Tafuta

Kusafisha makazi kwa ajili ya kuzuia virusi vya corona nchini Senegal Kusafisha makazi kwa ajili ya kuzuia virusi vya corona nchini Senegal  

Wasiwasi wa maaskofu Senegal juu ya kuzuka aina mpya ya Covid-19!

Kufuatia na kuzuka kwa aina mpya ya Covid-19,Maaskofu nchini Senegal wanaonesha wasi wasi wao na kwamba zinahitajika nguvu za pamoja katika kudhibiti janga hili.Waaamini waendeleea kuwa makini kwa kufuata kanuni za kiafya zilizowekwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Aina mpya ya Covid-19 imeleta wasi wasi hata kwa maaskofu katoliki nchini Senegal, ambao siku za hivi karibuni wamefanya mkutano na kujadili pamoja na Rais Macky Sall na Waziri wa Afya nchini humo. Wakati wa mkutano wao wa siku mbili kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari za Afrika (ACI), maaskofu wamesisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za pamoja kwa ajili ya kuthibiti kusambaa zaidi kwa namna ya pekee maambukizi hayo na wamethibitisha kwamba wako tayari kustisha maadhimisho ya liturujia na waamini ikiwa italazimika kufanya hivyo.

“kila mmoja wetu ni muwajibikaji wa mwenendo wa kaka na dada” amethibitisha Askofu Mkuu wa Dakar, Benjamin Ndiaye, na ambaye amewashauri waamini wote kutopuuza hatari, hivyo kuendelea kuheshimu kanuni za usafi za kiafya. Na kwa niaba ya maaskofu wote, Askofu Mkuu Ndiaye zaidi amemshukuru Rais Sall kwa hatua alizochukua kwa ajili ya kuthibiti janga. Na kwa Waziri wa Afya, Maaskofu wameomba ushirikiano wa kina kati ya Serikali na majengo 75 ya kiafya ya Kanisa Katoliki nchini humo katika mapambano dhidi ya janga hili baya.

Serikali ya Senegal, ilikuwa imelegeza vizuizi vya kuzuia maambukizi ya Covid-19 mwezi Julai mwaka jana, mara baada ya kuona kushuka kwa kesi za maambukizi, lakini maaskofu walipendelea kusubiri kwa usalama zaidi hadi tarehe Mosi Novemba 2020, kufungua Makanisa kwa ajili ya ibada kwa umma, huku wakishauri waamini waendelee kuwa wavumilivu katika imani na matumaini. Wimbi la pili sasa la maambukizi mapya yaliyorekodiwa wiki hizi za mwisho, yanaweza kusukuma mamlaka ya nchi kuweka tena hatua za vizuizi na maaskofu hawakukosa kueleza uwezekano huo wa kufunga makanisa yao kwa upya.

20 January 2021, 14:05