Tafuta

2021.09.09 Eneo la Qasr al-Yahud kurudishwa mikononi mwa usimamizi wa Ndugu wadogo wafranciskani huko Nchi Takatifu 2021.09.09 Eneo la Qasr al-Yahud kurudishwa mikononi mwa usimamizi wa Ndugu wadogo wafranciskani huko Nchi Takatifu 

Nchi Takatifu:Baada ya miaka 54 misa ya Ubatizo imefanyika eneo Yordani!

Wafranciskani wameweza kuadhimisha Dominika ya Ubatizo wa Kristo juu ya mto Yordani mahali alipobatizwa na Yohane Mbatizaji.Ni katika eneo la Qasr al-Yahud ambalo baada ya kugeuka kuwa kambi ya vita tangu mwaka 1967,sasa linarudia tena kuwa mahali pa amani na kwa ajili ya maombi.Kwa mujibu wa Padre Ibrahimu Faltas amesema ni siku moja ya kihistoria.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Ni kwenye ukingo wa mashariki wa Yeriko katika mlango wa mahali ambapo ubatizo uliopokelewa na Yesu mikononi mwa  Yohana Mbatizaji kwenye Mto Yordani. Wafransiskani kwa kawaida hutimiza hija yao kila mwaka kwenye eneo hilo  linalojulikana kama Qasr al-Yahud  yaani ngome ya Kiyahudi, karibia  tangu mwaka 1641. Lakini tangu 1967, kwa sababu ya Vita vya Siku Sita, eneo lote lilikuwa limefungwa kwa mahujaji na watalii. Eneo hilo baadaye likawa uwanja wa mabomu kwa hekta 55 na likabadilishwa kuwa eneo la kijeshi.

Kazi ya kuondoa mabomu

Ni kuanzia mwaka wa 2000 tu, katika tukio la hija ya Jubilei ya Papa Yohane Paulo II ya kwenda Nchi Takatifu, ilifunguliwa sehemu ndogo tu ya eneo hilo. Lakini baadaye, baada ya vita vya Intifadha ya pili, ilifungwa tena. Katika miaka ya hivi karibuni, operesheni ndefu ya kuondoa mabomu ya ardhini imetekelezwa katika eneo lote la Qasr al-Yahud. Kwa idhini ya mamlaka ya Israeli na Palestina, jumla karibu  mabomu 4,000 ya kutegwa yameondolewa. Katika kukamilisha kazi hiyo ilikuwa shirika la kibinadamu la Uingereza “Halo Trust”, lililobobea katika masuala haya. Na baada ya zaidi ya miaka 50, Kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji limekabidhiwa katika Usimamizi wa Nchi Takatifu.

Siku kuu ya Ubatizo

Jumapili tarehe 10 Januari 2021, katika Siku kuu ya Ubatizo wa Bwana, kuanzia asubuhi saa tatu, kumekuwa na safu ya matukio mbali mbali, iliyohudhuriwa na watu kadhaa kwa sababu ya janga la virusi, lililoongozwa na Usimamamizi wa Nchi Takatifu. Baada ya kuwasili kwenye Mto Yordani, maandamano na Misa ya sherehe vimefanyika. Tukio hilo  pia imejumuisha hija katika Mlima wa Majaribu.  Katika Siku hii maneno ya Injili yamesikika: “Basi Yesu kutoka Galilaya alikuja Yordani kwa Yohane, ili abatizwe na yeye. Lakini Yohane alitaka kumzuia, akisema: Je! Ni mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Lakini Yesu akajibu: “Acha kwa sasa, kwa sababu inafaa tutimize haki zote”. Baadaye akamruhusu afanye. Mara tu baada ya kubatizwa, Yesu alitoka majini; na tazama, mbingu zilimfungukia na akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa akija juu yake. Na hapo ikasikika sauti kutoka mbinguni iliyosema: Huyu ni Mwanangu, mpendwa; niliyependezwa naye”.

Padre Faltas:Ni siku ya kihistoria

Kwa hakika baada ya miaka 54 Wafransiskani wa Nchi Takatifu wameweza kufanya kumbu kumbu ya ubatizo wa Yesu katika eneo ambalo Yesu alibatizwa kwa njia ya mikono ya Yohane mbatizaji kwenye mto wa Yordani. Kwa mujibu wa Padre Ibrahim Faltas, mfransikani katika maeneo hayo Matakatifu amesema, imekuwa siku kuu, na  siku ya kihistoria kwa ajili yao ambayo hawakuwahi kusahau kamwe maeneo hayo matakatifu, hata wakati wa vita au wakati wa sababu nyinginezo ambazo zilisababisha kupoteza maeneo hayo. Misa ya Jumapili imeongozwa na Padre Francesco Pattoni, msimamizi wa Nchi Takatifu na  kuudhuriwa pia na Balozi wa kitume wa Yerusalemu na mabalozi kutoka Italia, Uhispania, Ubelgiji, na Ufaransa. Na wameudhuria ndugu wadogo wafransiskani tu ili kuadhimisha siku kuu hiyo kwa njia hiyo ni karibu watu 50 tu kutokana na sababu za virusi vya corona.

Ni furaha kubwa kwa wafranciskani kurudishiwa maeneo matakatifu

Ni furaha kubwa kurudi katika maeneo hayo matakatifu na ambayo imekuwa ni baraka ya kubariki Conventi kwa mara nyingine tena, ambayo amesema wamakabidhiwa miezi mitatu iliyopita. Ni nyumba ya watawa nzuri sana. Jumapili imekuwa siku ya sherehe, ya furaha kwa Wafransiskani wote, amesisitiza. Mwaka 2020 ulikuwa mwaka mgumu kwa kila mtu kutokana na janga la virusi vya corona na mambo mengine mengi. Lakini kwa kadiri ya wao Wafransisko wanavyohusika, wanaweza kusema kwamba nyumba hiyo ya watawa na chuo cha Aleppo vimerudi kuwa mikononi mwao. Kwa mujibu wa Padre huyo aidha  amesema Mwaka mpya, na siku kuzaliwa tena, hii ina maana ya ubatizo. “hamuwezi kufikiria ni kwa namna gani furaha kubwa tuliyo nayo wafransiskani katika Nchi Takatifu. Lakini pia hata kwa wafransiskani wote ambao wametoa maisha yao kwa ajili ya maeneo hayo. Amefikiri kwamba hata wale walioko mbinguni hana shaka kwamba wanafurahi kuona konventi  hiyo inarudi mikononi mwa usimamizi wa Nchi Takatifu.

10 January 2021, 16:01