Tafuta

Vatican News
Nchini Burkina Faso na Niger,zaidi ya watu nusu milioni wamekimbia makazi yao kutokana na ukosefu wa usalama unaohusishwa na mashambulio ya kigaidi. Nchini Burkina Faso na Niger,zaidi ya watu nusu milioni wamekimbia makazi yao kutokana na ukosefu wa usalama unaohusishwa na mashambulio ya kigaidi.  (SESAME PICTURES)

Burkina Faso:inahitaji kukabiliana na uhamiaji wa ndani kwa haraka!

Maskofu nchini Burkina Faso wanasisitiza juu ya dharura ya kukabiliana nayo hasa katika masuala ya wahamiaji wa ndani ili kuzuia mivutano ya ndani.Wamebainisha hayo katika Mkutano wao wa pili wa mwaka 2020-21.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Hali ya usalama bado inatia wasiwasi katika maeneo kadhaa, licha ya hali ya utulivu, Maaskofu wa Burkina Faso na Niger wanasema katika taarifa ya mwisho ya mkutano wao wa pili wa mwaka 2020-2021, ambapo wanasisitiza sana suala ambalo halijasuluhishwa wakimbizi wa ndani ambapo wanasisitiza hatari ya kusababisha mivutano zaidi, ikizingatiwa idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani ambao kuishi pamoja na wale waliowakaribisha na kuwa  sio rahisi kila wakati. Licha ya kuhakikishiwa na serikali, kulingana na Maaskofu ukweli juu ya nyanja unaonesha kuwa wanahitaji kuhakikishiwa na kuhisi kulindwa na viongozi wenye uwezo .

Nchini Burkina Faso na Niger, zaidi ya watu nusu milioni wamekimbia makazi yao kutokana na ukosefu wa usalama unaohusishwa na mashambulio ya kigaidi. Mashambulio ya vikundi vya kigaidi, ambayo yanakumbusha ya Al Qaeda kama ISIS, bado yanaendelea. Tarehe 18 Februari  watu wasiopungua 18 walipoteza maisha katika mashambulio tofauti nchini Mali na Burkina Faso. Shambulio hilo nchini Burkina Faso lilitokea asubuhi, kati ya miji ya Markoye na Tokabangou, ambapo watu wengine walikuwa wamevamiwa wakielekea Dolbel, katika nchi jirani ya Niger. Watu wanane walifariki na tisa walijeruhiwa, mmoja wao alikufa kutokana na majeraha

Ili kuruhusu kuishi kwa urahisi kati ya makazi ya watu waliokimbia makazi yao na yale ya wenyeji, Maaskofu wanapendekeza kuimarishwa mazungumzo kwa ujumla na kampeni ya uhamasishaji juu ya kuishi pamoja na viongozi tofauti. Inahitajika pia kufanya kazi kudhibiti suala la unyanyapaa, hasa katika maeneo yasiyo salama ambapo kuanza kwa shughuli hiyo hufanyika hatua kwa hatua. Ili kufanya hivyo, watu wanaalikw kuwa ushirikiano na vikosi vya ulinzi na usalama, na waamini kuendelea kuombea amani ya Burkina Faso na Niger. Miongoni mwa watu wanaonyanyapaliwa ni wachungaji wa Peuls, wanaochukuliwa kuwa wanashirikiana na vikundi vya jihadi ambavyo vinafurika katika ukanda wote wa Sahel. Wakati wa kazi yao, Maaskofu walitembelewa na Iman mkuu wa Fada, Aboubacar Kina, ambaye aliomba Baraza la  Maaskofu waombee amani na mshikamano wa kijamii huko Burkina Faso. Iman amesisitizia juu ya  uhusiano mzuri wa kidini kati ya jumuiya za Kikristo na Waislamu tangu miaka ya 1960.

21 February 2021, 11:58