Tafuta

Vatican News
2020.11.11 Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Zambia Askofu George Lungu. 2020.11.11 Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Zambia Askofu George Lungu. 

Zambia:Maaskofu watoa wito wa kupamba na umaskini kwa njia zozote!

Katika barua, yake Rais wa Baraza la Maaskofu,nchini Zambia,Askofu George Cosmas Zumaile Lungu,amealika serikali kuondoka katika eneo lake la faraja na ili kuangalia kilio cha kimya cha watu wake.Anawashauri watu wote kupambana na umaskini kwa kila njia na kila aina ya zana.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wasiwasi juu ya kuanguka kwa uchumi na athari kwa idadi ya watu maskini imeonesha siku za hivi karibuni na maaskofu katoliki wa Zambia. Katika barua yake Rais wa Baraza la Maaskofu, Askofu George Cosmas Zumaile Lungu, wa jimbo katoliki la Chipata, amealika serikali kuondoka katika eneo lake la faraja na kuangalia kilio cha kimya cha watu wao. Deni la nchi hiyo, kiukweli, limezidi maradufu katika miaka mitano iliyopita, kutoka dola bilioni 4.8 mnamo 2014 hadi bilioni 11.2 mnamo 2019. Zambia imepanda kwa kiwango cha juu zaidi katika miaka minne iliyopita (asilimia 17.4), kwacha (sarafu ya ndani) imepungua kwa asilimia 33 dhidi ya dola. Bei za watumiaji ziliongezeka kwa asilimia 16 zaidi ya mwaka uliopita.

Yote haya yamesababisha, kama ilivyoandikwa katika ripoti ya hivi karibuni ya ya “Mtandao wa Haki na Ikolojia ya Kijesuit” (Jena), “kudhoofika haraka uchumi ambao unahatarisha maisha ya kiuchumi na kijamii ya raia wa kawaida, hasa maskini, waliotengwa na wanyonge”. Kulingana na kituo cha utafiti cha Wajesuit, upungufu wa fedha, kiwango cha mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya sarafu vinaongezeka wanabainisha Jena, na sio mara ya kwanza Zambia kujikuta katika shida ya deni kama hilo. Serikali lazima ijifunze kutokana na uzoefu huu na kupata suluhisho la kudumu ili kuepuka kuwa katika hali hii kila wakati”, wanashauri.

Zambia, ni moja ya wazalishaji wakuu wa shaba ulimwenguni,lakini imeingia katika mgogoro wa deni wakati janga la covid-19, pamoja na kusababisha vifo vya zaidi ya 400 na zaidi ya 21,000 walioambukizwa, pia iliharibu uchumi wake na ikadhihirisha deni lake la umma kama lisiloweza…. Katika suala hili, Mtandao wa Haki na Ikolojia wa Kijesuit  wa Afrika unawataka watawala kuweka utaratibu wa uwazi wa kupunguza deni na mkakati wa uendelevu. Mtandao huu (Jena) unasema kuwa ukomavu wa uhuru wao na demokrasia utapimwa na lengo halisi ya viongozi weo kufikiria juu ya faida ya wote badala ya kujitajirisha wao wenyewe.

Mara kadhaa, maaskofu wamejaribu kuhamasisha sio tu mamlaka za serikali, bali pia maoni ya umma, kwa masuala muhimu ya nchi na sehemu dhaifu za idadi ya watu. “Kila mtu angepaswa kula, kati ya sasa na mwisho wa Desemba 2020” walikuw wamethibitisha mwezi Septemba uliyopita kwamba ikiwa kila mmoja wetu angeweza kutoa hata sawa ya senti 26 za dola ya kimarekani kila mwezi katika parokia moja nchini kiote Zambia”.

05 January 2021, 13:25