Tafuta

Vatican News
2020.01.27 Askofu Mkuu Kaigama wa Jimbo Kuu Abuja,Nigeria 2020.01.27 Askofu Mkuu Kaigama wa Jimbo Kuu Abuja,Nigeria 

Nigeria:Kaigama akemea ubaguzi &umaskini ili kukuza upendo &wema

Wakati wa mahubiri ya Askofu Mkuu wa Abuja,Nigeria tarehe 14 Februari amejikita kuelezea machungu yanayokatisha nchi hiyo:Ubaguzi wa kijamii,umaskini,vurugu,utekaji nyara na ufisadi.Amehimiza kila mtu kuziba pengo la kijamii kwa sababu umaskini umefafanuliwa kama ugonjwa wa hatari kijamii ambao unaonekana na kuhalalisha ubaguzi.Anapinga vikali tabaka za kijamii,maana katika Mungu hakuna anayebaguliwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican!

Ubaguzi wa kijamii, umaskini, vurugu, utekaji nyara, ufisadi: hizi ni kurasa zenye uchungu za historia ya kisasa ya Nigeria. Kurasa zilizokumbukwa na Askofu Mkuu wa Abuja, Ignatius Kaigama, katika mahubiri yake, Jumapili, tarehe 14 Februari 2021, akiwa  katika Kanisa kuu la Mama Yetu wa Nigeria. Haya ni matatizo makubwa katika nchi, alisema kiongozi huyo, huku akihimiza kila mtu kuziba pengo la kijamii, kiasi kwamba umaskini umefafanuliwa kama ugonjwa wa hatari kijamii ambao unaonekana  na kuhalalisha ubaguzi. Kwa maana hiyo, ametoa wito wa kuvunja vizuizi kati ya tabaka tofauti za kijamii, kwa sababu katika familia ya Mungu hakuna mtu anayepaswa kubaguliwa, kukataliwa au kutengwa.  Askofu Mkuu pia anatoa ushauri wa nguvu wa kujenga madaraja ya upendo na sio kuta za chuki, na kuonesha huruma hasa kwa wale wanaotendewa vibaya, kunyimwa na kukataliwa na jamii.

Mawazo ya Askofu Mkuu pia yamewaendea wagonjwa wa UKIMWI, walemavu wa akili au wa kimwili, wafungwa wa zamani, wasiojua kusoma na kuandika, walevi, walevi wa madawa ya kulevya, wagonjwa mahututi na wale wote ambao, wanapambana dhidi ya viruso vya corona, wameteseka au wanapata ubaguzi mbaya sana. Yote haya hufanyika kwa sababu ulimwengu unaonekana kumtenga Mungu, ukimchukulia kama mvamizi, badala ya kumwomba Muumba wa mbingu na dunia. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu Kaigama ameonya juu ya dhambi ambayo, amesema “ni mbaya zaidi kuliko ugonjwa wowote wa kuambukiza”. “Kiukweli huharibu roho zetu, hututenganisha na Mungu, huharibu uhusiano wetu na wengine, hutufanya watumwa daima; sisi hatutulii, hutunyima amani ya ndani na hututenganisha na jumuiya ya waamini”,alisisitiza.

Kinyume chake ulimwengu wa kisasa anaskofu Mkuu wa Abuja amebainisha “unahitaji watoa habari njema kama vile uponyaji wa mioyo iliyojeruhiwa, amani, furaha na maendeleo na sio shida za kibinadamu ambazo tunajishughulisha sisi wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya kubwa ya upungufu cha maadili”. Kwa njia hiyo, ushauri wa mwisho uliotolewa kwa waamini ni kukumbatia upendo ambao ni aina kuu ya upendo, bila hiyo, kama vile Mtakatifu Paulo amesema, sisi si kitu. Ikiwa hatuwezi kuonesha upendo wa kweli kwa wengine na kila kitu tunachosema hakina ufanisi na hakija kamilika; kile tunachoamini hakitoshi; kile tunachotoa sio muhimu na kila tunachofanya hakitoshelezi", alihitimisha kiongozi huyo.

18 February 2021, 15:01