Tafuta

Vatican News
Maadhimisho ya Miaka 200 ya Elimu Katoliki nchini Australia Maadhimisho ya Miaka 200 ya Elimu Katoliki nchini Australia 

Miaka 2000 ya Mafundisho ya elimu katoliki nchini Australia!

Maaskofu nchini Australia katika barua yao ya kichungaji wanasisitiza mafundisho ya elimu katoliki nchini humo kuwa ni msingi katika maisha ya Kanisa.Ni katika fursa ya kuadhimisha miaka 200 tangu kuanza kufundisha elimu katoliki kwa vijana wa imani hiyo na huduma katika jumuiya zao.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Katika barua ya kichungaji iliyochapishwa kwenye Tovuti ya Baraza la Maaskofu Australia, maaskofu mahalia wamependekeza kusheherekea miaka 200 ya kuanzishwa kwa elimu katoliki katika shule za nchi hiyo ambapo wanasema ni “hatua muhimu katika maisha ya Kanisa”. Ujumbe wa maaskofu ambao wameuelekezwa kwa wakuu wa mashule, wahudumu, wanafunzi na waamini, unafafanua mipango kamili kwa ajili ya kufanya tukio hilo muhimu na msingi katika maisha ya Kanisa na utambuzi wa mchango wa watawa, makuhani na walei katika kuanzishwa kwa elimu katoliki na jukumu la kipekee ambalo shule katoliki zinajikita nalo kuelimisha na kufundisha vijana wa imani na huduma katika jamuiya zao.

Nchini Australia, leo hii, kuna shule 1,751 katoliki ambazo huwafundisha wanafunzi 768,000 na huajiri watu 98,000  kwa mujibu wa taarifa yao na kwamba, karibu asilimia 40 ya shule  Katoliki ziko nje ya miji mikubwa katika maeneo ya kimkoa, katika jamuiya za vijijini na mbali sana. Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya  Elimu Katoliki, Askofu Anthony Fisher, amewaalika wale wote wanaohusika na elimu Katoliki kutambua hatua hii muhimu katika maisha ya Kanisa: “Tangu mwanzo kabisa wa kufunguliwa rasmi shule ya kwanza Katoliki,  ambayo ilikuwa ina inafundisha  wanafunzi 31 tu katika Mtaa wa Hunter huko Parramatta, shule Katoliki zimekuwa zikielimisha  zaidi ya mmoja kati ya wanafunzi watano wa Australia, na wengi zaidi uhudhuria shule za awali (Chekechea za katoliki, vyuo  katoliki na vyuo vikuu, ” amesema.

Askofu Fisher aidha amebainisha jinsi ambavyo wanayo bahati ya kuwa na shule katoliki katika miji na vitongoji vingi, vyuo mbali mbali na vyuo vikuu katika miji mikuu, ambayo hutoa huduma ya  wanafunzi kutoka  asili tofauti na imani na leo hii sio wote wanatoka katika familia maskini, kama walivyokuwa katika karne ya kwanza ya nusu ya elimu ya katoliki, hata hivyo wanaendelea kukaribisha na kuhakikisha kwamba shule zao pia zinapatikana kwa Waaborigine na wakaazi wa visiwa vya Torres Strait, wakimbizi, walemavu na wanafunzi wanaofadhiliwa ambao wanaishi katika hali duni. Pamoja na familia na parokia, shule katoliki ni sehemu kuu ya mkutano wa Kanisa na vijana na ni sehemu muhimu ya lengo la Kanisa kupitisha imani kwa kizazi kijacho na kufundisha vijana kama washiriki wa baadaye wa jamii ya Australia” ameshuhudia Askofu.

Katika barua ya kichungaji ya maaskofu, hata hivyo, suala dhaifu la unyanyasaji wa watoto pia limezungumzwa,  ambalo limesababisha uharibifu usioweza elezeka katika shule Katoliki na taasisi nyingine kwa miaka iliyopita, lakini zaidi ya yote umeharibu watoto wengi na familia, kama vile vile kuaminika kwa taasisi za Kanisa, pamoja na shule, machoni pa wengi. Dhamana, ambayo katika familia inajengwa tena kwa upande wa maaskofu. Barua ya kichungaji itasambazwa kwa njia ya kielektroniki kwa jumuiya za shule katoliki na wafanyakazi pia inapatikana kwa kupakuliwa kutoka kwenye tovuti ya Tume ya Kitaifa ya Elimu ya Katoliki. Miaka 200 ya elimu ya Katoliki huko Australia itaadhimishwa kwa mwaka wote huu wa  2021  wakiwa na safu za matukio mbali mbali ambapo mipango yote unaweza kupata kupitia link hii: https://www.ncec.catholic.edu.au

19 February 2021, 11:46