Tafuta

Nchini Sudan Kusini wametengeneza note mpya ili kuondoa  sarafu ndogo kuanzia 1, 2, 5, 10, 20, 25, 50, 100 na 500 Nchini Sudan Kusini wametengeneza note mpya ili kuondoa sarafu ndogo kuanzia 1, 2, 5, 10, 20, 25, 50, 100 na 500  

Fedha mpya yaanzishwa na serikali Sudan Kusini

Serikali nchini Sudan Kusini imeanzisha noti mpya zenye thamani kubwa. Kwa upande wa Kanisa nchini wanabainisha kwamba ni kieleleza cha ufisadi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 4 Februari 2021 Benki Kuu Nchini Sudan Kusini imeanzisha, noti mpya za pauni elfu moja mahalia (sawa na karibu euro 6). Katika kuelezea uchaguzi huo gavana wa Benki yenyewe, amesema ilikuwa ni hitaji la kupunguza gharama zote za uchapishaji wa noti ndogo na nafasi ya kuhifadhi. Nchini Sudan Kusini, kiukweli, ina sarafu sawa na 1, 2, 5, 10, 20, 25, 50, 100 na 500 za paundi, ingawa mbili za kwanza zilitoweka kutoka katika mzunguko mnamo 2014, kwa sababu ya mfumuko wa bei.

Kwa upande wa Kanisa Katoliki linasema kushangazwa na uamuzi huu,  hasa, Askofu Erkolano Lodu Tombe, wa jimbo la Yei, ambaye amezungumzia juu ya chaguo ambalo linaangazia ufisadi ulioenea nchini  humo na kutofaulu kwa uchumi wa kitaifa. “Noti kubwa sio suluhisho sahihi kwa shida ya uchumi, lakini ni onesho tu la hali inayozidi kuwa mbaya siku hadi siku”, amesema Askofu Tombe.  “Katika masoko fedha hazizunguki kwa sababu kati ya mamlaka kuna watu mafisadi ambao wanazishikilia peke yao, na kusababisha maafa halisi katika kiwango cha kitaifa” amebainisha.  Wakati huo huo, mbele ya umaskini uliokithiri nchini humo , Askofu Tombe amewahimiza waamini kuwa na ujasiri, bila kuangukia katika ijambazi na wizi. “Lazima tupambane na kidogo tulicho nacho. Mungu atafanya yote “, amesisitiza.

Ikumbukwe kwamba, kulingana na Uwazi wa Kimataifa (Trasparency International), shirika lisilo la kiserikali ambalo kila mwaka linachapisha ripoti juu ya ufisadi katika kiwango cha ulimwengu, mnamo 2020, Sudan Kusini ilikuwa katika nafasi ya pili katika orodha ya nchi zilizo na ufisadi zaidi duniani, ikitanguliwa na Somalia. Kwa kuongezea, Covid-19 imesababisha visa zaidi ya elfu 6 kwa jumla na zaidi ya vifo 80 nchini. Lakini janga hilo pia limekuwa na athari kubwa katika sekta ya uchumi, kwa sababu sehemu kubwa ya Pato la Taifa linategemea usafirishaji wa mafuta, mahitaji ambayo bei zake zimeshuka wakati wa dharura ya kiafya.

21 February 2021, 11:34