Tafuta

Vatican News
2020.03.06: Njia ya Msalaba, Yesu anabeba Msalaba 2020.03.06: Njia ya Msalaba, Yesu anabeba Msalaba 

Njia ya msalaba huko Yerusalemu itatangazwa kwa njia ya Mtandao!

Kutokana na hali halisi ya janga la covid-19 kutoweza kuzunguka,msimamizi wa kifransikani katika maeneo matakatifu,Padre Patton ameeleza kuwa katika kwaresima hii,wameandaa Njia ya Msalaba iweze kuingia katika nyumba za waamini na wanahija wote ulimwenguni kwa njia ya mtandao.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kipindi cha Kwaresima, katikati ya janga na ukosefu wa kuzunguka kutoka sehemu moja na nyingine Njia ya Msalaba, itaingia moja kwa moja katika nyumba za waamini kwa njia ya majukwa ya mtandao shukrani kwa mpango unaoitwa:”Hic-On the way of the cross”, uliotayarishwa na usimamizi wa Nchi Takatifu, kuwawezesha waamini na wanahija wote ulimwenguni  kufuatilia, kutoka Yerusalemu, hatua kwa hatua Njia ambayo Yesu aliyopitia miaka elfu mbili iliyopita, akiwa amebeba Msalaba wake mabegani, tangu eneo alilopigwa mijeredi hadi kusulibiwa kwake. “Kwa kuzingatia kwamba mahujaji hawezi kuja kwa Ardhi Takatifu, kutembea katika Njia hii ya Uchungu kila wiki, ambayo wakati wa Kwaresima ilikuwa ni ibada ya kweli  na mamia ya watu kila Ijumaa, tumefikiria kwenda kukutana na mahujaji, tukijua kwamba, ulimwenguni kote, wengi wamegeuza macho yao na mioyo yao kuelekea Yerusalemu”. Amesema hayo Padre Francesco Patton, msimamizi wa nchi Takatifu akizaungumza na Vatican News.

Kwa ufafanunuz hui zaidi amesema : “Hii safari, ambayo inatimizwa kwa kutafakari juu ya vituo vya kiutamaduni vya Njia ya Msalmba Yerusalemu na tafakari ambazo zinaweza kusaidia mahujaji waamini waliotawanyika  ulimwenguni kote kupata maana ya kina ya maisha yao, ya uwepo wao wenyewe, ujumbe wa tumaini katika wakati kama huu mgumu tunaopitia,  mateso na  kwa hiyo, pia usomaji wa masomo ya  mateso katika ufunguo wa Pasaka, kwa sababu basi hii ndiyo maana ya Njia ya Msalaba” amesisitiza Padre Patton.

Video fupi itatolewa kwa kila kituo, kuanzia picha za Yerusalemu, ya matukio mbali mbali yaliyofanyika kwa mujibu wa simulizi za Injili. Video kumi na tatu za vituo kumi na tatu, zilizounganishwa hasa kwenda mahali ambapo Yesu aliishi kupitia njia ya Uchungu, ambapo ni wazi shukrani pia kwa kjitihada na kushirikiana kwa Kituo cha vyombo vya habari cha Kikristo, picha hizo zimetajirishwa na maelezo hayo ambayo yanasaidia kuelewa maeneo, hali ya kiroho ya maeneo na, tunaweza kusema, ukweli wa nini ni siri ya Njia ya Msalaba. Tafakari hiyo itasaidiwa watawa wa Nchi Takatifu, ambao kila mmoja atazungumza kwa lugha yao ya kuzaliwa, kutoka mahali  patakatifu tofauti katika Nchi Takatifu, kama ushuhuda wa ukweli wa kimataifa wa Wafransiskani.

Matumaini ya Padre Patton ni kwamba Pasaka 2021 inaweza kuiishi kwa njia ya amani zaidi kuliko mwaka jana. Nchi Takatifu inaibuka polepole kutoka katika janga la corona, ameeleeza kwamba chanjo zimekuja kufunika kipande kikubwa cha idadi ya watu, lakini nchi bado imefungwa na kukosekana kwa mahujaji na athari kubwa za kiuchumi kwa jumuiya ndogo ya Wakristo ambao maduka yao ya ufundi, hasa Bethlehemu na Yerusalemu, zimefungwa kwa miezi. “Tunachojaribu kufanya kwa mahujaji ameongeza Padre Patton,  ni kusambaza, kwa kadri inavyowezekana, sherehe mbali mbali ambazo zimeunganishwa na makaburi ya binafsi, kwa njia hii mahujaji wa kweli, ambao tayari wametembelea Nchi Takatifu, wanaweza kwenda mahali ambapo imani yao pia imekua na nadhani hii ni muhimu”.

Wakati wa Juma Takatifu, kwa njia hiyo, wakati wote muhimu zaidi utasambazwa, pamoja na Siku Kuu tatu Takatifu za Pasaka kwenye Kaburi Takatifu, na sherehe ya sala takatifu huko Gethsemane na ile inayoitwa mazishi ya Yesu katika kaburi. Kwa mwaka mzima  anahitimisha Padre Patton kutakuwa na mfululizo  wa sherehe, kuwaruhusu waamini kutoka ulimwenguni na mahujaji kuhisi bado wanawasiliana na ardhi hii, kwa matumaini kwamba watarudi hivi karibuni. Njia ya Msalamba itakuwa inafanyuka kila Jumanne na Ijumaa hadi tarehe 30 Machi kuptia vymbo vya habari na mitanza ya Kijani ya Nchi Takatifu.

20 February 2021, 12:51