu uliozama katika giza la utawanyiko; wakati wa hivi karibuni, uliokumbwa na  mikasa ya  janga, imekuwa kwa wengi wetu mtihani wa imani na wakati huo huo jaribio la uwajibikaji kwa pande zote. Katika nafasi hii hakukuwa na ukosefu wa watu waliojitolea ambao walimiminika na kukimbilia kusaidia wahitaji, wagonjwa, wenye mateso, upweke, maskini na waliosahaulika”, amesisitiza. Kwa kuhitimisha Askofu huyo anaadika kuwa: “Tunashukuru watu wote waliowekwa wakfu ambao wanawasindikiza maisha yetu ya kila siku kwa njia tofauti. Tunajua vizuri ni kazi ngapi, ni nyingi sana za kuorodhesha hapa, ambazo zinafanywa katika Kanisa na ulimwenguni. Bwana mwema awalipe kadiri ya kujitolea kwao na bidii yao na baraka za kila siku”.

02 February 2021, 15:53