Tafuta

Vatican News
PALESTINIAN-RELIGION-CHRISTIANITY-CHRISTMAS PALESTINIAN-RELIGION-CHRISTIANITY-CHRISTMAS  (AFP or licensors)

Yordani:Patriaki Pizzaballa ashukuru Mfalme,Taasisi na makanisa dada kwa ukarimu!

Katika kuhitimisha ziara yake rasmi nchini Yordani tangu tarehe 7 hadi 21 Januari,Patriaki Pizzaballa ameshukuru Mfalme Abdullah II Ben Al Hussein,Taasisi zote na Makanisa dada kwa ukarimu wao waliomuonesha kwa siku hizo.Anawapongeza kwa ushirikiano na kuishi na umoja na udugu kama mfano ulimwenguni.Ameahidi kukumbuka nchi hiyo kila siku katika sala zake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika hitimisho la ziara yake ya kwanza rasmi katika nchi ya Yordani, Patriaki Pierbatista Pizzaballa wa Upatriaki wa  Yerusalemu, iliyoanza tangu tarehe 7 hadi 21 Januari 2021 ametoa shukrani nyingi kwa makaribisho aliyopata. Katika taarifa iliyowa cha na Ofisyai usimamizi wa Kilatino huko Amman, Patriaki Pizzaballa anashukuru awali ya yote Mfalme Abdullah II Ben Al Hussein, ambaye alizungumza naye katika mkutano kwa njia ya mtandao na kupongeza Kanisa la kitaltino kwa kile ambacho kinaendelea kufanyika huko Yerusalemu kwa ushirikiano na Makanisa dada.

Patriaki amekumbusha hata mahusiano  ya urafiki kati ya Mfalme na Papa Francisko, kwa maana hiyo hata kutoa shukrani kwa mfalme wa Ghazi Ben Mohammad, Mfalme  El-Hassan Ben Talal, na Mwenyekiti wa Seneti, Faisal Al-Fayez, Spika wa Bunge  Abdul Mon’em Odat na serikali ya Yordani kwa ujumla  kwa juhudi kubwa ambazo zimetimizwa katika kuandaa ziara yake na mikutano katika Uflame huo wa Hashemite.

Kwa mujibu wa Patriaki Pizzaballa ameelezea jinsi alivyochagua kuadhimisha Misa yake ya kwanza katika Eneo la Ubatizo wa Yesu kwa ajili ya umuhimu unaowakilisha eneo hilo na kuwaalika mahujaji na waamini waweze kutembelea mara tu janga litakapokuwa limekwisha. Akiwageukia maaskofu, mapadre na waamini walei wote amebanisha kufurahiwa na  mshikamano na ushirikiano kati ya familia moja kubwa ya Yordani na kusisitiza ulazima wa kuendelea kuhifadhi umoja huo.

Patriaki wa Kilatino wa Yerusalemu  kwa mantiki hiyo amesifu maelewano yaliyopo kati ya raia wa Yordani na amebainisha kuwa Yordani imekuwa mfano katika  ulimwengu kuhusu  mshikamano kati ya Wakristo na Waislamu. Shukrani za Patriaki Pizzaballa pia zimewaendea vyombo vya habari mahalia vya  Kiarabu na  kimataifa ambavyo vimeweza kuripoti kila wakati juu ya ziara yake huko Yordani na kwa Makanisa dada, ambayo, katika Tukio la Wiki ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo, waliandaa ziara ya Patriaki wa   Kilatino wa Amman kukutana naye na kushiriki katika Misa iliyoadhimishwa mahali pa Ubatizo wa Yesu. Hatimaye Patriaki amesisitizia hitaji la mipango mingi iwezekanavyo ya kufanikisha umoja wa Kikristo huku akitoa salamu zake  kwa familia yote ya  Yordani, chini ya uongozi wenye busara wa Hashemite, kwa serikali na kwa watu wa Yordani akisema: “Nitakumbuka na kutaja  daima Yordani katika maombi yangu ya kila siku, hasa katika siku hizi za ugonjwa wa Covid-19, pia kwa  ajili ya hudumu wa matibabu ya Ufalme na  ulimwengu kwa ujumla”.

23 January 2021, 12:39