Tafuta

Katibu Mkuu mpya wa Baraza la Maaskofu nchini Ujerumani Bi  Beate Gilles Katibu Mkuu mpya wa Baraza la Maaskofu nchini Ujerumani Bi Beate Gilles 

Amechaguliwa Katibu mkuu mpya wa Baraza la Maaskofu Ujerumani!

Kwa mara ya kwanza mwanamke anashika nafasi kuu katika Kanisa nchini Ujerumani.Huyo ni Bi Beate Gilles ambaye amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Ujerumani wakati wa Mkutano wao Mkuu kwa njia ya mtandao kuchukua nafasi iliyoachwa na Padre wa Kijesuit Hans Langendörfer aliyeshika nafasi ya ukatibu huo kwa miaka 24.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mtaalimungu Bi Beate Gilles, mwenye umri wa miaka 50 amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Ujerumani(Dbk) katika Mkutano wao mkuu uliofanyika Jumanne tarehe 23 Februati 2021 kwa njia ya Mtandao. Ni kwa mara ya kwanza mwanamke anachukua nafasi kama hiyo nchini humo, akichukua nafasi iliyoachwa na Mjesuit, Padre Hans Langendoerfer, ambaye amejihudhuru baada ya miaka 24 ya uongozi wake. Mtaalimungu huyo, Bi Gilles kwanza alikuwa mkuu wa Kitengo cha watoto, vijana na familia cha Jimbo la Limburg, na sasa kama mtangulizi wake, anachukua mwelekeo huo katika Shirikisho la Majimbo katoliki ya Ujerumani.

Askofu Georg Baetzing, Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ujerumani (Dbk), wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati ufuguzi wa mkutano kwa njia ya mtandao amezungumzia juu ya katibu mpya, kwamba anachukuliwa kama mtaalimungu mwenye nguvu, aliyejumuishwa sana katika miundo mbalimbali ya Kanisa Katoliki na amejaliwa ujuzi bora wa kuratibu.

Bi Beate Gilles mwenyewe hata hivyo amesema jinsi alivyoguswa na jukumu hilo jipya na kwamba yuko tayari katika shughuli hiyo mpya,akisisitiza hatua za kujikita nazo na zenye changamoto za Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, mahali ambapo katika muktadha kwa ujumla kuna shauku ya mabadiliko, ambapo wameanza njia ya kisinodi, na kwamba ni mchakato wa mageuzi Katoliki. Bi Gilles ni mtaalam wa Mawasiliano na shida za kijamii na za kazi,  ataanza  jukumu la nafasi yake mpya kuanzia tarehe 1 Julai 2021.

Katibu mkuu wa baadaye wa Baraza la Maaskofu Ujerumani vile vile amesisitiza kuwa rasilimali za Kanisa Katoliki nchini Ujerumani zinaendelea kupungua, kwa maana hiyo itakuwa muhimu kuzingatia mizizi ya Kanisa na malengo yake, ambayo ni kazi muhimu kuanza mara moja.

24 February 2021, 16:29