Tafuta

Vatican News
2020.12.17 Maaskofu Katoliki nchini Ghana na Balozi wa kitume 2020.12.17 Maaskofu Katoliki nchini Ghana na Balozi wa kitume  

Ghana,Kwaresima: Maaskofu wanatoa wito wa mapatano,haki &amani!

Baraza la Maaskofu nchini Ghana wanaalika waamini kuongeza nguvu ya mahusiano na Mungu,binadamu na kazi ya uumbaji wakati huu wa kioindi cha Kwaresima ambacho kinatoa fursa kamili ya kuchota huduma ya kweli ya Mungu.Ni kipindi ambacho kinafungua mioyo katika tumaini la kuwa tumependwa daima licha ya kuwa sisi ni wadhambi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni wito wa nguvu wa kutia moyo katika kuhamasisha mapatano, haki na amani unaoneshwa katika barua ya kichungaji ya Kwaresima iliyochapishwa na Baraza la Maaskofu nchini Ghana (Gcbc). Wakiwaalika waamini kuweka nguvu yao katika uhusiano na Mungu, ubinadamu na kazi ya Uumbaji, Maaskofu wanasisitiza kuwa Kwaresima inatoa fursa kamili ya kuchota huruma ya kweli ya  Mungu. Ni kipindi ambacho kinafungua mioyo katika tumaini la kuwa tumependwa daima, licha ya kuwa sisi ni wadhambi. Kwa maana hiyo maaskou wanashauri kufanya mazoezi ya sala, kujinyima, kufunga, kutoa sadaka na kukaribia katika sakramenti ya kitubio.

Siku arobaini zilizotangulia Pasaka zinawakilisha, kwa dhati wakati maalum wa kupatanishwa na Mungu;  Lakini sio hayo tu: “waamini wanaalikwa kujipatanisha wao kwa wao, kwa sababu upatanisho wetu na Mungu haujakamilika bila hiyo na wenzetu. Kwa maana hiyo ni  lazima ihusishe katika kategoria zote: maaskofu, makuhani, dini, wakuu ya serikali, viongozi wa kisiasa na vyama, wenzi wa ndoa, wazazi na watoto”. Maaskofu wanasisitiza kwamba waamini wafungue mioyo yao  kwa watu wote familia, marafiki, kaka, dada na pia kwa maadui  na kwa walewote ambao wameumizwa na maneno, vitendo na au kutotimiza wajibu. Wakati huo huo, maaskofu wanapendekeza, kwa kipindi cha Kwaresima, kuwa na umakini zaidi kwa wale walio katika mazingira magumu zaidi katika jumuiya, kwani huruma, ambayo ni moyo wa upatanisho na wengine, pia inajumuisha kusaidia wale wanaohitaji. “Ni lazima kukumbuka  kutekeleza kwa vitendo matendo ya kibinadamu na ya kiroho ya hudum”a na wakati huo huo wanawaomba waamini wasifuate  ulimwengu huu, bali waruhusu wabadilishwe ili kuweza kutambua mapenzi ya Mungu na yale mema.

Katika sehemu nyingine muhimu ya ujumbe huo wa kichungaji, imejikita katika kazi ya utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. Katika kipindi cha Kwaresima waamini wanaweza kuchukua fursa ya kujipatanisha na kazi ya maumbile, wakitafakari juu ya vitendo vinavyoharibu mazingira, kama vile utupaji ovyo wa taka, hata za viwandani; shughuli za migodi ndogo ya dhahabu haramu; ukataji miti, uchafuzi wa mazingira wa rasilimali maji na aina zote za uharibifu wa mazingira. Kwa sababu hiyo, Kanisa Katoliki la Ghana linasisitiza kwamba “dunia ndiyo makao yetu ya pamoja. Na bado, kwa matumizi yetu ya kutowajibika, tumeisababishia uharibifu mwingi”. Badala yake, kwa kuwa mazingira matakatifu hutufanya kuwa na afya njema na furaha”. Waamini wanahimizwa kutunza mazingira kama amabvyo wangejitendea wenyewe. Uongofu wa kiekolojia ni kanuni msingi iliyosisitizwa  na Baraza la Maaskofu nchini Ghana (Gcbc), mchakato ambao unahitaji kutambuliwa wazi kuwa jukumu lao wenyewe, na jirani zo, kwa kazi ya umbaji na kwa Muumba na maombi ya huruma ya Mungu kwa dhambi hizo dhidi ya Uumbaji ambazo bado szinaonekana kutotambuliwa. Ujumbe wa maaskofu unaendelea,kwamba Kwaresima  pia ni wakati mzuri wa kukuza haki na amani, kwa sababu haiwezekani kuwa na upatanisho wa kweli kama kuna ukosefu wa haki. Kwa maana hii haki itakuzwa kibinafsi na kitaifa, kwa kuchunguza dhamiri nafsi huku wakijua kuwa wana hatia ya vitendo vya udhalimu, na ili kuchukua hatua zinazofaa kufikia amani ndani ya jamii zao. Kutokana na mtazamo huu pia wanapata jitihada za kulifanyia kazi ili kuwa na  taifa lenye amani.

Kifungu kirefu cha Ujumbe wa Kwaresima kutoka kwa Maaskofu wa Ghana kimetengwa kwa ajili ya janga la Covid-19 ambalo limesababisha visa zaidi ya 78,000 na zaidi ya vifo 560 nchini humo.  Virusi vya Corona havijaumbwa na Mungu, wanaandika katika ujumbe wao na wala janga la Yule aliyetupatia Mwanawe wa pekee kwa ajili ya wokovu wetu.  Kwa hakika, katika janga hilo linatupatia mafundisho matatu; kwamba vitu vya kidunia sio vya milele; kwamba katika ukimya, kama ule wa karantini (lockdown), unaweza kusikia vizuri sauti ya Mungu na kwamba jwangwa la kiroho la Covid-19 ni mahali ambapo tunaomba  kwa Mungu mpaji. Maaskofu aidha wameshauri waamini watu wa Mungu kuendelea kuheshimu itifaki za usafi wa mazingira, hasa katika maeneo ya ibada, mashuleni , maofisini, madukani, na mahali popote  katika kipindi cha “Kwaresima mwaka huu na sherehe ya Juma Kuu  Takatifu. Hati hiyo inahitimishwa kwa sala kwa Bikira Maria mbarikiwa na kuombea taifa zima.

18 February 2021, 14:53